Thursday, October 18, 2012

TATIZO LA MAJI LATIKISA SONGEA,NDOO MOJA YAUZWA SHILINGI 500

Mtoto akchezea maji huku pembeni wazazi wake wakifua kwenye maji ya mto Mfaranyaki
 Kutokana na tatizo la maji wananchi wamekuwa wakitumia maji ya mto kwa shughuli mbalimbali
 Hapa ni katika mto Mfaranyaki,shughuli  zimepamaba moto.
Foleni ya maji ni katika Bomba la Hospitali

 Hapa ni Mkokoteni linatoka mbali kutafuta maji.
 Mikokoteni katika foleni ya maji Songea.
Jamaa akisubiri  maji na Mkokoteni wake.

KIONGOZI WA KUNDI LA UAMSHO LA KIISLAMU APOTEA ZANZIBAR

 Na Mwandishi wetu na Mashirika ya habari
 Zanzibar
Ramani ya Zanzibar

Wasiwasi umetanda kisiwani Zanzibar kufuatia kutoweka kwa kiongozi wa kidini Sheikh Farid Hadi Ahmed.
Watu wawili wametiwa nguvuni waliohusika na maandamano na ghasia zilizosababisha uharibifu mkubwa kisiwani humo.
Kuna hofu kuwa kiongozi huyo huenda amekamatwa na polisi na anazuiliwa Tanzania bara kutokana na kuwa amepinga utawala wa chama tawala cha Tanzania bara CCM.
Kwingineko, hapo jana polisi nchini Tanzania walimkamata mhubiri mwenye utata anayetuhumiwa kwa kuchochea vurugu wiki jana , na kusababisha maandamano mapya.
Kulingana mkuu wa polisi, Suleiman Kova ,Sheikh Ponda Issa Ponda, mkuu wa Jumuiya ya waislamu, vuguvugu ambalo halitambuliki na serikali ya Tanzania, alikamatwa kwa kuchochea vurugu.
Kukamatwa kwa Sheikh Ponda, mini Dar es Salaam, inakuja baada ya kukamatwa kwa watu 31 waliozua vurugu na kupora mali ya watu wakati waandamanaji walijawa na ghadhabu na kuandamana wiki jana wakiharibu makanisa kadhaa mjini humo.
Maandamano ya wiki jana yalisababishwa na tetesi kuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na miwili aliikojolea Quran.
Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake kufanya maandamano kinyume na sheria na kutoa wito wa ghasia na umwagikaji damu mjini Dar es Salaam na nchini kote.
CHANZO-BBC

MBUNGE KENYA MATATANI KWA UCHOCHEZI



 Kenya
Sheikh Mohammad Dor

Wakati  Tanzania kukiwa na machafuko ya kuchoma moto malkanisa huki Kenya  Kiongozi mmoja mkuu wa kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni mbunge mteule ameshtakiwa kwa kuchochea ghasia.

Mbunge Sheikh Mohammad Dor alisema kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani.

Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo Omar Mwamnuadzi.
Sheikh Dor alikamatwa jana jioni baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza kufadhili vuguvugu hilo, ingawa aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka ya uchochezi.
Wanachama wa MRC wanaotaka kujitenga na Kenya

Kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe kumi na tatu mwezi Novemba.
Sheikh Dor ambaye amelaani msako unaoendelea wa polisi dhidi ya kundi hilo mjini Mombasa, alisema kuwa kundi hilo ambalo mahakama ilisema kuwa sio haramu, kwa mtu kuamua kulifadhili sio kosa.
Dor ni mmoja wa wabunge kumi na wawili wa Kenya ambao hawakuchaguliwa ingawa waliteuliwa kuwakilisha maswala kadhaa bungeni.

