Wednesday, October 31, 2012

HATUWEZI KUWA NA KATIBA BORA BILA KUWA NA MISINGI BORA YA KATIBA

  nilikuwa miongoni mwa Waandishi wanaonolewa kuhusiana na kujenga uwezo wa kuandika habari za mchakato wa kupata katiba mpya.hapa ni nje ya Hoteli ya Dodoma Hoteli yakofanyika mafunzo hayo ya siku mbili.
 Bw. Israeli Ilunde wa Asasi ya YPC akitoa Mada ya Ushawishi na utetezi katika mchakato wa kutengeneza Katiba mpya Tanzania
 Profesa Abdul Sharif wa Baraza la Katiba Zanzibar akitoa Mada kuhusiana na Mchakato wa Katiba  mpya  na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 Hapa anasema Wananchi hawakushirikishwa katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kwamba katika mchakato wa kupata Katiba mpya makosa yasijirudie bali wanapaswa kushirikishwa.kulia ni Bw. Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba.
 Wanahabari wakifuatilia mada kwa umakini kubwa
Profesa Sharif akichambua mada.Anasema hatuwezi kuwa Katiba bora bila kuwa na misingi bora ya  Katiba

Utoro wa wabunge wakwamisha azimio


Ukumbi wa Bunge ukiwa na wabunge wachache jambo lililosababisha kushindwa kupitishwa kwa azimio la bunge la kuridhia marekebisho ya pili ya mkataba wa ushirikiano kati ya Jumuiya ya nchi za Ulaya pamoja na nchi wanachama wa Umoja wa nchi za afrika, Caribbean na Pasifiki, mjini Dodoma, jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 


Dodoma
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kifungu cha 77 (1), akidi kwa kila kikao cha Bunge wakati wa kufanya uamuzi itakuwa ni nusu ya wabunge wote, kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 94 ya Katiba, isipokuwa kwamba, idadi hiyo haitahusu hoja kuhusu uamuzi wa kubadilisha masharti yoyote ya Katiba kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba.
Fuul story


UTORO wa baadhi ya wabunge jana ulikwamisha kupitishwa kwa azimio la Marekebisho ya ya Pili ya Mkataba wa Ushirikiano Kati ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za Afrika, Caribean na Pacific (ACP).
Hii ni mara ya pili kwa wabunge kukwamisha shughuli za Bunge katika kipindi cha miezi minne kutokana na utoro. Awali, utoro huo ulikwamisha kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Kukwama kwa bajeti hiyo kulikuja wiki moja tu tangu Spika wa Bunge, Anna kukemea tabia ya utoro akisema tabia hiyo ilikuwa imekithiri.
Jana, hali hiyo ilitokea baada ya Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa kuhitimisha kujibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia azimio la mkataba huo aliloliwasilisha baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Mara baada ya Waziri Mgimwa kumaliza kujibu hoja ili kutoa nafasi kwa Bunge kupitisha azimio hilo, ndipo Mbunge wa Mkanyangeni (CUF), Mohammed Mnyaa aliposimama na kuomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni ya Bunge, Kifungu cha 68 akitaka Bunge lisipitishe azimio hilo kutokana na idadi ndogo ya wabunge waliokuwa ndani ya ukumbi.
Aliomba Bunge lipange muda mwingine wa kupitisha azimio hilo ili marekebisho yaliyopo katika mkataba huo yapitishwe kwa mujibu wa kanuni.
Spika wa Bunge, Anne Makinda alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kulipitisha azimio hilo hadi leo asubuhi.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kifungu cha 77 (1), akidi kwa kila kikao cha Bunge wakati wa kufanya uamuzi itakuwa ni nusu ya wabunge wote, kama ilivyofafanuliwa katika Ibara ya 94 ya Katiba, isipokuwa kwamba, idadi hiyo haitahusu hoja kuhusu uamuzi wa kubadilisha masharti yoyote ya Katiba kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba.
Wakati Spika akiahirisha Bunge, baadhi ya wabunge walionekana wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge huku wengine wakiwa katika mghahawa uliopo katika viwanja hivyo.
Bunge la Tanzania kikatiba, linapaswa kuwa na wabunge 357.
Akichangia azimio hilo Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliishauri Serikali kuwa makini na mikataba ya kimataifa huku akitaka mkataba huo wa ACP usaidie kurejeshwa kwa Sh360 bilioni zilizofichwa nchini Uswisi na baadhi ya Watanzania.
Mnyika alisema kifungu cha 29 cha mkataba huo kinataja ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwamo kuzuia biashara haramu na rushwa.
Alitaka Serikali itumie kifungu hicho kuomba mabilioni ya fedha yaliyofichwa na baadhi ya Watanzania katika benki mbalimbali huko Uswisi.
Suala hili limeibuka bungeni wakati, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe mwishoni mwa wiki iliyopita alikaririwa akimtuhumu , Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea kuwa ameiandikia barua Serikali ya Uswisi akieleza kuwa Serikali ya Tanzania haina maslahi na fedha hizo madai ambayo Dk Hoseah aliyakanusha. Zitto alidai kuwa fedha hizo zimefichwa na vigogo 10.

Mbunge wa Kisarawe (CCM), Seleman Jaffo akichangia azimio hilo, aliitahadharisha Serikali kuwa makini wakati wa kuingia mikataba ya kimataifa akisema mingine inaweza kuwa na matatizo kwa taifa.
Alisema Watanzania wasipokuwa makini katika kuingia mikataba ya kimataifa, wanaweza kujikuta wanaridhia mambo yasiyofaa kwa taifa kama vile kukubali ndoa za jinsia moja.
Awali, akiwasilisha azimio hilo, Dk Mgimwa alisema madhumuni ya mkataba huo ni kujenga ushirikiano imara utakaowezesha kujenga uchumi endelevu ili kupunguza umasikini katika nchi wanachama.

