Tuesday, September 11, 2012

CHADEMA YAWATAKA WAZIRI NCHIMBI IGP MWEMA KUJIUZULU


Ramani ya Tanzania
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka waziri wa mambo ya ndani pamoja na mkuu wa jeshi la polisi kujiuzulu kufuatia mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi yaliyotokea wiki moja iliyopita huko mkoani Iringa.
 Vilevile uongozi wa chama hicho umemtaka rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya kimahakama itakayochunguza kifo hicho kwa madai kwamba hawana imani na kamati iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani kwa maelezo kuwa haina mamlaka ya kisheria.
Huku mazingira yaliyopelekea kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi yakiwa bado yamegubikwa na utata, chama cha Demokrasia na maendeleo kimewataka waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi na mkuu wa jeshi la polisi Said Mwema kuachia ngazi mara moja kama njia ya kuwajibika.
Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe, amesema kuwa Chadema haina imani na kamati iliyoundwa na waziri Nchimbi kwa madai kwamba imekosa mamlaka ya kisheria.
Hivyo amemtaka rais Jakaya Kikwete aunde tume ya kimahakama itakayochunguza kifo cha mwandishi huyo na kwamba, iwapo hayo hayatatekelezwa, chama hicho kitafanya maandamano makubwa.
Kwa upande mwengine, waandishi wa habari nchini wamedhamiria kufanya maandamano ya kimya kimya nchi nzima hapo kesho kulaani kuuawa kwa mwandishi mwenzao. Maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika katika mikoa yote kuanzia saa mbili asubuhi. Kwa upande wa Mkoa wa Dar es Salaam, yamepangwa kuanza katika kituo cha runinga cha Chanel Ten na kumalizikia katika viwanja wa mnazi mmoja.
Katibu mkuu wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania, Nevil Meena amesema kuwa tukio la kuuawa kwa mwandishi huyo wa habari marehemu Daudi Mwangosi tarehe mbili mwezi huu katika kijiji cha Nyololo huko mkoani Iringa, kumeibua hisia kali miongoni mwa waandishi wa habari pamoja na wanaharakati huku wengi wao wakihoji usalama wa waandishi wanapokuwa kazini hasa katika mazingira magumu.

WAZIRI MEMBE ATEMBELEA WILAYA MPYA YA NYASA, AANGALIA MPAKA KATI YA TZ NA MALAWI










Akisalimiana na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma Daud Masiko ambaye pia ni kamanda wa takukuru mkoani Ruvuma.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kushoto,akisalimiana na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe katika uwanja wa ndege wa Songea wakati Waziri huyo alipooongoza ujumbe wa wataalamu kuangalia mpaka kati ya Tanzania na nchi jirani ya malawi katika ziwa nyasa ambapo kumekuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili juu ya uhalali wa umiliki wake
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe akisalimiana na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki kabla ya kutembelea ziwa nyasa jana kuangalia mpaka kati ya Tanzania na Malawi ambao umeleta mgogoro mkubwa juu ya nani mmiliki halali kati ya nchi hizo.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lituhi wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
Mkuu wa Brigedi ya kusini Songea Kanali John Chacha akisamiliana na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe mjini Songea.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza na wazee wa mji mdogo wa Lituhi wilayani Nyasa hawapo pichani juu ya ufahamu wao kuhusu mpaka halali wa nchi mbili za malawi na Tanzania uliopo katika ziwa nyasa Katikati Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe.
Mzee Gidion Ndembeka kulia akimuonesha Waziri wa mambo ya nchi za nje Bernad Membe kitabu chenye mipaka halali kati ya Malawi na Tanzania iliyopo ndani ya Ziwa Nyasa.
Mzee aliyefahamika kwa jina moja la Ngatunga akizungumza jana wakati wa ujumbe wa wataalamu kutoka Serikalini ulipotembelea ziwa nyasa wilayani nyasa Ruvuma ili kupata ushahidi wa mmiliki halali wa ziwa nyasa ambalo limeziingiza katika mgogoro Malawi na Tanzania.
Picha na Muhidin Amri.

