Monday, January 28, 2013

MWANAMKE MWENYE HIPS KUBWA DUNIANI APATIKANA

             .Ni Mmarekani Mikell Ruffinel


LOS ANGELES, Marekani
WAKATI wanawake wengi duniani wakihangaika kukuza ukubwa wa makalio yao, huku wengine wakitumia njia ya kuvaa taiti zenye hipsi, wanaume wengi huko mjini Los Angeles wamejikuta  wakigeukageuka kumwangalia mwanamke mwenye makalio makubwa kupita kiasi kila apitapo njiani.
Mikel Ruffinelli ni mwanamke ambaye mpaka sasa ‘ameishavunja shingo’ za wanaume wengi. Makalio yake na hispi zake za asili zimemfanya atawazwe kuwa mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake wote duniani.
Mikel anayeishi nchini Marekani hajatumia dawa za mchina wala dawa zozote kama wafanyavyo akina dada wengine na ndiye aliyetambulishwa kuwa ndiye mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake duniani. Mpaka sasa mama huyo mwenye familia yake ana  hispi zenye  mita 2.44.
Umbile lake halikuja hivihivi, bali alikuwa ni mtu mwenye umbile la kawaida, licha ya kukiri kuwa ndugu zake wengi wana maumbile makubwa.
Hipsi za mwanamama huyo zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku kadiri alivyokuwa akijifungua watoto wake.
Mikel Ruffinelli, ambaye ni mama wa watoto wanne ana umri wa miaka 39 na ni mkazi wa Los Angeles amejisifia kuwa umbile lake limekuwa likiwachanganya wanaume wengi.
Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, hispi zake zina mzunguko mkubwa wa inchi 96.
“Nalipenda umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet,” alinena Mikel na kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa siyo wale wembamba wembamba.”
Lakini kauli hiyo, imepingwa vikali na Jennifer Lopez, Kim Kardashian na Beyonce ambao wanasema inategemea na mwanaume husika na namna kile anachokipenda, lakini wakati mwingine hutegemea na mazoea ya mwanamume.
Mikel pamoja na kutamba na maumbile yake hayo ambayo anadai ni urithi toka kwenye familia yake ambapo karibuni ndugu zake wote wa kike nao wana hispi kubwa.
Mikel amelazimika kuishi tofauti ili aweze kuendana na umbile lake, hawezi kuenea kwenye gari ndogo hivyo gari analoliendesha ni kama lori.
Akiwa nyumbani kwake inabidi akae kwenye makochi yaliyotengenezwa kwa chuma badala ya mbao, pia kitanda chake nacho ni futi saba kwa saba.
Mume wa Mikel, Reggie Brooks mwenye umri wa miaka 40 ameelezea kupagawishwa na umbile la mkewe na ameongeza kuwa kila siku humsifia kwa kumwambia jinsi gani alivyo mrembo.
Mikel na mumewe wapo kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa na wamefanikiwa kupata watoto watatu ambapo mtoto wa kwanza wa Mikel alizaliwa katika ndoa yake ya kwanza kabla hajaachika na kuolewa na Reggie.
  CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

Sunday, January 27, 2013

MWAKYEMBE ATAMBA KUIFANYA BANDARI YA DAR KUWA YA KISASA

 
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe. 

