Ofisi za Polisi mkoa wa Iringa
Na Joseph Mwambije,
Iringa
MTU mmoja anayedhaniwa kuwa jambazi Mkazi wa Mbinga
Mkoani Ruvuma akiwa na jambazi Mwenzake ameuawa na wananchi wakati
wakitaka kumnyang’anya shilingi milioni tatu Mfanyabiashara aitwaye
Kavenga Paul Mfanyabiashara wa Ipogoro Wilayani Iringa.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi aliyekuwa Mkoani
humo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Michael Kamuhanda alisema tukio
hilo lilitokea Agost 10 saa 3.00 usiku maeneo ya Ipogoro Mkoani Iringa.
Amemtaja mtu aliyeuawa
kwa tuhuma za ujambazi kuwa ni Michael
Mhonyo ambapo baada ya kupekuliwa alikutwa na kiatmbulisho cha kupigia kura
kinachomtambulisha kuwa ni Mkazi wa Mbinga Mkoani Ruvuma.
Kamanda huyo wa Polisi anafafanua kuwa katika tukio hilo Bw. Kavenga Paul na
Mkewe Rehema Kavenga wakiwa katika
maeneo ya Ipogoro baada ya kufunga duka walivamiwa nna majambazi wawili mmoja akiwa na
bastola.
‘Katika tukio hilo
majambazi hao walifyatua risasi nne hewani na kati ya hizo moja ilimjeruhui Bi.
Rehema kwenye kisigino cha mguu wa kulia na amelazwa katika Hosptali ya Mkoa wa
Iringa na afya yake inaendelea vizuri’alisema Kamanda huyo na kuongeza kuwa
Baada ya Wananchi kusikia
milio ya risasi walitoka na kuwazingira majambazi hao na kumuua mmoja na
mwingine mwenye bastola alikimbia na
jina lake halikupatikana na uchunguzi wa Polisi
bado naendelea’alisema.
Alitoa wito kwa wananchi kutotembea na pesa na badala yake
kuweka fedha Benki na kwamba wawe waangalifu wanapotembea na pesa pia
wanapokuwa na pesa nyingi kuomba ulinzi wa jeshi la Polisi na Taasisi zaa
Ulinzi.
Mwisho
Makao Makuu ya Polisi Mkoawa Iringa.
No comments:
Post a Comment