Akielekezwa sehemu ya kukaa na Alhaji Mustapha Songambele
Mkuu wa Mkoa Said Mwambungu akiingia. ukumbini
Akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa Bw. Mwambungu.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa kwenye Baraza la Idd.Wa kwaza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Bi. Senye Ngege,wa pili kushoto ni Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mama Mwambungu
Na Joseph Mwambije,
Songea
SHEIKH Mkuu wa Wailsamu Nchini Mufti Shabaan bin
Simba amewata Waislamu ambao wanahitaji kujua idadi yao kujihesabu wenyewe
kwenye Misikiti yao badala ya kuzuia zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa
kugoma kuhesabiwa na kuzuia wengine kuhesabiwa.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye Baraza la
Idd Elftri lilofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana
ya Songea ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Ibada ya Idd Eftri iliyofanyika
Kitaifa Mkoani Ruvuma.
Kiongozi huyo wa Waislamu Nchini amwataka Waumini wa
dini hiyo kuachana na baadhi ya Viongozi wa Kiislamu wanaowahamasisha
kuiasi Serikali kwa kuchochea vurugu kwa kuwa kufanya hivyo ni
kinyume cha miongozo ya Kurani tukufu inayowataka kutii mamlaka ilimradi
isiende tofauti na Mungu.
‘Waislamu wajihesabu wenyewe misikitini wasiitegemee
Serikali kuwatolea hesabu yao
kwamba wako wangapi hivyo basi kupinga Zoezi la Sensa kwa madai ya kutokuwepo
kipengele kinachoeleza dini si sahihi’alisema Mufti Simba.
Aliwataka kuwa na Kompyuta katika Misikiti yao na
kuhifadhi kumbukumbu zao na kujua wana vijana,watoto na yatima
wangapi badala ya kupinga kuhesabiwa kwa maendeleo ya Nchi.
Sheikh Simba alifafanua kuwa Sensa ya watu na makazi ni kwa
maendeleo ya
Nchi hivyo kupinga si sahihi na na kuwataka Waumini wa
Kiislamu kutopinga maendeleo na kuwapuuza Masheikh wanawahamasisha kupinga
maendeleo.
Katika hatua nyingine amewataka Waislamu kutenda mema ili
kuongeza idadi yao
na kubainisha kuwa licha ya uchache wao watang’ara ikiwa watajizuia kutenda
maovu.
‘Mjizuie kutenda maovu kwa kuwa Mwanadamu asiyejizuia
kutenda maovu mwisho wake daima huwa ni mbaya na msipokuwa na uwezo wa kujizuia
kutenda maovu ibada ya funga kwenu haina maana’alisema na kufafanua
Katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
mmejizuia kutenda maovu muendelee hivyo na kuendeleza kazi mliyopewa na
Mungu ya kutenda mema hivyo Muwe viumbe mliozaliwa upya baada ya Mfungo.
Aliwataka Waislamu kuachana na maneno ya kwamba wao
wanaonewa na badala yake wawe wanachanga pesa kwa ajili ya kuwasaidia yatima na
wajane na kwa maendeleo kwa ujumla huku wakikataza maovu na kuhimiza mema.
Akizungumza kwenye Braza hilo
Katibu wa Baraza la waislamu Tanzania(BAKWATA)
Mkoa wa Ruvuma Sheikh Abdul Shakhil alisema wana mpango wa kujenga Kituo
cha Afya na Sekondari katika Manispaa ya Sengea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye alimwakilisha
Rais Kikwete ambaye alitakiwa kuwa Mgeni Rasmi alisema katika kipindi cha hivi
karibuni umezuka utamaduni mgeni kwa Watanzania wa kuchochea chuki na
uhasama miongoni mwa Watanzania na kuwataka Viongozi wa dini kukemea
vitendo hivyo.
Alisema kuwa gharama ya machafuko ni kubwa sana kwa Taifa hivyo aliwataka Watanzania
kutofurahia vitendo vya kuchochea machafuko na badala yake kuendelea kuitunza
tunu ya amani,umoja wa Kitaifa na mshikamano
Alisema Serikalikali itaendelea kushirikiana na Viongozi wa
dini kwa kuwa inatambua,kuheshimu na kuthamini sana mchango wa dini
katika mafanikio na maendeleo ya Taifa.
Mwisho
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea wakiwa kwenye Baraza hilo.
Mufti Simba akizungumza kwenye Baraza hilo.
Akiongea.
Baadhi ya waumini wakiwa Barazani hapo
No comments:
Post a Comment