CHANZO CHA KUUWAWA DAUDI MWANGOSI KILIANZIA HAPA

CHANZO CHA KUUWAWA DAUDI MWANGOSI KILIANZIA HAPA

Mwandishi wa Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi akiwa amekamatwa katika eneo la vurugu za Chadema na Polisi Nyololo wilayani Mufindi jumapili iliyopita na hapa ndipo Daudi Mwangosi alipoibuka na kupinga kukamatwa kwa mwanahabari Mushi na ndipo kichapo kilipogeuka kwake na hata kuuwawa kwa bomu .
SOURCE-KWA MUJIBU WA MTANDAO WA FRANCIS GODWIN

WAZIRI NCHIMBI AZOMEWA AFUKUZWA KATIKA MAANDAMANO YA WANAHABARI JIJINI DAR ES SALAAM

WAZIRI NCHIMBI AZOMEWA AFUKUZWA KATIKA MAANDAMANO YA WANAHABARI JIJINI DAR ES SALAAM

Katika ya isiyo ya kawaida wanahabari jijini Dar es Salaam wamemzomea na kumfukuza Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Dkt Emma nuel Nchimbi katika maandamano ya Kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi leo jijini DAR.

Hatua hiyo imetokea baada ya waziri huyo wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kufika katika viwanja vya jangwani kwa ajili ya kujipa jukumu la kupokea maandamano bila mwaliko.

Kutokana na zomea zomea hiyo ya wanahabari hao dhidi ya waziri NCHIMBI hali ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo kuondolewa na rais wa UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari polisi.

Wakati hayo yakiendelea huko mkoani Mara jeshi la polisi lateka ofisi ya waandishi wa habari Kama njia ya kushinikiza wasifanye maandamano yao 
 HABARI HII NI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA FRANCIS GODWIN

MAANDAMANO YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA IRINGA KULAANI MAUAJI YA MWANGOSI

Wakipita mtaa wa uhindini

Mwandishi wa habari wa startv Malembea akiwa amebeba picha kubwa ya marehemu mwangosi
Waandishi wa habari wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali



Waandishi wa Habari Iringa wakijiandaa kuanza maandamano ya amani

Saturday, September 8, 2012

MKURUGENZI WA HOSPITALIYA PERAMIHO AFANYA JUBILEI YA MIAKA 25 KATIKA KUTOA MISAADA YA KIJAMII KWENYE TARAFA YA RUVUMA

 Mkurugenzi wa Hospitali ya Misheni Peramiho Doctor Ansigar Stuffe akizungumza kwenye jubiei yake ya miaka 25 na huduma za kijamii anazozifanya kwenye Tarafa ya Peramiho Mkoani Ruvuma kupitia  kupitia huduma ya afya ya msingi Hospitali  ya Peramiho(HAM) ilyoanzishwa mwaka 1987.
 Hapa wanavikwa mavazi ya jadi pamoja na Mratibu wa afya ya msingi(HAM) Abel Mapunda anayevikwa mavazi hayo ya kabila la Wamasai.
 Mganda hawa walikuwa kivutio
 Mratibu huyo waAfya ya ya msingi  akizungumza
 Hapa anapokea risala.
 Hapa anapokea zawadi.
 Diwani wa Kata ya Lilambo Bw. Yobo Mapunda ilikofanyika jubilei hiyo akizungumza
 Katibu Tarafa wa Tarafa ya Ruvuma Bi Digna Mhagama akizungumza kwenye Jubilei hiyo.
 Hapa anakagua mradi wa vyandarua ili kuwakinga wananchi hasa watoto na ugonjwa huo ambapo  amefanikiwa kupunguza ugonjwa huo kwa asilimia 80.
Hapa anakagua kisima cha maji mtiririko cha kijadi alichowajengea wananchi.

ALBINO RUVUMA WAOMBA KUPATIWA MAFUTA MAALUMU ILI KUKINGA NGOZI ZAO

 Watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino) wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kukabiliana na mazingira wanayoishi
Albino wakiwa kwenye mafunzo hayo ambapo wameomba kupatiwa mafuta maalumu wanayoyatumia ili ngozi zao zisidhurike.