Mafao ya kujitoa
Hatimaye, Serikali imesalimu amri na kukubali yaishe baada ya kufuta tangazo lake la Agosti mwaka huu la kusitishwa kwa fao la kujitoa.
Hata hivyo, habari zilizopatikana zinaeleza kuwa hatua hiyo ya Serikali inatokana na kelele za wabunge na wanaharakati ambao kwa zaidi ya miezi miwili, wamekuwa wakihoji juu ya sheria hiyo.
Suala hilo la fao la kujitoa liliibuka katika kikao cha wabunge wakati wakipewa taarifa ya shughuli za Bunge katika Mkutano huu unaendelea kilichokaa jana mchana katika Ukumbi wa Pius Msekwa.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Spika Anne Makinda alilitolea ufafanuzi kwa kueleza kuwa Serikali itawasilisha muswada bungeni kufanya marekebisho ya fao hilo.
Jaffo ambaye alikuwa amewasilisha kwa Spika kusudio la kuwasilisha hoja binafsi kupinga kuondolewa kwa fao hilo, alimwambia mwandishi wetu jana kuwa amepokea barua ya kumpa taarifa kuwa Serikali itawasilisha bungeni muswada wa marekebisho.
Alisema marekebisho hayo yataruhusu mifuko yote ya jamii kuendelea kutoa mafao ya kujitoa kama ilivyokuwa awali.
Mbunge huyo alisema amepokea kwa furaha uamuzi huo wa Serikali ili wafanyakazi waendelee kunufaika na mifuko hiyo ya jamii.
“Nashukuru kilio changu kimesikilizwa na Serikali kwangu mimi huu ni ushindi, kwani wafanyakazi wengi nchini hawana kazi za uhakika,” alisema
Alisema wafanyakazi wengi hususan wa sekta ya madini, hawana uhakika wa ajira hivyo kuondolewa kwa fao la kujitoa kungewapa wakati mgumu.
Mnyika pia alikuwa amewasilisha kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kupinga fao la kujitoa kuondolewa katika bunge hili.
Katika Mkutano wa Nane wa Bunge, Jaffo alipinga sheria hiyo ya kufuta fao la kujitoa alipoomba mwongozo wa Spika na mara baada ya kuwasilisha hoja zake, aliungwa mkono na wabunge wengi isipokuwa Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola ambaye alisimama na kutetea sheria hiyo.
CHANZO-MWANANCHI

WANAHABARI NCHINI WATAKIWA KUANDIKA NA KUTOA MAONI KUHUSIANA NA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA

 Deus Kibamba -Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba
Na Joseph Mwambije,
Dodoma
WAANDISHI wa habari Nchini wametakiwa kuandika  na kutoa maoni yao kuhusiana na mchakato wa kupata Katiba mpya ili Wananchi wajue kinachoendelea na kwamba umakini unatakiwa ili iweze kupatikana Katiba bora.
Wito huo umetolewa  jana(leo) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba wakati akitoa mada kuhusiana na Mchakato wa kupata Katiba mpya kwa Waandishi wa habari zaidi ya 36 kutoka Mikoa mbalimbali Nchini ambao wanapatiwa mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uwezo wa wa kuandika habari kuhusiana na mchakato  wa Katiba mpya.
‘Waandishi pelekeni maoni yenu kuhusiana na mchakato wa kupata katiba mpya na pia muandike habari na makala kuhusiana na Katiba mpya ili tupate Katiba bora yenye maslahi kwa Taifa na wananchi’anasema Bw. Kibamba.
Alisema kuwa Watanzania wasipokuwa  amakini itapatikana Katiba mbovu kuliko iliyopo sasa hivyo alisisitiza kuwa umakini unatakiwa katika kuelekea kupatikana kwa Katiba mpya.
Mwenyekiti huyo wa jukwaa la Katiba alisema kuwa Sauti ya Jukwaa la Katiba itapelekwa kwa wananchi na Wanahabari na kwamba Jukwa hilo pia linalinda Katiba iliyopo isivunjwe na ndio  maana alisema kuwa alipouawa Marehemu Daud Mwangosi wa  hawakunyamaza kwa kuwa Katiba  ilivunjwa.
Alisema kuwa katika mchakato wa kupata Katiba mpya Wanahabari wana nafasi  ya pekee na kuwahamasisha waandishi wa habari kuandika habari kuhusiana na Mchakato wa kupata Katiba mpya uanaoendelea.
Aliwataka Wanahabari kutokuwa waoga kuandika habari  za Katiba na kubainisha kuwa wale watakaonyanyaswa kwa kuandika habari za mchakato wa Katiba mpya Sheria itawalinda.

 Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada katika Ukumbi wa Dodoma Hotel Mjini Dodoma.
 Bw. Abdinery Chihimba Mtoa mada kutoka Kenya akitoa uzoefu wa Nchi hiyo kupata Katiba mpya
 Watoa mada Profesa Abdul Sharif  wa Baraza  la Katiba Zanzibar na Deus Kibamba wakisikiliza kwa makini uzoefu wa Katiba mpya ya Kenya.

 Mmoja wa washiriki Bw. Kimambo kutoka Kilimanjaro akifuatilia kwa makini.

Wakimbizi wa Burundi nchini TZ warejeshwa makwao

Ramani ya Burundi

Serikali ya Tanzania imeanza rasmi hatua za kuwarejesha makwao raia wa Burundi waliovuliwa hadhi ya ukimbizi.
Ni katika hatua za kuifunga rasmi kambi ya Mtabila ambayo ni kambi pekee iliyokuwa ikihifadhi wakimbizi wa Burundi nchini humo wapatao elfu thelathini na saba.

