Wednesday, August 15, 2012

WANAHABARI 170 NYANDA ZA JUU KUSINI NA MIKOA YA MTWARA NA LINDI WAPATIWA MAFUZO YA SENSA

 Mandhari ya Mji wa Iringa ambako mafunzo hayo yalifanyika ili Wanahabari waweze kuandika  kwa usahihi na kuhamasisha Zoezi la Sensa.Hapo ndipo Wanahabari 170 wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini na Mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika.
 Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma akisimama  kutambulisha Waanishi wa Mkoa wake.Nyuma ya Kuchonjoma ni Katibu wa Mkuu wa Chama hicho Bw. Andrew Chatwanga.
 Baadhi ya Wanahabari wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini na Mikoa ya Lindi n Mtwara wakisikiliza kwa makini mada ya Dodoso kubwa na dogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma akifungua  mafunzo hayo.Wa kwanza kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa huo Bi. Getrude Lupaka.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa Bw. Daud Mwangosi akizungumza kwenye mafunzo hayo.Anayemfuatia ni Kamaanda wa Polisi wa Mkoa  wa Iringa Bw. Michael Kamuhanda. na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt Prisca Warioba.
 RC Dkt Ishengoma na DC Warioba wakipitia makabrasha kwenye mafuinzo hayo.
 Wanahabari wa Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja na RC Ishengoma(mwenye gauni la bluu waliokaa) baada ya kufungua mafunzo hayo.Waliokaa wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Ruvuma Press club bw. Andrew Kuchonjoma.Wa kwanza waliochuchumaa ni Mmiliki wa Mtandao huu Bw. Joseph Mwambije.
 Picha nyingine ya pamoja na Mgeni rasmi.Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Ruvuma Press Club Bw. Andrew Chatwanga.
 Wanahabari wakijaribu kupata picha  kwa ajili ya vyombo vyao vya habari kwenye mafunzo hayo.
 Mmoja a Watoa mada kwenye mafunzo hayo Bw. Bakary Kimwanga.Akisisitiza juu ya kuandika habari za sensa kwa usahihi
 Mwenyekiti wa mafunzo hayo Bw. Christopher Nyenyembe akizungumza kwenye mafunzo hayo.kushoto moja wa Waratibu wa Mafunzo hayo.
Mmiliki wa Mtandao huu akibadilishana mawazo na wanahabari wenzake.

No comments:

Post a Comment