CHANZO-BBC

Wednesday, October 17, 2012

HARAKATI ZA WANAHABARI RUVUMA KUANZISHA RADIO YAO,DR ANSIGAR ACHANGIA SHILINGI MILIONI 5 KUANZISHA RADI0 HIYO

 Mkurugenzi wa afya ya msingi Tarafa ya Peramiho Bw. Abel Mapunda akikabidhi Cheki ya shilingi milioni 5 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Peramiho Dr Ansigar Stuffe kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Bw. Andrew Kuchonjoma(kulia)
 Wakishikana mikono na kukabidhiana Cheki.
 Bw. Mapunda akionyesha fomu kwa Waaandishi wa habari kabla ya kuikabidhi.Katikati ni Mwenyekiti wa Klabu ya Wanahabari Ruvuma Bw. Kuchonjoma.wa mwisho kulia ni Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Bw. Andrew Chatwanga.
 Kuchonjoma akimkabidhi Cheki hiyo Mweka hazina wa Klabu hiyo Bi Joyce Joliga mara baada ya kuipokea.Katikati ni katibu wake Bw. Chatwanga.
 Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa cheki hiyo kwa ajili ya kuanzisha radio ya kijamii.Walioketi wa kwanza kushoto Katibu Mkuu Bw. Chatwanga ,Makamu Mwenyekiti Bi Leticia NyoniMkurugenzi wa afya ya msingi ,Abel Mapunda na mwisho ni Mwenyekiti BW. Kuchonjoma.
 Bw. Kuchonjoma akishukuru  kwa niaba ya Wanhabari wa Mkoa  wa Ruvuma baada kupewa msaada huo.
Kushoto ni Bw. Abel Mapunda na Dr Ansigar Stuffe ambao wamewasaidia Wanahabari Ruvuma shilingi milioni 5

RAIS OBAMA NA MIIT ROMNEY WATOANA JASHO

Rais Obama na Mitt Romney watoana jasho

 
Barack Obama na Mit Ronmney wamemenyana katika mjadala wa pili wa kempeini za uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao
Rais Barack Obama na mshindani wake wa Republican,Mitt Romney, wametoana jasho katika mdahalo wa pili kwenye kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.
Wawili hao walikabiliana mbele ya wapiga kura ambao bado hawajaamua nani watakaye mpigia kura kwenye uchaguzi huo mwezi ujao.
Walizungumzia sera ya kodi, ajira na nishati kila mmoja akijaribu kumtia dosari mwenziye wakati wakielezea watakavyofanikisha sera zao kuhusu maswala hayo.
Walikosoana mara kwa mara huku wakati mmoja Rais Barack Obama akimtuhumu Romney kwa kusema uongo.
Mpiga kura mmoja ambaye angali kuamua mgombea atakayemchagua, alisema kuwa hali ya ubishani kati ya wawili hao haikutoa taswira nzuri kuwahusu.
Mdahalo huu ni wa pili huku wagombea hao wakisubiri mdahalo mmoja na wa mwisho siku ya Jumatatu kabla ya uchaguzi kufanyika baadaye mwezi ujao.
Mhariri wa BBC wa maswala ya Amerika ya Kaskazini, anasema kuwa baada ya mjadala wa mapema leo asubuhi, Barack Obama ameweza kujiimarisha tena kwa wapiga kura kwani alionekana kuibuka mshindi.
Katika majibizano makali kuhusu mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya, bwana Romney alisema kuwa tukio hilo lilifedhehesha sera ya Obama katika eneo la Mashariki ya kati.
Naye Obama alisisitiza kuwa atafanya kila awezalo kuwakamata washukiwa wa mauaji hayo.

CHANZO-BBC

RWANDA YAWAUNGA MKONO WAASI WA DRC

Kiongozi wa kisiasa wa M23 Jean Marie Runiga

Waziri wa ulinzi nchini Rwanda, ametuhumiwa kwa kuamuru uasi katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya wataalamu wa Umoja wa mataifa.
Ripoti hiyo ya kisiri, iliyofichuliwa na shirika la habari la Reuters, inasema kuwa Uganda pia inaunga mkono waasi wa M23 ambao wamekuwa wakipigana na jeshi la DRC tangu mwezi Aprili.
Ripoti hii inakuja baada ya ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa kutolewa mwezi Juni ambayo ilituhumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi hao
Lakini Rwanda na Uganda zimekuwa zikikna madai ya kuunga mkono waasi wa M23.
Duru zinasema kuwa katika kipindi cha miongo miwili iliyopita, Rwanda imeunga mkono makundi ya waasi Mashariki mwa Congo, kama njia moja ya kupiga vita waasi wa kihutu waliokimbilia eneo hilo baada ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Baadhi wanatuhumu Rwanda kwa kutumia waasi kupigana vita vyake dhidi ya DRC , nchi ambayo ina utajiri mkubwa wa madini na eneo zima la Maziwa Makuu.
Taarifa za hivi punde za wataalamu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa zinatoa maelezo zaidi kuhusu Rwanda kujihusisha na vita vya DRC.
 Wananchi wakikimbia kutokana na vita.