Sanjari na uamuzi wa kuwarejesha makwao raia hao, shughuli hii inaambatana na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao hawako tayari kurejea Burundi.
Shughuli ya kuwarejesha makwao kwa hiyari raia wa Burundi waliokuwa wakimbizi hadi mwezi Agosti mwaka huu kabla ya kuvuliwa hadhi ya ukimbizi na serikali ya Tanzania,ilimalizika rasmi Jumatatu ambapo kuanzia leo kinachofuata dhidi ya wakimbizi hao ni kuandikishwa kwa kufuatwa kwenye maeneo wanakoishi kambini na kisha kupakiwa kwenye magari na kurejeshwa Burundi.
Akizungumza na mwandishi wa BBC mjini Dar es Salam Eric David Nampesya, mkuu wa kambi hiyo ambaye ni mwakilishi wa wizara ya Mambo ya ndani nchini humo, Bwana Frederick Nisajile, alisema utaratibu huo utakavyokuwa baada ya kukamilika kwa shughuli ya kurejea kwa hiyari ya 'Kimombo Voluntary repatriarition.'
Bwana Nisajile alisema inatarajiwa kuwa raia wa Burundi wapatao elfu moja watarejeshwa makwao kila siku katika utaratibu huu ambao pia utawahusisha maafisa wa idara ya Uhamiaji ili kuwakamata wale wote watakaokaidi kurejea makwao.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi UNHCR Bi Chansa Kapaya anasema hakuna uwezekano kwa Raia hao wa Burundi kutafutiwa nchi ya tatu kwa sababu wao si wakimbizi tena kwa wakati huu.
Nafasi hiyo haipo tena,nafasi kama hiyo hutolewa kwa wakimbizi,hawa walipokuwa wakimbizi zamani na kwa sasa walishavuliwa hadhi ya kuwa wakimbizi,kwa maana hiyo hawawezi kupewa nafasi ya kutafutiwa hifadhi katika nchi ya tatu,kwa maana hiyo suluhisho pekee kwao ni kurejea Burundi.
Kuanza kufungwa kwa Kambi hiyo ya Mtabila kunahitimisha miaka 19 tangu ilipofunguliwa mnamo mwaka 1993,wakati huo ilipoanza kupokea raia wa Burundi waliokimbia machafuko ya kivita yaliyofuatia mauaji ya aliyekuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Burundi hayati Melchior Ndadaye.
CHANZO-BBC

RUSHWA NJE NJE UCHAGUZI WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM

WAPAMBE NUSURA WAZICHAPE KAVUKAVU, UCHAGUZI KUFANYIKA DODOMA LEO

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima 

WAPAMBE NUSURA WAZICHAPE KAVUKAVU, UCHAGUZI KUFANYIKA DODOMA LEO
Full story



Mwandishi Wetu, Dodoma
WAKATI uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ukifanyika leo, suala la rushwa, makundi na wajumbe kutaka kuzipiga yalitawala jana.
Uchaguzi huo wa wazazi ndiyo wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili.
Tuhuma hizo za rushwa zimejitokeza licha ya juzi wagombea mbalimbali kukaririwa wakiyakana makundi ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na ajenda maalumu ya kusaka urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia chama hicho.
Kampeni na rushwa
Mmoja wa wajumbe kutoka mkoani Iringa aliuambia Mtandao huu kuwa tayari baadhi ya wajumbe wanaoonekana kuwa na msimamo mkali wamekuwa wakipewa Sh100,000 kila mmoja wakati wajumbe wengine wamekuwa wakihongwa kati ya Sh40,000 na 70,000.
“Nikimwona Rais Jakaya Kikwete nitamwambia. Hali hii siyo nzuri na haiwezi kuvumiliwa. Kama alivyosema juzijuzi hapa nilimsikia, lazima achukue hatua, la sivyo chama chetu kitakufa,” alisema mjumbe huyo ambaye aliomba asitajwe jina.
Katika hatua nyingine, makundi ya baadhi ya wajumbe waliokuwa wameketi katika moja ya baa maarufu mjini Dodoma, juzi usiku walitimka mbio baada ya kuona gari likiegeshwa pembezoni mwa baa hiyo.
Wajumbe hao waliokuwa kwenye harakati za kupanga mikakati ya kuzunguka katika nyumba za kulala wageni kwa ajili ya ‘kuonana’ na wajumbe, walitimka wakidhani kuwa gari hilo lilikuwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Wagombea wanaowania uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo juzi, kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na maslahi na makundi yanayodaiwa kushiriki katika vitendo vya kutoa rushwa katika uchaguzi huo unaofanyika leo. Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Martha Mlata alikataa kuzungumzia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo, unahitimisha uchaguzi wa jumuiya tatu za chama hicho, baada ya ule wa UWT na UVCCM ambazo zilizua malalamiko kutokana na kutawaliwa na madai ya rushwa.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifunga mkutano wa UWT na baadaye alipofungua ule wa UVCCM,   alikemea vitendo hivyo na kueleza athari za rushwa katika chaguzi za chama.

Mchuano wa wabunge
Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa UWT, mchuano mwingine mkali unaonekana katika kinyang’anyiro cha ujumbe wa Nec, huku kukiwa na idadi kubwa ya wabunge wanaowania nafasi hiyo.
Majina 16 yamepitishwa kuwania viti vitatu vya Nec kwa upande wa Tanzania Bara, wakati kwa upande wa Tanzania Visiwani majina yaliyopitishwa ni saba kugombea nafasi mbili.
Miongoni mwa wanaowania nafasi tatu Bara ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, Stella Manyanya na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu.
Pia wamo wabunge ambao majimbo yao yapo kwenye mabano Said Bwanamdogo (Chalinze), Vita Kawawa (Namtumbo), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) na Mbunge wa zamani wa Viti Maalumu, Esther Nyawazwa.
Wengine katika kundi hilo ni Norad Kigola, Priscilla Mbwaga, Dk Salim Chikago, Jeremia Wambura, Bernard Murunya, Thobias Mwilapwa, Paulo Kirigini na Clementina Mollel.
Kutoka Zanzibar, wanaowania nafasi mbili za Nec ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Perera Ame Silima, Abdulla Khamis Feruz, Ali Suleiman Othman, Fatuma Abeid Haji, Panya Ali Abdalla, Twaha Ally Muhajir na Hassan Rajab Khatib.
Pia mkutano wa leo unatarajiwa kumchagua Makamu Mwenyekiti, nafasi inayowaniwa na Hassan Rajab Khatib, Ali Issa Ali na Dogo Iddi Mabrouk.
Utawachagua pia wajumbe wa Baraza Kuu la Wazazi na wawakilishi wa jumuiya hiyo katika mabaraza ya UVCCM na UWT.

