Wednesday, August 1, 2012

MTANZANIA MKAZI WA MBINGA RUVUMA ATENGENEZA GARI

GARI aina ya Canter -Kanyalika lililotengenezwa  na Castory Turuka kwa kutumia mabati chakavu.
 GARI hilo likiwa barabarani maeneo ya Mbinga Mkoani Ruvuma,hapa ni taswira ya mbele linavyoonekana.
 Mtengenezaji wa gari hilo Bw. Turuka,anasema hiyo ni gari yake ya nne kuitengeneza na kwamba bado linaendelea kutengenezwa hivyo gharama ya gari hiyo bado hajaitaja.
 HAPA akiwa ndani ya gari hiyo,anasema mara ya kwanza alitengeneza gari ndogo aina ya Kanyalika Toyota Hilux ambayo anaiuza kwa shilingi milioni 5.
 TASWIRA ya Gari hiyo inavyoonekana kwa mbele.Bw. Turuka anasema anahitaji Serikali imuwezeshe ili aweze kutengeneza magari mengi zaidi.
HAPA inapakia mizigo.

No comments:

Post a Comment