Maelfu ya watu wameachwa bila makao kufuatia mapigano Mashariki mwa DRC
Wataalamu hao wanasema kuwa waasi wa M23 wanapokea amri za moja kwa moja kutoka kwa mkuu wa majeshi ya Rwanda, Generali Charles Kayonga, " ambaye naye anafuata amri za waziri wa ulinzi Generali James Kabarebe.
Wataalamu hao pia wanasema kuwa Rwanda imekuwa ikitoa silaha kwa waasi hao na kuweka mikakati ya kusajili waasi zaidi ili kuliganya kundi hilo kuwa kubwa.
Maelfu ya watu nchini DRC wamepoteza makao yao kufuatia vita hivyo kati ya waasi na wanajeshi wa Rwanda.
Ripoti hiyo iliyoonwa na shirika la habari la Reuters inasema kuwa wanajeshi wa Rwanda na Uganda wamesaidia waasi wa M23 kupanua harakati zao katika eneo la Mashariki mwa DRC.


SOURCE-BBC

WATUHUMIWA WA MKURUGENZI WA GAZETI LA JAMHURI WALIVYOTINGA MAHAKAMANI

 Watuhumiwa waliomuibia Mkurugenzi wa gazeti la Jamuhuri Bw. Deotatus Balile ambao wanatuhumiwa kumuibia vifaa mbalimbali ikiwemo Laptop na fedha vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi  milioni 4 wakiwa nje ya Mahakama ya Wilaya ya Songea.
 Katibu Msaidizi wa Klabu  ya Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Bw. Moses Konala(kushoto) na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Bw. Andrew Chatwanga wakiwa nje ya Mahakama hiyo.

 Wattuhumiwa hao wakitoka Mahakamani huku wamefunika nyuso zao,pia walikutwa na funguo 80 za kufungua vyumba kwenye nyumba za kulala wageni na moja Master key.
 Bado wakiwa wamefunika nyuso zao wakiwepa kupigwa picha.
 Kutokana Watuhumiwa hao kudaiwa kuwa hatari nje ya Mahakama hiyo kulikuwa na ulinzi mkali kama inavyoonekana.
 Mkurugezi wa gazeti la Jamuhuri Bw. Balile ambaye alikuja kutoa mafunzo kwa Waandishi wa habari Ruvuma akizungumza na Afisa wa Polisi Inspekta Anna tembo ambaye alifanya kazi kubwa  na kufanikisha Watuhumiwa kukamatwa na kufikishwa Mahakamani.
 Inspekta Anna Tembo akisalimiana na Katibu Mkuu  wa Klabu ya  Waandishi wa habari Bw. Chatwanga baaada ya kutoka Mahakamani.Katikati ni Bw. Balile.
 Inspekta Anna Tembo akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa wa habari Bw. Andrew Kuchonjoma huku Bw. Balile akiwapiga Picha.
Bw. Balile akifurahia jambo na Inspekta Anna Tembo baada ya Watuhumiwa wake kukamatwa.

MAHAFALI KATIKA SHULE YA SEKONDARI WILIMA SONGEA

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Songea Bw. Rajabu Mtiula akisalimiana na Meneja wa Shule ya Wilima iliyoko Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.
 Mwenyekiti huyo kulia akikagua jengo jipya  la Utawala la Shule hiyo.
 Igizo hili la Wachungaji wako bize,lilikuwa kivuti katika Mahafali hayo yaliyofana.
 Mmoja wa Wahitimu akipokea Cheti cha kuhitimu kidato cha nne.
 Jengo la utawala linavyoonekana.
 Mwenyekiti Mtiula akisalimiana na mmoja wa Wanafunzi wa Shule hiyo.