Vijembe vya kampeni
Kampeni zimekuwa zikipamba moto kadri muda wa uchaguzi unavyokaribia na mbinu mbalimbali zimekuwa zikitumika ili kujihakikishia ushindi.
Magari mengi yamepambwa picha nyingi za wagombea, wapambe wanapita sehemu mbalimbali kuomba kura na kuta za uzio wa ofisi za CCM zimechafuka kwa picha za wagombea.
Ushindani mkubwa unaonekana kuwa baina ya Barongo na Bulembo ambao jana walikuwa kivutio kikubwa walipokutana katika ofisi za CCM Makao Makuu, Dodoma ambako walikumbatiana kisha kuanza kurushiana vijembe.
Bulembo alisema: “Nilipomkuta anachukua fomu, nilimwuliza mwalimu wangu huyu (Barongo) kwamba nilidhani kwamba sasa unaniachia nikutue mzigo, kumbe bado tena nawewe unagombea?”
Barongo alimjibu akisema: “Hilo haliwezekani kabisa, ujue ninyi bado watoto hamjakomaa bado mnahitaji kuongozwa, kwa hiyo wewe tulia kwanza muda mwafaka ukifika nitakukabidhi.”
Jana asubuhi, Bulembo alifika katika Viwanja vya Bunge kuomba kura kwa baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuiya hiyo.
Muda mfupi kabla ya wabunge kuingia ukumbini, Bulembo alikuwa nje ya lango kuu la kuingilia kwenye ukumbi wa Bunge na kila mbunge aliyejitokeza alimsalimia kisha kuomba kura kwa wale ambao ni wajumbe hao.
Mlata jana kwa muda mrefu hakuonekana katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM na taarifa zinasema huenda alikuwa akihudhuria kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo kilichofanyika jana katika Chuo cha Mipango.
Licha ya kutokuwapo kwake, kulikuwa na vijana wachache waliokuwa wamevalia mabango makubwa yenye picha yake, vifuani na kwenye migongo yao wakimpigia kampeni.
Wafuasi nusura wazichape
Wakati Bulembo na Barongo wakirushiana vijembe kwa furaha, watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wao nusura wachapane makonde walipokuwa wakiimba nyimbo za hamasa CCM Makao Makuu.
Wafuasi hao jana walikuwa wakizunguka wakiwa na mabango yenye kuwanadi wagombea hao katika ofisi hizo kati ya saa sita na saa nane mchana huku wakiimba nyimbo za hamasa.
Hali hiyo ilisababisha kutosikilizana katika eneo hilo, hivyo kuwalazimu maofisa wa CCM kuviamuru kuondoka na kuelekea katika mbele ya jengo la vikao vya NEC maarufu kama White House. Viliitikia wito na kwenda huko ambako viliendelea kuimba nyimbo za hamasa.
Wakati vikiwa katika eneo hilo, wafuasi hao walianza kurushiana maneno makali kwa huku kila upande ukidai kufanyiwa rafu na upande mwingine, hali iliyozua tafrani iliyodumu kwa zaidi ya dakika 20.
Hata hivyo baadhi ya makada wa pande hizo mbili, walitumia busara na kuwatuliza na kila kikundi kuelekea upande tofauti na kuhitimisha shamrashara hizo.
Chanzo-gazeti la  Mwananchi

Tuesday, October 30, 2012

WAANDISHI WA HABA RI KUTOKA MIKOA MBALIMBALI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO WA KUANDIKA HABARI KUHUSIANA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibanmba akitoa Mada ya Katiba mpya-Tulipotoka,Tulipo na Tuendako kwa Waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Dodoa Hotel.Picha chini zinaonyesha matukio mbalimbali kwenye mafunzo hayo
 Deus kibamba akionyesha Katiba ya sasa inayotakiwa kufanyiwa mabadiliko
 Akionyesha utata kwenye Katiba ya sasa

 Wanahabari wakinukuu ili wasipitwe na kitu kwa ajili ya kujikumbusha
 Wakifuatilia kwa makini
 Akionyesha kitu kuhusiana na Katiba

Wanahabari wakifuatilia kwa makini.

Nini htma ya mgogoro waTanzania na Malawi katika kugombea Ziwa?

Ziwa  Nyasa  ambalo Wamalawi wanaliita Ziwa Malawi

Hali ya wasiwasi inatanda kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mzozo wa mpakani ambao umekuwa ukitokota kwa miaka mingi lakini sasa umefika daraja ya juu katika wiki chache zilizopita.
Mzozo unahusu umiliki wa ziwa Malawi ambalo ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika na ambalo linapakana na Malawi, Tanzania na Msumbiji.
Tangu miaka ya sitini, Tanzania na malawi zimekuwa zikizozana kuhusu umiliki wa ziwa hilo, lakini mzozo huu wa sasa umekuwa mbaya zaidi hasa ikizingatiwa ripoti za kupatikana gesi na mafuta katika ziwa hilo.
Msumbiji haijahusika kivyovyote na mzozo huu.
Nini hasa kinazozaniwa?
Fahari ya nchi na maswala ya kujiendeleza kiuchumi kwa Malawi na Tanzania kila mmoja akisimama kidete kusisitiza msimamo wake.
Kwa Tanzania, ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago Niassa.
Malawi na Tanzania ni koloni za zamani za Uingereza wakati Msumbiji ilikuwa chini ya ukoloni wa Ureno. Uingereza iliichukua Tanzania kutoka kwa Wajerumani baada ya wao kushindwa katika vita vya kwanza vya dunia.
Kando na ripoti za kuwepo mafuta na gesi katika ziwa hilo, ziwa lenyewe ni kivutio kikubwa cha watalii.
Malawi inasema inashauriana na Msumbiji kuhusiana na uchimbaji wa mafuta katika siku za baadaye ili kuzuia mzozo wa kidiplomasia .
Je hii ni mara ya kwanza kwa mzozo huu wa ziwa Malawi kutokea?
Hapana. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania.
Makubaliano hayo yaliafikiwa na Muungano wa Afrika na Tanzania ikaitikia ingawa shingo upande. Mzozo mpya kati ya nchi hizo ukaripotiwa tena kati ya mwaka 1967 na 1968.
Rais Joyce Banda anataka Muungano wa Afrika kutatua mzozo wa ziwa Malawi

