Ndugu Wasomaji wa Mtandao huu tunawaletea Makala ya Binti Ndembo na Uchawi na Mchambuzi wako wa masuala ya Uchawi Mwanahabari Adam Nindi.
Fuatana naye
Kwa
habari za kina nilikuwa nikiifahamisha Jamii kwa kitu kinachoitwa uchawi
ambacho ndicho changamoto kwa watu wanaoishi pembezoni.
Mganga wa jadi bint Frola
Ndembo
Nikiwa
katika kambi ya Mganga mashuhuri wa Nyanda za juu Kusini Mama Binti Flora
Ndembo nimeweza kupata siri kubwa kuhusu uchawi. Wachawi wenyewe wamesema
wamejiingiza katika uchawi baada ya kuona Jamii ikiwatenga, wale ambao ambao
hawana uchumi wa kutosha ndio wanaunda umoja wa kuwatesa wenzao.
Mchawi
mkuu wa wachawi wote ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalinina
hatimaye kuchaguliwa kuwa katibu wawachawi mkoa wa Ruvuma amesema yeye alijiunga na uchawi kwa ajili ya
kutaka kujikinga na watu wabaya lakini mara
baada ya kustaafu alipendekezwa kuwa Katibu Mkuu wa wachawi Mkoa wa Ruvuma.
Lakini
yeye mwenyewe amesema ameamua kujitoa baada ya wachawi wenzie kumuua mototo
wake ambaye alifikia ngazi ya kuwa Askofu; hapo ndipo alipoona kuwa uchawi
hauna maana.
Nikiwa
katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika
maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi
mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake
kuweka rehani mwili wake baada
Nikiwa
katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika
maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi
mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake
kuweka rehani mwili wake baada wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Nikiwa bado katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo, nilitiwa na fadhaha baada ya kumuona Binti mwenye umri wa miaka 10 aliyepewa uchawi na Mama yake na kuweza kupewa mboga ya akiba ambacho ni kidonda kilicho ubavuni ambacho yeye alikiri kuwa akikosa mboga hutumia kwa kuchovya kwenye kidondaMaskini Binti huyo katika maisha yake hadi kufikia miaka hiyo 10 alikuwa akichukia shule kama nini lakini baada ya kufika kwa Binti Ndembo ameacha uchawi na kuomba akaendelee na Masomo
Kamanda
wa Polisi aliye hamia Iringa Michael Kamuhanda kushotona Kamanda Mpya Mkoa wa
Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki
Ndugu yangu nikiwa katika kambi hiyo na Binti
Ndembo nimeona mambo mengi cha kufurahisha mganga huyo hana uchochezi. Yeye
amekuwa akipatanisha ndugu hao na kuwa Jamii moja. Nikiwa Kambini hapo
nimeshuhudia Viongozi wa ngazi za juu akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akitoa elimu Shirikishi kwa kutaka Jamii iachane
na Mambo ya Ushirikina.
Mganga
huyo mashuhuri mbali ya kutibu watu wenye asili ya Ushirikina lakini hata hivyo
ameshaweza kukamata Majambazi Sugu, na wao kusalimisha silaha zao na kuachana
na Ujambazi.
Jambo
la kuingilia Masuala ya Ujambazi, Mganga huyo mashuhuri amepata misukosuko kwa
kuwahi kupigwa risasi mbili na kukimbizwa Hospitali ambako alitolewa.
Amewahi
kufungwa Kamba na kutupwa msituni na kuambiwa aachane na masuala ya kufuata
Majambazi lakini uganga wake uliweza kumwokoa.
Pia
kwa Mara ya Kwanza Mganga huyo aliweza kubainisha ndoa iliyofungwa kati ya Mama
na Mtoto wake wa kuzaa mwenyewe. Hatimaye aliweza kuibainisha Ndoa hiyo
hadharani.
Ndugu zangu wasomaji, Shabaha yangu ni
kutaka kuendelea kupata mawazo kutoka kwenu, kitu kikubwa ambacho kinasababisha
Maendeleo kuto chukua Kasi ni Kushiriki katika Mambo ya Ushirikina. Sasa hapa tumeona watu walio wengi wakiacha
Uchawi na kutangaza Hadharani.
Ahsante sana Mr, Mwambije the Great,kwa habari zako na matukio unazotupasha wananchi.
ReplyDeleteBig up kwa binti Frola Ndembo!
Ahsante sana Mr, Mwambije the Great,kwa habari zako na matukio unazotupasha wananchi.
ReplyDeleteBig up kwa binti Frola Ndembo!
Big up kwako Mwambije the great!
ReplyDeleteBig up kwa binti Frola Ndembo
Mimi Nahitaji Uchawi, Nitaupata Vipi.
ReplyDelete