Akiagana na Meneja wa Shule hiyo baada ya mahafali kumalizika.

HIKI NI KIJIJI CHA CHENGENA KATIKA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

 Kijijini Chengena katika wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.Picha nyingine chini zinaonyesha mandhari ya kijiji hicho.


Tuesday, October 16, 2012

MCHEZA SHOO TOKA KIJIJI CHA MTWARA PACHANI WILAYANI NAMTUMBO MKOANI RUVUMA AKIFANYA VITU VYAKE

Hapa ni katika Mahafali ya  29 ya darasa la saba katika kijiji cha Kilangalanga wilayani Namtumbo.

WAHITIMU WA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA MSINGI KILANGALANGA WILAYANI NAMTUMBO MKOA WA RUVUMA

 Cha kusikitisha inaelezwa kuwa tayari  baadhi ya wazazi wameshaanza kuchukua nauli za kuwasafirisha mjini kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali zikiwemo za ndani.
 Wahitimu wa darsa la saba katika kijiji cha kilangalanga Wilayani Namtumbo.
Wakiimba wimbo wa Shule.

WATOTO KATIKA KIJIJI CHA CHENGENA WILAYANI NAMTUMBO

 Watoto hawa niliwakuta katika kijiji cha Chengena Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma wakiomba kibarua cha kuchota maji
 Watoto hawa niliwakuta katika kijij cha Chengena wilayani Namtumbo wakiomba kibarua cha kuchota maji kwa Nesi mmoja aitwaye Imakulata Komba wa Zahanati ya kijiji hicho.
Maskini watoto hawa wanaomba kibarua cha kuchota maji.

Monday, October 15, 2012

WARAKA KWA WADAU WANGU,WANAOTEMBELEA MTANDAO HUU

Kwenu wadau wangu salaam.
Napenda kuwaomba radhi kwa kutokuwawekeeni vitu vipya hii ni kutokana na kuwa bize na mambo mbalimbali.
Wadau wangu nawapenda.Endeleeni kutembelea mtandao huu.
Ni mimi Joseph Mwambije

Saturday, September 22, 2012

Julius Malema matatani kwa utata wake

 Na Mashirika ya habari
Afrika kusini

Julius Maleme
Polisi wa Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa mwanasiasa wa Afrika kusini anayeleta utatanishi, Julius Malema, ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha ANC.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo kuhusu mashtaka ya ku-ghu-shi fedha, rushwa, na wizi kwa njia za udanganyifu.
Kamati maalumu ya uchunguzi, iitwayo "the Hawks", imekuwa ikichunguza shughuli za kibiashara za Bwana Malema.
Bwana Malema, ambaye aliwahi kuwa mfuasi mkubwa wa Rais Jacob Zuma, amegombana na washirika wake wa zamani, na akafukuzwa chamani, kwa kutoa wito kuwa serikali ya Botswana inafaa kupinduliwa.

Friday, September 21, 2012

PIKIPIKI HIZI KWA AJILI YA KUBEBEA WAJAWAZITO BADO ZINAPIGWA NA VUMBI KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA

 Hizi ni pikipiki maalumu kwa ajili ya kubebea wajawazito toka maeneo ya vijijini na kuwafikisha hospitalini.



DC SONGEA ATEMBELEA WAFANYABIASHARA WA MITUMBA MAJENGO

 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti akizungumza na mmoja wa Wafanyabiashara wa mitumba  katika Vibanda vya majengo ambako wafanyabiashara hao wamehamishiwa.
Hapa akikagua moja ya vibanda hivyo.Wafanyabiashara wanaofanya biashara za mitumba katikati ya Mji wa Songea wamehamishiwa Majengo.