Nini chanzo cha mzozo huu wa hivi sasa?
Mwezi Septemba mwaka 2011, Malawi ilitoa leseni ya kuchimba mafuta kwa kampuni ya British Surestream Petroleum Limited. Sehemu iliyotolewa kwa uchimbaji wa mafuta ni sehemu yenye mraba wa kilomita 20,000 sehemu ambayo Tanzania inasema ni yake.
Vyombo va habari viliripoti mwezi Julai kuwa , mitumbwi ya wavuvi na ya watalii kutoka Malawi inavuka na kuingia upande wa Tanzania
Tanzania nayo ikasema kuwa itatafuta ushauri kutoka jamii ya kimataifa ikiwa nchi hizo hazitaweza kusuluhisha mzozo huo zenyewe.
Nchi hizo mbili zilifanya mkutano mwezi Julai mjini Dar es Salaam kuhusu mzozo wa mpaka
Tarehe 30 mwezi Julai, Tanzania, iliitaka Malawi kusitisha shughuli za kutafuta mafuta kwenye ziwa hilo hadi mzozo kati yao utakaposuluhishwa lakini maafisa wa Malawi wakasisitiza kuwa ziwa hilo lote ni la Malawi na kwamba hakuna sababu ya kusitisha shughuli zake za kutafuta mafuta
Tanzania ilisema kuwa ikiwa Malawi itaendelea na shughuli zake kutafuta mafuta itaathiri mazungumzo yanayoendelea kati ya nchi hizo mbili.
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe alisema kuwa ikiwa Malawi haitafuata maagizo hayo, Tanzania itaiona hatua yake kama kitendo cha uvamizi.
Nini kimesababisha hofu ya hatua za kijeshi?
Hofu ya mzozo kutokota na kuwa mbaya zaidi ilijitokeza wakati Tanzania iliposema kuwa italinda mipaka yake na kuzingatia sheria za kimataifa.
Kisiwa cha Likoma kwenye ziwa Malawi
Maafisa kutoka pande zote walikutana tena mjini Dar es tarehe 4 na 5 mwezi Agosti, lakini Malawi ilisisitiza kuwa haitasitisha shughuli zake za kutafuta mafuta
Waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania Membe alinukuliwa akisema katika taarifa yake kali kuwa watapambana na Malawi kijeshi.
Matamshi yake aliyatoa bungeni kulingana na taarifa kwenye mtandao wa The Guardian.
Mtandao wa Nyasa Times ulitoa taarifa kuonyesha kuwa kuna taharuki kati ya nchi hizo mbili kuhusu mpaka wa Ziwa , lakini waziri wa usalama wa ndani wa Malawi Uladi Mussa akasisitiza utulivu.
"Tunashauriana na serikali ya Tanzania na mambo yatakuwa sawa. Ikiwa hali itakuwa mbaya kesi hii tutaiwasilisha kwa mahakama ya kimataifa ya haki" alisema waziri huyo.
Mnamo tarehe 11 mwezi Agosti, Rais wa Malawi Joyce Banda alisema kuwa yuko tayari kufanya kila hali ikiwemo kujitolea maisha yake kwa sababu ya watu wa Malawi.
Watanzania wanaoishi karibu na ziwa hilo wakaanza kutoroka wakihofia vita.
Je kumekuwa na juhudi za kidiplomasia kumaliza mzozo huu?
Maafisa wa chi hizi mbili walikutana kati ya tarahe 20 na 25 mwezi Agosti, mjini Mzuzu,Kaskazini mwa Malawi, lakini Rais Banda akarejelea msimamo wake kuwa ni wazi kuwa Ziwa hilo ni la Malawi.
Wakati wa mkutano wa chi za ukanda wa Afrika Kusini (SADC),nchini Msumbiji, Rais Banda alikutana na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete, aliyekana kuwa nchi yake inajiandaa kwenda vitani na Malawi. Kikwete alisema kuwa matamshi kuhusu vita yalitolewa na wanasiasa wa upinzani ambao wana jazba.
Mjini Mzuzu mkutano uliisha bila maafikano. Siku chache baadye Rais Banda alisema kuwa mzozo huo utasuluhishwa katika mahakama ya kimataifa ya ICJ.
Malawi baadaye ilikosa kufika kwenye mkutano kati yake na Tanzania kati ya tarehe 10 na 15 Oktoba kulingana na mtandao wa The Citizen
Rais Jakaya Kikwete anataka mahakama ya kimataifa kuhuzu mizozo kutatua mzozo kati ya nchi yake na Malawi
Je Juhudi za kidipmomasia zimefanikiwa?
Hapana. Mwanzo Tanzania imepandisha mzozo huo kwenye daraja ya juu zaidi kwa kutoa ramani mpya inayoonyesha mpaka ulio katikati mwa ziwa Nyasa.
Afisaa mmoja kutoka wizara ya nyumba wa Tanzania amesema kuwa ramani hiyo inaondoa hali ya kutoelewana kwa kuonyesha mpaka unaozozaniwa.
Tarehe tatu mwezi Oktoba Rais Joyce Banda aliakhirisha mkutano kati ya nchi hizo mbili hadi Tanzania itakapojieleza kuhusu ramani hiyo.
Alimtuhumu Rais Kikwete kwa kumhadaa na kwamba anapanga kulipua mitumbwi ya Malawi katika ziwa hilo.
Kikwete alitangaza siku hiyo hiyo kuwa Tanzania itawasilisha kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya mizozo.
Kwa upande wake Rais Banda ameutaka muungano wa Afrika kuingilia kati mozo huo.
Je mzozo huu ni kuhusu mpaka tu au kuna liengine?
CHANZO-BBC