KASI YA MATENGENEZO BARABARA YA SONGEA-NAMTUMBO INATIA MATUMAINI

 Magari yakiwa katika foleni kupisha matengenezo katika barabara ya Songea-Namtumbo
Barabara hiyo inayotengenezwa na Kampuni ya SOGEA SATOM ilivyo sasa.Kukamilika kwa barabara kutarahisisha usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma

MADINI YATAUPAIOSHA MKOA WA RUVUMA KIMAENDELEO -RC MWAMBUNGU

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu akitafakari jambo kabla ya kuzungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mambo mbalimbali  ya Mkoa huo.Kuhusu  Madini ya makaa ya mawe yaliyoko katika kijiji cha Rwanda Wilyani Mbinga amesema kazi imeshaanza na wanunuzi wakubwa ni  Nchi ya Malawi na Viwanda vya sementi vya Tanga na Mbeya.
 Akihojiwa na  na Mhariri Mkuu wa Kituo cha Televishenicha Mlimani cha jijini Dares-salaam Bw. aminia Mgheni aliyekuwa Mkoani  hapa na wenzake.
 Mkuu wa Mkoa Bw. Mwambungu akisisitiza jambo kuhusiana na tahadhari zilizochukuliwa kuhusiana na mgodi wa Urani ulioko Wilyani Namtumbo Mkoani Ruvuma.Alisema tahadhari zote zimechukuliwa kuwaondolea madhara wananchi na kuwataka kuondoa hofu..Alisema  madini hayo yataufanya Mkoa kupiga  hatua kimaendeleo.
 Wanahabari mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.Katika hatua nyingine amewaonya Mawakala wa pembejeo wanaochanganya mbolea na chumvi na  sementi kuwa watachukuliwa hatua za kisheria wakibainika.Kutoka kushoto Moses Konala wa Tanzania daima,Amon Mtega wa Mtanzania na Cresensia Kapinga wa gazeti la Majira.
Wanahabari katika mkutano huo,wa pili kushoto ni Stephano Mango wa gazeti la Dira na  Jonh Magafu.

,SUMAYE AIJIA JUU POLISI KUHUSIANA NA MAUAJI YA MARA KWA MARA YANAYODAIWA KUFANYWA NA JESHI HILO

 