HABARI KAMILI

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametamba kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa ya mfano duniani kwa utoaji wa huduma bora za upakiaji na upakuaji kwa wananchi wa ndani na nje ya nchi.
Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na madereva wa malori na wadau wengine wa bandari baada ya madereva hao kumtaka awasikilize kero zao wakati alipokuwa bandarini hapo na msafara wa mawaziri kutoka nchini Uganda.
Dk Mwakyembe alilazimika kurudi bandarini hapo jana baada ya juzi kuombwa na madereva hao kuonana naye ili wamweleze kero zao na yeye aliahidi kurudi kesho yake ambayo ilikuwa jana.
Katika mazungumzo hayo Waziri Mwakyembe aliwataka madereva hao kuwa wawazi kueleza kero zote zinazowakabili bandarini hapo kwa kuwa yeye hasa ndiye mwenye dhamana ya kurekebisha na kuboresha huduma bandarini.
Wadau hao walimweleza waziri kuwa kero ni nyingi zikiwamo za upatikanaji wa vibali vya upakiaji na foleni ya magari, ratiba na muda wa kupakia, mwingiliano wa kazi za meli na malori ya mizigo na madai ya rushwa kwa wafanyakazi hasa wa kitengo cha upakiaji wa makontena bandarini hapo.
Waziri aliwataka watendaji bandarini hapo kuondoa urasimu kwani hakuna haja ya malori ya kusafirisha mizigo nje ya nchi kuwa na foleni ndefu bandarini hapo kwa kuwa suala hili linapunguza ushindani wetu katika soko.
“Hakuna haja ya malori ya mizigo yaendayo nje ya nchi kuchelewa kutoka, na ndiyo sababu inayofanya Mombasa wanatuzidi kwa ufanisi” alisema Mwakyembe.
Katika kuimarisha utoaji wa huduma waziri aliwataka TICTS kufanya kazi kwa saa 24 kila siku na kwa siku saba ili kuondoa msongamano wa malori tofauti na sasa ambapo mizigo hupakiwa siku za Jumatatu mpaka Jumatano kuanzia saa 5.00 asubuhi kwa awamu tatu kwa siku kama alivyothibitishiwa na Meneja wa TICTS Bandari ya Dar es Salaam, Daniel Tawale. Akitafuta suluhu ya kero zote za bandarini hapo toka kwa wadau tofauti, waziri alisema kuwa kamati ya muda iundwe ili kwa muda wa siku saba ifanye utafiti na imshauri nini cha kufanya ili kuinusuru bandari hiyo.
“Nataka niunde kamati ndogo sasa hivi ili ichunguze na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike na inipe majibu ndani ya siku saba ofisini kwangu ili niweze kufanya uamuzi sahihi kwa kuwa ni lazima tubadilike ili tuweze kuhudumia wateja wengi wanaotuzunguka” alisema waziri wakati akiunda kamati hiyo.
Waziri aliunda kamati ndogo yenye wajumbe 10 toka sekta tofauti za wadau wa bandari ambayo itaongozwa na Daniel Silla toka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili kuchunguza na kubainisha kero zilizopo bandarini hapo na suluhisho zake.
Wajumbe wengine walioteuliwa ni sekta zao kwenye mabano ni Castrol Felician (TRA), Meshack Gideon (Dereva wa Ndani), Chacha Lukwi (Mshauri wa Madereva), Agness Mathias (KK Security), John Masasi (TICTS), William Kapera (TPA Usalama), Martin Paul (Evergreen Shipping Agent), Jones Jonathan (Wakala Usafirishaji) na Aloyce Gabriel (Wakala Uingizaji).
“Tarehe 03 mwezi Februari nataka ripoti ofisini kwangu ikiwa na uchunguzi mlioufanya ili kuiboresha bandari hii kwa kuwa nataka tuwe bandari ya mfano katika dunia hii” alisema Dk Mwakyembe.

CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

WATU NANE WAUAWAWA KATIKA VURUGU ZA MTWARA NA MOROGORO,NYUMBA ZA VIONGOZI ZACHOMWA MOTO

Wakazi wa mji mdogo wa Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro  wakiwakimbia askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)  katika barabara ya Dodoma-Morogoro juzi.