Ahukumiwa miaka 25 jela kwa ushirikina na uuzaji wa wasichana

 Na Mashirika ya  habari

Osezua Osolase
Mwanaume aliyewafanyia vitendo vya kishirikina au ''Juju'' wasichana ambao alikuwa anawalangua kutoka nchini Nigeria hadi barani Ulaya amehukumiwa jela miaka 20 nchini Uingereza.
Osezua Osolase raia wa Nigeria na mwenye umri wa miaka 42,kutoka mtaa wa Gravesend, Kent aliwatumia wasichana maskini kwa kuwahadaa kuwa wangepata maisha mazuri baada ya kufika alikokuwa anawapeleka.
Jaji Adele Williams wa mahakama ya Canterbury Crown alisikia katika ushahidi uliotolewa mahakamani dhidi ya mshtakiwa na kumwambia kuwa alikosa utu kwa kufanya vitendo kama vile.
Osolase alipatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo ubakaji na kumfanyia dhulma za kingono mtoto mdogo.
Jopo la majaji lilisikia katika kesi hii iliyoisha siku ya Ijumaa kuwa vitendo vya kishirikina pia vilitumiwa kuwatia hofu waathiriwa watatu wa vitendo vya Osolase.
Jaji alisema kuwa Osolase ambaye ni mwathiriwa wa HIV, aliwatia hofu waathiriwa wake ili kuwalazimisha kumtii na kukaa kimya.
"umetenda dhulma na kuwafanyia unyama waathiriwa vitendo vyako'' jaji alimwambia bwana Osolase.
"wewe sio mwaminifu hata kidogo. Una kiburi na ukatili, hauna ubinadamu wala huruma kwa waathiriwa wako.'' aliongeza jaji
Aidha jaji Williams alisema kuwa bwana Osolase aliwaharibu wasichana hao wakati alijua kuwa ana virusi vya HIV na hata kumbaka msichana mmoja wakati akijua alifanya kitendo kibaya sana .
Osolase aliwapeleka wasichana hao kwake nyumbani kabla ya kuwapeleka barani Ulaya kufanya kazi ya ukahaba.
Mahakama ilisema kuwa mwanaume huyo arejeshwa nyumbani Nigeria atakapomaliza kuhudumia kifungo chake.
Mmoja wa wasichana alielezea yaliyomkuba wakati akifanyiwa vitendo vya kishirikina, alisema alitolewa damu mwilini , kisha akakatwa nywele zake za kichwani na sehemu zake za siri.Baada ya hapo alilishwa kiapo kutosema chochote.
Osolase alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Stansted mwezi Aprili alipojaribu kupanda ndege mwaka jana
CHANO-BBC.

Purukushani migodini nchini A. Kusini

Wafanyakazi wa migodi wanaogoma

Makabiliano makali yamezuka kati ya Polisi na wachimba migodi katika mgodi wa madini ya Platinum wanaogoma Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg.
Polisi waliwafyatulia risasi za mipira na kuwarushia waandamanaji gesi ya kutoa machozi katika makabiliano hayo ambapo wachimba madini hao wanataka nyongeza ya mishahara.
Kampuni ya Anglo-American Platinum imekubali kuwarudisha kazini wachimba madini elfu kumi na mbili waliofutwa kazi na kuwalipa malimbikizo ya mishahara, suala lililokataliwa mbali na wachimba madini hao.
Msururu wa migomo ya wachimba migodi na madini imeendelea kukumba Afrika Kusini katika miezi ya hivi karibuni na kuathiri pakubwa uchumi wa nchi hiyo.
CHANZO-BBC

Kiongozi wa upinzani Rwanda ahukumiwa jela

Victoire Ingabire
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire amehukumiwa miaka minane gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la uhaini
Viongozi wa mashtaka walitaka afungwe maisha jela kwa kutishia usalama wa nchi.
Mahakama imempata na hatia ya kupuuza mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Ingabire hakuwa mahakamani wakati hukumu ilipotolewa dhidi yake kwani amekuwa akisusia kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo akisema imeshinikizwa ksiasa,.
Alikamatwa mwezi Aprili mwaka 2010 na kuzuiwa kushiriki uchaguzi uliofanyika mwaka huo.

CHANZO-BBC

Monday, October 29, 2012

RUVUMA YATIKISWA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,SIASA ZATAWALAMAJI YAWA BIDHAA ADIMU


RC AMETOA SIKU KUMI KWA WATU WANAOHARIBU MAZINGIRA VINGINEVYO WATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA
 kundi kubwa la ng'ombe katika poli la hifadhi ya selous.
Chini,picha zinaonyesha misitu ikiwa imeteketezwa na watu wanaofanya biashara ya mkaa



 miti ikiwa imekatwa na msitu kuwa kipara.

 Msiitu ukiwa umebaki kipara kutokana na uharibifu wa mazingira.

VIGOGO 10 WAHUSISHWA MABILIONI YALIYOFICHWA USWISI,ZITO ASISITIZA NYARAKA ZIPO ADAI HOSEA NDIYE ANAYEZIZUIA



Mheshimiwa Zitto Kabwe 
By Boniface Meena  
ZITTO ASISITIZA NYARAKA ZIPO, DK HOSEAH NDIYE ANAYEZIZUIA


VIGOGO 10 wametajwa kuhusika katika kashfa ya kuficha Sh303.7 bilioni katika benki mbalimbali nchini Uswisi.
Katika orodha hiyo inadaiwa kuwa yupo kiongozi mmoja mwandamizi mstaafu, maofisa watatu wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mawaziri wastaafu ambao baadhi yao bado ni wabunge na aliyewahi kuwa kiongozi mwandamizi wa Benki Kuu Tanzania (BoT).
Majina hayo ambayo mwandishi wetu amefanikiwa kuyaona, yamo katika orodha ya mchunguzi mmoja wa kimataifa wa masuala ya ufisadi (jina tunalo).
Juzi, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alimshukia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah akimtuhumu kuandika barua Uswisi akisema Tanzania haina masilahi na mabilioni ya fedha yaliyofichwa katika benki zilizopo nchini humo. Hata hivyo, Dk Hoseah alikanusha madai hayo akisema hajawahi kufanya hivyo.
Akizungumza jana Zitto alisisitiza kauli yake akisema: “Sijawahi kumsema Dk Hoseah kwa lolote, kwa nini leo nimsingizie? Yeye mwenyewe anajua ushirikiano niliompa wakati wabunge wanapinga yeye asichunguze malipo ya posho mara mbili kwa wabunge.”
“Nilisimama kidete kusema Takukuru wapo sahihi na mimi nilikwenda mwenyewe kwao kuhojiwa na kuagiza wajumbe wa kamati yangu (Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma), waende kuhojiwa. Spika aliyestaafu (Samuel Sitta) akaizima kashfa ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili. Mwulizeni amesahau? Sasa leo nimzushie ili iwe nini?.”
Alisema orodha ya Watanzania wenye fedha huko Uswisi, ipo na ameiona na nyaraka zinaweza kutolewa kwa taasisi za Serikali tu.
“Dk Hoseah kazuia nyaraka hizo. Akitaka nimwonyeshe mtu anayeweza kutoa nyaraka hizo, nipo tayari isipokuwa aahidi kuiweka wazi,” alisema Zitto.
Alisema katika orodha ambayo Waziri wa Fedha wa Ufaransa anayo, kuna Watanzania lakini akaituhumu Serikali akisema haitaki kufuata njia halali za kupata orodha hiyo kwa kuwa viongozi wengi na wafanyabiashara wakubwa wana akaunti katika benki za Uswisi.
Juni 26, mwaka huu gazeti hili lilichapisha habari kuhusu utoroshwaji wa fedha hizo na kueleza kuwa Polisi wa Kimataifa (Interpol) nchini kwa kushirikiana na Takukuru inachunguza suala hilo.
Kiasi hicho cha fedha kimedaiwa kuingizwa katika akaunti za Watanzania na kampuni moja ya uchimbaji mafuta na kampuni kadhaa za uchimbaji madini ambazo zinafanya kazi Tanzania.
Chanzo hicho kiliongeza kwamba kiasi hicho cha fedha kipo katika akaunti sita tofauti zinazomilikiwa na Watanzania wakiwamo wanasiasa wakubwa.
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa tangu akaunti hizo zifunguliwe, wamiliki wake halali hawajawahi kuingiza hata shilingi.
“Uchunguzi wetu unaonyesha kuwa fedha hizo zipo katika akaunti sita tofauti ambazo zinamilikiwa na wanasiasa wakubwa nchini na wenzetu wa Uswisi wameeleza fedha hizo zimeingizwa na kampuni kadhaa ambazo zinahusika na mafuta pamoja na madini hapa nchini,” kilidokeza  chanzo hicho.
Kugundulika kwa kiasi hicho cha fedha katika benki za Uswisi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Taifa ya Uswisi (SNB) iliyotolewa mwaka huu.
 CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