Tuesday, September 18, 2012

Ugumba wawatesa Watanzania wengi


 

Wauguzi nchini Kenya wakiwa wamewabeba watoto walipatikana kwa njia ya mwananmke kupandikizwa mbegu za kiume, ripoti za nchini kenya zinaonyesha watanzania 60 wamekwenda nchini humo kupata huduma hiyo. Picha na Arthur okwemba
WASAKA WATOTO KENYA KWA SH5.4 MIL, HADI SASA WANAWAKE 60 WAMEHUDUMIWA DAKTARI WA MUHUMBILI AKIRI TATIZO NI KUBWA
Na Mwandishi Wetu,
TATIZO la uzazi linaonekana kushika kasi nchini baada ya idadi kubwa ya wanandoa kukimbilia Kenya kupata huduma ya upandikizaji wa watoto kwa gharama ya zaidi ya Sh5 milioni.Kati ya wageni 10 wanaokwenda katika vituo vya upandikizaji vya Aga Khan na Nairobi IVF Centre nchini humo, wanne wanatoka Tanzania.Licha ya kuwapo kwa huduma hiyo nchini, imeelezwa kwamba Watanzania wengi wanakimbilia huko kutokana na unafuu wa gharama na ubora wa huduma.
Huduma hiyo ni ya mwanamke kupandikizwa mbegu ya kiume ili kuweza kushika mimba na baadaye kupata mtoto.
Mmiliki wa Kituo cha Upandikizaji cha Nairobi (Nairobi IVF Centre), Dk Joshua Noreh alisema kwa mwaka kliniki yake hupokea zaidi ya wagonjwa 270 kutoka mataifa mbalimbali  likiwamo Bara la Ulaya.
Alisema wagonjwa kutoka Tanzania walianza kumiminika katika kliniki hiyo kuanzia mwaka 2006 na ukiondoa gharama za matibabu ambazo ni Sh5.4 milioni zipo gharama za ushauri na uchunguzi wa tatizo.
“Gharama ya ushauri peke yake ni Sh42,000 za Tanzania. Baada ya ushauri, mgonjwa hutozwa Sh420,000 kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo. Gharama za matibabu hutegemea ukubwa wa tatizo. Tiba yenyewe ni upandikizaji wa mbegu, hadi hatua za kuirutubisha,” alisema.
Dk Noreh alisema ukijumlisha gharama za usafiri, malazi, mlo na tiba kwa wagonjwa wanaotoka Tanzania, wengi wao hutumia kati ya Sh8milioni hadi Sh10 milioni, kwa ajili ya kupata mimba.
Imeelezwa kuwa raia wa Uganda hukimbilia Kenya kukwepa gharama kubwa kwani nchini humo hugharimu kiasi cha Sh500,000 ya Uganda (sawa na Sh9.5 milioni) wakati huduma hiyo hupatikana Kenya kwa Sh300,000 (sawa na Sh5.4 milioni) kwa mzunguko.
“Tuna vituo zaidi ya vitano vya IVF hapa Kenya, ndiyo maana Kenya imekuwa kimbilio la wanandoa au wapenzi kupata matibabu ya aina mbalimbali za ugumba. Lakini  kikubwa ni huduma bora na gharama nafuu ndiyo sababu ya ongezeko hili la wageni kutoka nje.”
Alisema baadhi ya nchi hazina huduma ya IVF hivyo wanandoa huenda Kenya na wengine wanayo huduma hiyo katika nchi zao ila wanachagua Kenya kwa sababu ya urahisi wa tiba hiyo na kuwapo kwa mbegu za wanaume wa Kiafrika zilizohifadhiwa.
Nchi nyingine ambazo wanandoa wake wanaongoza   kwenda Kenya kwa ajili ya kupata huduma ya upandikizaji wa watoto ni Uganda, Sudan ya Kusini, Marekani na Ethiopia.
Mtaalamu kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi, Dk Prafull Patel alisema idadi ya wanaohitaji huduma hiyo imekuwa ikiongezeka kwa kasi kutoka mataifa ya Afrika, Uingereza na Marekani.
Alisema zaidi ya robo tatu ya wanaopata huduma hiyo ni watu kutoka nje ya Kenya, lakini hasa ni kutokana na unafuu wa gharama za huduma hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine.
Nchini Uganda, IVF inagharimu Sh9,000,000 za Tanzania wakati Uingereza inagharimu zaidi ya Sh10,800,000 za Tanzania na kwa wenza zinafikia Sh21,600,000 kwa kila mzunguko huku Marekani ikigharimu Sh10,620,000 na Sh19,800,000 kwa mzunguko.
Hii inamaanisha kwamba gharama nchini Kenya ni nusu ya gharama inayolipiwa Marekani, Ulaya na nchi nyingine za Afrika. Hiyo inaelezwa kuwa chanzo cha ongezeko la idadi ya wageni kwenda Kenya kusaka tiba ya ugumba.