HABARI KAMILI
WATU wanane wameuawa na wengine kumi na moja kujeruhiwa kutokana na vurugu zilizizotokea jana mkoani Mtwara na Itete wilayani Ulanga, mkoani Mororgoro.
Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, Amima Simbo alithibitisha vifo vya watu saba waliofikishwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa muuguzi huyo, maiti zilizopokelewa hospitalini hapo zilionekana zikiwa na matundu yanayodhaniwa kuwa ni ya risasi, baadhi yao kichwani, begani, viunoni na tumboni.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Habari zaidi zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya kundi la waandamaji, wengi wakiwa vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda waliokuwa wakipinga mwenzao kukamatwa na kutaka kuvamia Kituo cha Polisi ili kumwokoa.
Vurugu hizo ziliendelea kuutikisa Mkoa wa Mtwara kwa siku ya pili mfululizo na kuutikisa Mkoa wa Mtwara, baada ya vurugu nyingine kuibuka wilayani Masasi jana.
Habari zinasema mbali na vifo na majeruhi, nyumba za wabunge wawili wa wilaya hiyo zimechomwa moto, ambapo pia magari, trekta, Ofisi za CCM Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ziliharibiwa kwa kuchomwa moto.
Wabunge ambao nyumba zao zimemwa moto ni Mariam Kasembe wa Masasi Mjini na Anna Abdallah Mbunge wa Viti Maalumu wilayani humo.
Juzi vurugu hizo zilitokea katika Mikoa ya Morogoro kati ya wakulima na wafugaji na kusababisha kifo cha mtu mmoja wakati mkoani Mtwara wananchi  wa eneo la Chikongola waliizingira nyumba ya diwani wa Kata ya Mikindani, Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake.
Katika vurugu hizo polisi walilazimika kutumia silaha yakiwamo mabomu ya machozi ili kupoza hali ya hewa, ambapo nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia ilichomwa moto.
Akizungumza na Mtandao huu kuhusu vurugu hizo, Mbunge wa Masasi Mjini, Mariam Kasembe alisema kuwa nyumba yake iliyoko Masasi mjini imechomwa moto na kuteketea kabisa, huku mali zikiibwa na kwamba familia yake sasa haina makazi.
Aliongeza kwamba mbali na uharibifu, vurugu hizo zimesababisha pia mama yake mzazi kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.
“Wamechoma trekta na gari lililokuwepo nyumbani kwangu, watoto wangu na mume wangu walipoona hali hiyo wakakimbia,” alisema Kasembe akieleza kuwa hawezi kuthibitisha chanzo cha vurugu hizo, lakini anahisi kuwa zinatokana na mgogoro wa gesi.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

Friday, January 25, 2013

SITA AJIPIGIA CHAPUO YA URAIS


.Asema anafaa  kuwa Rais

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta 
,”
HABARI KAMILI


WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema kwamba anazo sifa za kuwa Rais wa Tanzania na anafikiria kugombea 2015, iwapo dhamira yake itaridhika na mazingira na upepo wa kisiasa wa wakati huo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mtandao huu Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri.
Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge.
Hata hivyo, alisema hana mkakati wowote sasa wa kuendesha harakati za kutafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kama baadhi ya wengine (bila kuwataja), wanavyofanya... “Sina sababu za kuanza kutafuta support (kuungwa mkono) wala uundaji wa kamati za ushawishi kwa watu sasa,” alisema Sitta.
Badala yake alisema atasubiri hadi muda wa kuchukua fomu za kugombea utakapofika ndipo atakapojitathmini na kusema endapo atabaini kuwa Watanzania wengi wanamuunga mkono, atachukua uamuzi wa kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Aitahadharisha CCM
Waziri huyo aliwahadharisha wanachama wa CCM kwamba wasipokuwa makini, wanaweza kuipoteza nafasi hiyo ya urais na kwenda kwa vyama vya upinzani.
Alionya kuwa iwapo watamteua mtu asiye mwadilifu, Watanzania hawatamchagua na badala yake watampa nafasi hiyo mgombea yeyote kutoka vyama vya upinzani.
Alisema Watanzania wengi wana werevu wa kutosha kujua watu ambao ni mafisadi na ambao wamekuwa wakitumia fedha zao chafu kwa ajili ya kutaka wakubalike mbele ya macho ya Watanzania. Alisema suala la uadilifu ni moja ya vigezo muhimu ambayo CCM wanapaswa kuvizingatia ili kupata ushindi wa kiti cha urais mwaka 2015.
“Ndiyo maana nilipokuwa mbele ya Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba niliweka wazi kwamba Tanzania tunahitaji kuwa na jopo la kuhoji viongozi na wananchi wawe na fursa ya kuwachambua,” alisema Sitta.
Alisema kinachohitajika Tanzania ni mfumo ambao utajenga mazingira ya kuwa na viongozi waadilifu katika ngazi zote.
Alisema hali hiyo itaepusha mfumo unaoonekana sasa wa viongozi kwenye ngazi mbalimbali kuishi kiujanjaujanja, kujinufaisha na kutojali athari kwa uchumi wa nchi na Watanzania kwa ujumla.
Alitoa mfano wa uzembe uliofanywa na viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambao umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kupoteza uaminifu kwa nchi mbalimbali zinazopakana na Tanzania.
Alisema uzembe huo umeifanya Bandari ya Dar es Salaam kuingiza Sh38 bilioni kwa mwezi tofauti na Mombasa ambayo inaingiza Sh300 bilioni.
CCM ni imara?
Akizungumzia miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM, mbunge huyo wa Urambo Mashariki alisema anaamini kwamba chama hicho kimefanya vizuri licha ya kuchafuliwa na watu wachache kutokana na tabia zao za ufisadi.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