Marekani yatahadharishwa kuhusu 'Sandy'

 29 Oktoba, 2012 - Saa 07:09 GMT
Kimbunga Sandy

Rais wa Marekani Barack Obama, amewatahadharisha wamarekani kuchukulia kwa uzito kimbunga Sandy huku maafisa wakianza kufunga eneo la Mashariki mwa pwani ya nchi hiyo wakisubiri kimbunga hicho kupiga.
Majimbo kadhaa yametangaza hali ya hatari huku mamilioni ya watu wakiathiriwa na dhoruba kali wakati shule na barabara zikifungwa.
Wataalamu wanahofia kimbunga hicho huenda kikawa kikali mno wakati kitakapopiga sehemu za nchi hiyo.
Baadhi ya mikutano ya kisiasa ya hadhara imesitishwa huku Rais Obama akionya watu kuchukua hatua za kujikinga na athari za zaidi za kimbunga hicho.
Usafiri wa kimataifa kutoka nchini humo umeathirika sana. Mashirika ya ndege ya Ufaransa, Uingereza na Virgin Atlantic yamesitisha safari zao katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo ikiwemo miji ya , New York, Baltimore, Newark, Washington, Boston na Philadelphia kuanzia leo.
Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa vimbunga, saa nane asubuhi ya leo, kimbunga hicho, kilianza kuelekea Kaskazini kikienda kwa kasi ya kilomita 760, Kusini Mashariki mwa mji wa New York.
Hali ya tahadhari imetangazwa katika miji ya Maryland, New York, Pennsylvania, Virginia, Washington DC na North Carolina.
Kimbunga hiki kinatoa fursa kwa Rais Obama kuonyesha uongozi wake mbali na siasa na ikiwa atakosa kuonyesha uongozi unaostahili huenda wakosoaji wake wakatumia fursa hiyo kumponda na kumlaumu kwa kosa lolote.
CHANZO-BBC

Sunday, October 28, 2012

CCM YASHINDA VITI VYA UDIWANI MKOANI RUVUMA,CCM CHADEMA WAKATANA MAPANGA

 Mmoja wa Majeruhi wa majeruhi wa vurugu zilizotokea  oktoba 27m Bw.  Mashaka Mbawala wakati wa kampeni za lala salama  na uchaguzi ulifanyika oktoba 28 mwaka huu.ccm  imerejesha viti vyote viwili.
Mashaka akitafakari jambo na kueleza kuwa wamekuwa wakitumika kwa maslahi ya watu hivyo hataendelea tena kutumika kisiasa kutokana na kipigo alichokipata

UVCCM WAZICHAPA KAVU KAVU DAR


Wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), wanaomuunga mkono Mwenyekiti mpya wa Taifa wa Umoja huo, Khamis Sadifa Juma na viongozi wenzake, wakimtwanga mmoja wa wanachama waliojitokeza kumpinga mwenyekiti huyo kwa mabango(wa pili kushoto), wakati alipowasili  makao makuu ya umoja huo Dar es Salaam jana, akitokea mkoani Dodoma alipochaguliwa kushika nyadhifa hiyo. Picha na Rafael Lubava 
 


“Kama Rais Jakaya Kikwete kweli yuko makini na kauli zake ni za dhati, basi atengue matokeo ya uchaguzi huu maana kanuni zimekiukwa na kusema kweli rushwa ilitawala. Atumie nafasi yake kurejesha hadhi ya chama kwani huu uchaguzi ni batili,” alisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Morogoro, Augustine Matefu.
 
Full Story....


SHAMRASHAMRA za kumpokea Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) , Khamis Sadifa Juma jijini Dar es Salaam jana ziligeuka uwanja wa vita baada ya makundi yanayopingana kuchapana makonde.

Tafrani hiyo ilianza baada ya kundi moja la vijana waliokuwa wanane kutokea likiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kupinga ushindi wa mwenyekiti  huyo, wakati  utambulisho wa ugeni huo ukiendelea katika ofisi za makao makuu ya UVCCM, zilizopo jijini Dar es Salaam.

Baada ya kundi hilo kujitokeza na mabango yao, ndipo vijana wa upande wa Mwenyekiti (Juma), walipoanza kuwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata baadhi yao.

Kukiwa hakuna msaada wa Polisi, vijana hao walilishambulia kundi hilo kwa muda, huku baadhi yao wakitiwa nguvuni na vijana hao na kuingizwa katika ofisi ya UVCCM huku waandishi wa habari wakizuiwa kuwahoji watuhumiwa wala kuingia ndani ya ofisi hiyo.