ASEMA MATUMIZI YA SILAHA ZA MOTO HAYATATUI MIGOGORO, ASKARI WALIOKAMATWA IRINGA, KUFIKISHWA KORTINI JUMATATU
Na Mwandishi wetu, Morogoro
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuacha kutumia silaha za moto au nguvu ya ziada linapokabiliana na raia, badala yake litumie busara kutatua migogoro.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro, baada ya kufunga mafunzo wa wahariri wa vyombo vya habari yaliyohusu utawala, Sumaye alisema kufa mtu katika mapambano ya polisi na raia siyo kitu kidogo.
Kauli hiyo ya Sumaye inaonekana kuwalenga polisi ambao wanadaiwa kusababisha kifo cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa Televisheni ya Channel Ten mkoani Iringa, David Mwangosi.
Mwandishi huyo aliuawa Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Nyololo, Iringa kwa kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa bomu, wakati polisi walipokuwa wakiwazuia viongozi na wanachama wa Chadema kukusanyika wakati wakifungua tawi la chama hicho kijijini hapo.
Mpaka sasa askari watano wa jeshi hilo, akiwamo anayetuhumiwa kumlipua kwa bomu marehemu Mwangosi, wamekamatwa na wanaendelea kuhojiwa na jeshi hilo mkoani Iringa.
Sumaye alisema kuwa katika siku za karibuni, polisi wamekuwa wakikimbizana na raia mara kwa mara pamoja na kutumia silaha na nguvu isiyo ya kawaida hata pale pasipostahili. Jambo ambalo alisema siyo sahihi kwa mustakabali wa jeshi hilo.
“Si lazima sana kwa polisi kutumia silaha hasa za moto kila wakati. Nimekuwa nikitazama kwenye televisheni mara kwa mara na kuona polisi wakitumia silaha, hata sehemu za kuvunja nyumba tu huko vijijini. Nawashauri watumie busara,” alisema Sumaye na kuongeza:
“Tusidhani risasi inaweza kutatua migogoro wakati wote. Risasi inaweza kuharibu kila kitu, zitumike pale inapokuwa ni lazima kwani Watanzania siku zote si watu wa fujo.”
Alisema kutokana na tukio la hivi karibuni la kuuawa kwa mwandishi wa habari, Serikali, Polisi na vyombo vingine vya usalama, watakuwa wamejifunza kitu katika kutatua migogoro na migongano baina yao na wananchi wanaowaongoza.
Alisema kwamba Jeshi la Polisi nchini linapaswa kutambua  kuwa matumizi ya nguvu kupita kiasi ikiwa ni pamoja na kutumia risasi kutawanya raia, si suluhisho la migogoro baina yake na wananchi, bali kinachohitajika ni busara zaidi, ili kuepusha maafa.
Akizungumzia suala la polisi kupambana na wanasiasa alisema, mazingira ya siasa kwa sasa yamechangamka zaidi ikilinganishwa na yale ya zamani na kwamba wakati mwingine wanasiasa wamekuwa wakichangia vurugu na hivyo kulilazimisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu ya ziada.
“Sisi wanasiasa tusiwe kichocheo cha kuleta vurugu na badala yake tutumie njia za kistaarabu na si kuchokoza vyombo vya usalama. Kinachotakiwa busara zitumike pande zote, vinginevyo tutaendelea kuumiza watu,” alisema.
Kuhusu uhusiano baina ya Serikali na waandishi wa habari, Sumaye alisema kinachoathiri hali hiyo katika nchi za Afrika ni kutokana na baadhi ya Serikali kutotaka mambo yake yawe wazi. Alisema katika mazingira mengi hata pale unapokuwapo uhusiano huo unakuwa wa kinafiki usioleta tija kwa pande zote.
Alisema iwe ni polisi na wananchi au polisi na waandishi, busara zitumike zaidi badala ya nguvu katika kutafuta suluhisho kwani siku zote mapambano hayatatui na badala yake, yanaweza kuharibu kabisa amani iliyopo.
Akifunga mafunzo hayo ya siku nne yaliyohusu utawala, Sumaye alisema vyombo vya habari ni sehemu ya maisha ya kila siku katika jamii kwa kuwa vina habarisha mambo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Alisema vinatoa taarifa ya nini Serikali zinawafanyia watu wake na nini hazifanyi ili wananchi waweze kudai haki zao na hata kuikumbusha wajibu wake pale inapojisahau. Muda mwingine vyombo vya habari vimekuwa kisu kikali kwa sababu si Serikali zote zinazopenda kukosolewa, kukumbushwa na kupewa changamoto kwa yale zilizoyafanya na zinayopaswa kuwafanyia wananchi wake.
“Vyombo vya habari ni kama kioo tunachojitazama kila asubuhi kabla kutoka nyumbani kwenda ofisini au kuhudhuria mikutano muhimu, ili kujua kama umevaa uhusika wa kile unachokwenda kukifanya au kukizungumza mbele ya jamii. Huwezi kuvunja kioo kama kitakuonyesha kitu ambacho huhitaji kukiona kwenye mwonekano wako.
Hivyo si sahihi kuvilaumu au kuviadhibu vyombo vya habari pale vinapokosoa na badala yake ni kujirekebisha,” alisema Sumaye.

Watuhumiwa wa mauaji ya Iringa
Katika hatua nyingine askari watano wanaoshikiliwa Iringa wanaendelea kuhojiwa, huku taarifa zikieleza kuwa wanaweza kufikishwa mahakamani Jumatatu, kutokana na kushindikana jana.
Jana, taarifa zilisambaa kwamba askari hao walikuwa wafikishwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, lakini hadi jioni, walikuwa hawajafikishwa. Pia hakukuwa na taarifa zozote za nini kilikuwa kinaendelea.
“Ni kweli walitakiwa wafikishwe leo, lakini hadi sasa hawajafika, wakifika nitawaeleza,” alisema mmoja wa wafanyakazi wa mahakama hiyo jana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda hakutaka kueleza lini watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kile alichosema kwamba kwa sasa yeye siyo msemaji wa jambo hilo.
“Hapa alikuja IGP (Said Mwema), na sasa yuko DCI (Robert Manumba). Kwa mazingira haya uhuru wangu wa kuzungumza uko limited, (una kikomo),” alisema.
Alipoulizwa watuhumiwa hao wako mahabusu ipi, alihoji... “Wapi?” Aliendelea kusema, “Nashindwa kusema wapo au hawapo kwa kuwa mimi siyo msemaji wa jambo hilo, ila nawashauri m-cross-check  (kuthibitisha), vizuri vyanzo vyenu vya habari.”