Thursday, January 24, 2013

KIGAMBONI YAWA MJI UNAOJITEGEMEA

.yanyofolewa Temeke

(Picha na www.ippmedia.com)
 HABARI KAMILI
 
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi, Prof Anna Tibaijuka akiuzungumza na waandishi wa habari juu ya serikali kuunda Wakala wa Uendelezaji wa mji wa Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. 
 
Wengine ni Mkurugenzi wa Upimaji Ramani, Sellasie Mayunga (kushoto), Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji Albina Bura na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uendelezaji wa mji wa Kigamboni, Vicent Shahidi.
Serikali imetangaza kuuondoa Mji wa Kigamboni kuwa chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na kuanzisha mamlaka ya upangaji wa mji huo ijulikanayo, kama Wakala wa Kusimamia Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni (KDA).

KDA ambayo ilianzishwa na serikali kisheria Januari 18, mwaka huu, itasimamia uendelezaji wa mji huo unaotarajiwa kuwa wa kisasa.
      
Mji huo pia unatarajiwa kuwa kitovu cha kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jiji la Dar es Salaam ili liweze kushindana na miji mingine duniani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii na kukuza ajira, hasa kwa vijana.                                                                                                         Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, aliwaambia waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, kuwa KDA itaongozwa na mkurugenzi mtendaji. Alisema mkurugenzi huyo atateuliwa pamoja na wakurugenzi sita watakaokuwa na wakuu wa idara.

Hata hivyo, alisema kwa sasa KDA inaongozwa na kaimu mkurugenzi mtendaji. Mbali na hilo, alisema KDA pia itasimamiwa na Bodi ya Ushauri pamoja na Baraza la Ushauri.

Alisema Baraza hilo litakuwa na wajumbe wanaowawakilisha wadau wote, hususan wabunge na madiwani wa eneo litakaloendelezwa na KDA.

Waziri Tibaijuka alisema KDA itakuwa na kazi ya kutafuta fedha za kutosha kwa ajili ya mradi, kupanga mji na kusimamia ujenzi wa mji kwa viwango vya kimataifa. Hata hivyo, alisema wananchi watashirikishwa kushauri.

Alisema fidia kwa wananchi ambao makazi yao yatatwaliwa kwa ajili ya kupisha uendelezaji wa mji itatolewa, lakini hawatahamishwa, badala yake watapewa makazi mapya katika mji huo mpya wa Kigamboni.

Hata hivyo, alisema ambaye atalipwa fidia hataruhusiwa kwenda kuishi katika makazi yaliyo nje ya mji mpya wa Kigamboni.

Alifafanua kuwa, atakayeruhusiwa ni yule atakayeonyesha hatimiliki ya kiwanja anachokwenda kujenga nje ya mji huo kwa ajili ya kuishi huko.