‘’Hatutaki waandishi humu ndani, tokeni na asiingie mtu, hawa tutashughulika nao wenyewe, wanatusumbua mno hawa kwa siku nyingi,” alisikika mmoja wa vijana hao akiongea kwa sauti ya juu.
Baada ya purukushani hizo zilizodumu kwa zaidi ya nusu saa, hali ya hewa ilitulia na ratiba iliendelea huku vijana wengine wanaomuunga mkono mwenyekiti wao wakichukua jukumu la kulinda usalama wa eneo hilo na kuwapeleka Kituo cha Polisi Mnazi Mmoja vijana wawili waliowakamata kwa mahojiano.
Mwenyekiti mpya wa UVCCM alitamba kuwa atapambana na watu wanaotaka kuvuruga umoja huo.
Alisema: “Mimi ni mwanajeshi nimekaa kwenye kambi nyingi za jeshi, hivyo naelewa nitakavyopambana nao.”

Viongozi wa Kitaifa
Hata hivyo, sherehe hizo hazikuhudhuriwa na kiongozi yeyote wa kitaifa wa CCM.

Akizungumza baada ya mapokezi hayo, Mwenyekiti  wa UVCCM Taifa aliwataka vijana kuwa na umoja akisema kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki ni kujenga chama na kuhakikisha CCM inashinda katika chaguzi zote.

‘’Kilichobaki sasa ni kujenga chama, haipendezi kuendeleza uhasama ndani ya chama, sisi sote ni wamoja na tuache makundi kwani nayachukia na kuwachukia wale wanaoanzisha na kuendeleza makundi,’’ alisema Khamis Sadifa Juma.

Wiki iliyopita, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa UVCCM mjini Dodoma, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walikutana na waandishi wa habari na kulalamika kwamba rushwa ilitawala uchaguzi huo, huku wakiwatuhumu viongozi wa UVCCM na baadhi ya makada wa chama hicho kwa kuhusika na vitendo hivyo.

Waliotajwa ni pamoja aliyekuwa makamu mwenyekiti wa umoja huo, Beno Malisa, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, Bashe na mtoto wa Lowassa, Fredy.

“Kama Rais Jakaya Kikwete kweli yuko makini na kauli zake ni za dhati, basi atengue matokeo ya uchaguzi huu maana kanuni zimekiukwa na kusema kweli rushwa ilitawala. Atumie nafasi yake kurejesha hadhi ya chama kwani huu uchaguzi ni batili,” alisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Morogoro, Augustine Matefu.

Walidai kuwa Bashe, ndiye aliyekuwa mratibu wa uingizaji wa fedha katika eneo la mkutano ambazo zilitumika kugawanywa kwa wajumbe na kwamba Malisa na Shigela waligawa Sh1 milioni kwa viongozi wa mikoa kama hatua ya kumpigia kampeni mmoja wa wagombea walioshinda.

Hata hivyo, Bashe alikanusha tuhuma hizo akisema siyo kweli na kuongeza: “Mimi sijatumwa na Lowassa, wala sifanyi kazi na Lowassa. Nafanya kazi ya CCM, lakini nampenda sana Lowassa kwa sababu ni mmoja wa viongozi na makada wa chama, ambao wameonyesha mapenzi ya dhati kwa CCM na uvumilivu wa hali ya juu.”

Kada mwingine, Livamba Adinan Selemani alisema: “Vijana kweli tumempuuza Rais, kweli mtu ambaye hana hela hawezi kupata uongozi UVCCM, kwa maana nyingine nchi yetu inakwenda pabaya. Watu wachache wenye fedha wanaweza kuamua kufanya wanachotaka, hivyo ndivyo uchaguzi wetu wa vijana ulivyokuwa.”

Mjumbe mwingine, Kichanta Selemani alisema malalamiko ya viongozi wa UVCCM kuwapendelea baadhi ya wagombea yalifikishwa kwa Lukuvi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Wakati makada hao wa CCM wakizungumza na waandishi wa habari, lilitokea kundi jingine la makada wa chama hicho ambao walianza kuzozana na wenzao wakisema kuwa malalamiko yao yanatokana na kushindwa na kwamba walitaka kutumia “Viongozi wa ngazi za juu za CCM” kuwachagulia vijana viongozi.
CHANZO-MWANANCHI

Friday, October 26, 2012

AJALI IMETOKEA MAENEO YA BOMBAMBILI NA KUSABABISHA KUPASUKA USONI KWA DEREVA PIKIPIKI

Gari lililogongwa
Ajali hii imetokea maaneo ya white house jirani na ofisi za Tbc songea majira ya saa 5:20 jioni ,
Ajal hii imehusisha dereva pikipiki (yeboyebo) na gari aina ya Vitara iliyokuwa ikitokea msamala ikielekea mjini.
Chanza cha hajali hiyo kwa mashuhuda walioiona wamedai dereva wa gari aina ya vitara alisimama gafla kwenye matuta badala ya kupunguza mwendo.
Ndipo kijana huyo ambaye ni dereva pikipiki(yeboyebo) alipomva na kumgonga kwa nyuma na kuchanika usoni, Kijana huyo amepelekwa hospital ya mkoa wa Ruvuma kupata matibabau.
Pia wamesema dereva wa Gali hilo ambaye akufahamika jina kwa haraka alikuwa akiendesha gari huku amelewa ,
Aidha wamelaana juu ya hawa madereva wanaoendesha magari wakiwa wamelewa kwani wanasababisha ajari nyingi barabarani pia wanaiomba serikali kuchukua mkondo wake kwa hawa madereva wanaoendesha huku wamelewa.
Ilikupunguza ajali nyingi barabarani pia nakuwataka hawa madereva wa pikipiki(Yeboyebo) kuendesha kwa umakini wawapo barabarani kwani wamekuwa wakiendesha kwa kutofata sheria za barabarani.
Huyu mzee alievaa shati la mistari ndie mwenye gari
  Askari wa Barabarani wakiwa eneo la tukio
Mashuhuda wakiangalia ajali

madereva pikipiki(yeboyebo) wakitoa ushirikiano kwa Askari wa barabarani
 
     CHANZO-de masho.blogspot.com