BILL CLINTON AMPIGIA DEBE BARACK OBAMA

 Na Mashirika ya habari
Marekani
Rais mstaafu wa Marekani  Bill Clinton na Barack Obama
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton amemtetea vikali mgombea urais wa chama cha Democrats nchini Marekani Barack Obama.
Katika hotuba iliyochukua muda wa dakika 50 katika kongamano la chama hicho linalofanyika mjini Charlotte, North Carolina, Clinton alikosoa sera za uchumi za chama pinzani cha Republican.
Bill alisisitiza kuwa sera ya uchumi ya Barack Obama imeweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo ambao ulikuwa umedorora. Bwana Clinton alimaliza hotuba yake kwa kumteua rais Obama kuwa mgombea rasmi wa urais wa chama.
Rais Obama atamenyana na mgombea wa chama cha Republican Mitt Romney katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba.
Hotuba ya Clinton ni dalili ya kuimarika kwa uhusiano kati yake na Obama na pia kama juhudi za kupiga jeki mvuto wa obama miongoni mwa wazungu wanaofanya kazi.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa wapiga kura wa chama hicho wamekuwa waangalifu sana kuhusu sera za Obama lakini Clinton ana rekodi nzuri ya kuwashawishi watu kumuunga mkono Obama.
Clinton aliambia wafuasi wa chama '' Amueni nchi mnayotaka kuishi. Ikiwa mnataka viongozi wasio wajali basi pigieni kura chama cha Republican. Mkitaka nchi yenye nafasi nyingi na ambayo majukumu yanagawanywa, basi sote tuko pamoja. Lazima mumpigie kura Barack Obama na makamu wake Joe Biden."
Bwana Clinton alikosoa vikali chama cha republican kwa kuzuia juhudi za uchepuzi wa uchumi na badala yake kujihusisha na mijadala kuhusu sera.
Kura za maoni zinaonyesha Barack Obama akiongoza kwa asilimia 47 huku mpinzani wake Mit Romney akimfuata kwa asilimia arobaini na sita.

RAIS OBAMA AWAOMBA WAMAREKANI KUMPA FURSA NYINGINE YA KUWAONGOZA

Rais wa Marekani Barack Obama
Na Mashirika ya habari
Marekani
Rais wa Marekani Barack Obama, amewaomba wamarekani kumpa fursa nyingine kuiongoza nchi hiyo.
Ombi lake amelitoa katika kilele cha kongamano la chama cha Democratic mjini North Carolina
Akijiwasilisha kama mgombea wa urais mwenye kuleta matumaini kwa wamarekani, Rais Obama alisema kuwa uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba, utatoa fursa kwa wapiga kura kuchagua kati ya maono mawili tofauti kuhusu hatma ya Marekani.

 Aliwataka Wamarekani kuwa wavumilivu akisema kuwa matatizo yanayokabili Marekani yamekuwa yakiongezeka kwa miaka mingi na kuwa itachukua muda kuweza kuyatatua.

Lakini aliongeza kuwa ikiwa watamchagua tena, ataweza kubuni nafasi mpya za kazi, kupunguza madeni na kuimarisha uchumi wa Marekani.

Rais Obama alisema anajiona kama kiongozi aliyekuwa amewekwa kwa mizani kujaribiwa uongozi wake na kuwa amefaulu. Alisema mpinzani wake wa Republican, Mitt Romney, hayuko tayari kwa mashauriano ya kidiplomasia.

Alitofautisha malengo yake na yale ya chama pinzani na kurejelea kauli mbiu yake ya mwaka 2008 , kuwataka watu kuwa na matumaini.
"sikuwahi kusema kuwa safari hii itakuwa rahisi na sitatoa ahadi hiyo hii leo'' Obama aliambia kongamano la wajumbe wa Democrat.
Mitt Romney wa chama cha Republican atapambana na Rais Obama kuwania urais huku kura za maoni zikionyesha wawili hao wakikaribiana.