Upandikizaji unavyokuwa
Upandikizaji huo hufanyika kwa kuchukua mbegu za mwanamume na kuzipandikiza katika mirija ya uzazi ya mwanamke.
Mwanamke mwenye matatizo huweza kwenda peke yake kupandikizwa kwa kununua mbegu zilizohifadhiwa katika kliniki au wanandoa kwenda pamoja na mwanamume kutoa mbegu ambazo zitapandikizwa kwa mwanamke.
“Tiba huchukua mwezi mmoja, huanzia siku ya pili baada ya mwanamke kumaliza hedhi na siku ya yai kurutubishwa lakini mwanamume hutumia siku moja tu pale mbegu zake zinapohitajika.”
Dk Noreh alisema sababu ya kuanza tiba siku ya pili baada ya mwanamke kumaliza mzunguko wake wa mwezi ni kulenga tarehe za uchavushaji, kwani kipindi hicho mbegu za mwanamume hupandikizwa na kusababisha mimba kutungwa.
“Mbegu zilizorutubishwa huachwa kwa siku mbili mpaka tano ndani ya chombo maalumu ili kukuza kiinitete (embryo) kabla ya kuhamishwa katika nyumba ya uzazi ya mwanamke kwa ajili ya kutungisha mimba ya kawaida.”
Alisema tatizo la ugumba linaongezeka duniani na njia hiyo inatumika kuwasaidia wanawake wasiokuwa na mayai ambao mirija yao ya kuyasafirishia imeziba na wanaume ambao manii yao ni dhaifu na hushindwa kuogelea hadi kufikia yai la mwanamke...
“Tatizo la ugumba kwa sasa ni wastani wa asilimia 10, hiyo ina maana kwamba kati ya wanandoa 10 mmojawapo hana uwezo wa kushika mimba. Kiwango hiki kwa sasa kinakua kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wanawake wa sasa kuchelewa kuolewa wakitoa kipaumbele kumalizia masomo,” alisema Dk Noreh.

Wataalamu wa Tanzania
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma alisema ongezeko la Watanzania kufuata huduma hiyo Kenya, limesababishwa na kukua kwa tatizo la uzazi nchini.
Dk Mwakyoma alisema huduma hiyo hutolewa kama tatizo la uzazi analo mwanamke. Alisema kama mwanamume ndiye mwenye tatizo, huduma hiyo haiwezi kutolewa.
“Kama mwanamke ana tatizo la uzazi, kwa mfano mirija imeziba, kizazi kimelegea, anaweza kufanyiwa upandikizaji na kupata mtoto, lakini kama mbegu za mwanamume ni dhaifu, hakuna kitu kinafanyika,” alisema.
Dk Mwakyoma ambaye aliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 80 ya wanaume nchini wana tatizo la ugumba wa kudumu au wa muda, alisema mfumo wa maisha wa sasa ndicho chanzo cha ongezeko la tatizo la uzazi.
Daktari kutoka kituo kimoja cha upandikizaji nchini ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema huduma hiyo inapatikana katika kituo hicho kwa bei nafuu kuliko huko Kenya.
“Gharama za hapa zinategemea ukubwa wa tatizo la mhusika, mchakato wake na afya yake. Wapo wengine hawahitaji kupandikizwa, wengine wanahitaji tu dawa, pia wapo wengine wanaweza kufanyiwa upandikizaji kwa zaidi ya mara moja,” alisema.
Alisema tangu kufunguliwa kwa kituo hicho Februari mwaka huu, idadi ya wanandoa wanaokwenda kupata huduma hiyo imekuwa ikiongezeka. Hata hivyo, hakutaka kuweka wazi takwimu rasmi kwa mwezi au tangu kufunguliwa kwake.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI