Akisalimiana na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma Daud Masiko ambaye pia ni kamanda wa takukuru mkoani Ruvuma. |
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kushoto,akisalimiana na Waziri wa
mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe katika uwanja wa
ndege wa Songea wakati Waziri huyo alipooongoza ujumbe wa wataalamu
kuangalia mpaka kati ya Tanzania na nchi jirani ya malawi katika ziwa
nyasa ambapo kumekuwa na mvutano kati ya nchi hizo mbili juu ya uhalali
wa umiliki wake
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe
akisalimiana na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki
kabla ya kutembelea ziwa nyasa jana kuangalia mpaka kati ya Tanzania na
Malawi ambao umeleta mgogoro mkubwa juu ya nani mmiliki halali kati ya
nchi hizo.
Baadhi
ya wananchi katika kijiji cha Lituhi wilaya mpya ya Nyasa mkoani
Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani
kuhusiana na mzozo ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika
ziwa Nyasa.
Mkuu
wa Brigedi ya kusini Songea Kanali John Chacha akisamiliana na Waziri
wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe mjini
Songea.
Wananchi wakimsikiliza
Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe hayupo pichani kuhusiana na mzozo
ulipokati ya Tanzania na Malawi juu ya mpaka katika ziwa Nyasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza na wazee wa mji mdogo
wa Lituhi wilayani Nyasa hawapo pichani juu ya ufahamu wao kuhusu mpaka
halali wa nchi mbili za malawi na Tanzania uliopo katika ziwa nyasa
Katikati Waziri wa mambo ya nje Bernad Membe.
Mzee Gidion Ndembeka kulia akimuonesha Waziri wa mambo ya nchi za nje
Bernad Membe kitabu chenye mipaka halali kati ya Malawi na Tanzania
iliyopo ndani ya Ziwa Nyasa.
Mzee
aliyefahamika kwa jina moja la Ngatunga akizungumza jana wakati wa
ujumbe wa wataalamu kutoka Serikalini ulipotembelea ziwa nyasa wilayani
nyasa Ruvuma ili kupata ushahidi wa mmiliki halali wa ziwa nyasa ambalo
limeziingiza katika mgogoro Malawi na Tanzania.
Picha na Muhidin Amri.
No comments:
Post a Comment