Friday, September 7, 2012

SERIKALI IMEMSAHAU MPIGANIA UHURU HUYU ALIYEWAHI KUWA BOSI WA KIKWETE MTWARA

 Mke wa Kiongozi huyo Bi. Eva Simon wa zamani akizungumna Waandishi wa habari.
 Mke wa mzee huyo Bi. Eva simon ambaye alikuwa Bibi maendeleo kwenye miaka 1973 akiwa Hospitali hapo.Pia alisom,a na Spika wa Bunge la tanzania Bi Anne Makinda ambapo walikuwa wakimuita Ana Samamba.Anasema kuwa alisoma na Bi. Makinda kwenye miaka ya 1962 hadi 1965 na kwamba walisoma darasa moja Middle School Peramiho.
 Hapa akiwa katika Hospitali.

 RAIS KIKWETE SIKIA KILIO  MZEE HUYU
SERIKALI imemsahau mpigania Uhuru na alyewahi kushika nyadhifa nyigi za kisiasa Nchini na za Kiserikali huku akiwahi kuwa Katibu wa CCM  na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Josephat(75)  rangimbaya maarufu kwa jina la Liriku liku ambapo amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akisumbuliwa na maradhi.

Aliwahi kufanya kazi na Rais Kikwete wakati akiwa Katibu wa CCM Wilaya ya Mtwara yeye alikuwa Katibu wa Mkoa na Mkuuwa Mkoa.Pia aliwahi kuwa Katibu wa Tanu katika Wilaya mbalimbali Nchini na wakati akiwa Bwana Afya wa Wilaya enzi za mkoloni alitaka usawa kati ya Waafrika na Wazungu hali iliyopelekea afukuzwe kazi
 Mtoto wa Kiongozi huyo Bw. Juvenali Mhagama akimuuguza baba yake
 Mtoto huyo akiwa Hospitali
 Mke wa mzee huyo Bi. Eva simon akimuuguza mumewe
Bw. Juvenali akimjulia hali Baba yake

MKUU WA WILAYA YA SONGEA AONGOZA MAMIA KUMZIKA AFISA MTENDAJI WA MTAA WA MABATINI WILAYANI HUMO

       MAMIA WA SHIRIKI  KUMZIKA                                                                                                    WAANDISHI NAO WASHIRIKI                                                                                                      
 Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Manbatini Songea Bi. Gabriela Komba wakati wa uhai wake.Amezikwa kwenye Makaburi ya Mfaranyaki Songea.Alikuwa akiugua ugonjwa wa mifupa.

 Mama wa Marehemu
 Mkuu wa Wilaya Songea Bw. Joseph Joseph Mkirikiti(kati kati) amewaongoza waombolezaji kumzika Mtendaji huyo wa Mtaa.Wa kwanza kushoto ni Meya wa Manispaa ya Songea Bw. Charles Mhagama na wa kwanza kulia ni Mwanahabari wa Gazeti la Majira Songea Bw. Mhaiki Andrew.
 Jeneza la mwili wa Marehemu likiteremshwa kaburini.U mavumbi na mavumbini utarudi.Wanadamu Mkubukeni Muumba wenu wakati wa uhai wenu.
 Mume wa Marehemu Mwalimu Samsoni Komba(wa kwanza kushoto)  akimlilia Mkewe,wa kwanza kulia ni Baba Mkwe wa Marehemu akiwa amemshika mjukuu wa Marehemu.
 Mume wa Marehemu akimuaga Mkewe.
 Baba Mkwe wa Marehemu Thomas Lipuka Komba akiwa na mkewe akimuaga Mkamwana wake na kuweka Taji kwenye kaburi lake.
 Katibu Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Bw. Moses Konala  akitoa Neno kwenye msiba huo
 Mamia ya wakazi wa Songea kwenye msiba huo.
 Mama wa Marehemu akigaragara kwenye Kaburi la Mwanae
Mwombolezaji akiwa amebeba msalaba kwenye msiba huo.