Waziri Tibaijuka alisema eneo litakalosimamiwa na KDA lina ukubwa wa hekta 50,934.
Alisema katika uendelezaji huo, kata zote za Kigamboni zimeunganishwa na kwamba, mji huo utaendelezwa na kuwa wa kisasa.

Waziri Tibaijuka alisema yeye ni miongoni mwa wataalamu duniani walioshiriki katika ujenzi wa mji wa Dubai.

Hivyo, akasema hataki kuona tena Watanzania wakifika Dubai waanze kuushangaa mji huo.
Alisema eneo la mji wa Kigamboni linahusisha Kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila, Kisarawe II, Kimbiji na Pemba Mnazi.

Waziri Tibaijuka alisema katika kusimamia uendelezaji huo, KDA itaongozwa na mpango kabambe.

Alisema mpango huo ni pamoja na kuwa na mji uliopangwa kwa kiwango cha kimataifa utakaokuwa mfano wa kuigwa na miji mingine nchini.

Pia kupunguza ujenzi holela, kuongeza mapato ya serikali yanayotokana na shughuli za kiuchumi na kijamii, kama vile viwanda, hoteli, utalii, biashara, elimu, ofisi, afya na vituo vya michezo.

Vilevile, kupunguza msongamano wa magari na huduma za kiuchumi na kijamii katikati ya jiji la Dar es Salaam, kuongezeka kwa thamani ya ardhi katika maeneo ya mji kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara, maji na umeme itakayowezesha kukuza biashara, ujenzi wa majengo na viwanda.

Pia kuhamasisha uwekezaji ili kuongeza ajira, hasa kwa vijana na wananchi wengi wataweza kumiliki nyumba katika maeneo yaliyopangwa na kutumia nyumba zao kupata mikopo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali.

Alisema mji mpya wa Kigamboni utakuwa na watu takriban 400,000 kulinganisha na watu 80,000 waliopo sasa.

Waziri Tibaijuka alisema katika kutekeleza mpango huo, uwakilishi wa wananchi utakuwapo kama ambavyo umekuwapo katika mchakato wa ufanikishaji wake.

Hii ni hatua mpya na kubwa inachukuliwa na serikali katika kukabiliana na mradi wa Kigamboni ambao wananchi kadhaa wakiongozwa na Mbunge wao, Dk. Faustine Ndugulile, wanadai kuwa wananchi hawajashirikishwa katika mradi huo.

Tayari wananchi hao wameunda kamati ya kusimamia madai yao wakihofia kwamba huenda unalenga kuwapora maeneo yao na kuwapa wawekezaji wakubwa.

MBUNGE AZUNGUMZA
Ndugulie akizungumza na NIPASHE jana jioni, alisema anasikitishwa na hatua zinazozidi kuchukuliwa na serikali kwa eneo la Kigamboni bila kuwashirikisha wananchi.

“Kweli tunaanza mwaka mpya vibaya. Yaani hawa wameshindwa kuwashirikisha wananchi kwenye zile kata za awali nne sasa wameongeza zingine na eneo kubwa zaidi bila hata kuzungumza nao… huu  ni uvunjaji wa sheria, kwa nini lakini?” alihoji.

Mbunge huyo alisema ingawa dhana ya mradi huo ni nzuri, lakini kutokuwashirikisha wananchi ni uvunjaji wa sheria.
“Serikali inaendelea na ubabe na kuvunja sheria sijui ni kwa nini,” alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

Tuesday, January 22, 2013

MKAPA KUTAKA SULUHU SUALA LA GESI KWAPOKEWA KWA HISIA TOFAUTI

Mkapa akoleza mjadala wa gesi

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa 


HABARI KAMILI
WITO wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kutaka suluhu ya mgogoro wa gesi unaoendelea baina ya Serikali na wakazi wa mikoa ya kusini, umepokewa kwa hisia tofauti. Baadhi ya wasomi wamempongeza huku wakazi kadhaa wa Mtwara wakimpinga.

Juzi, baada ya mgogoro huo kuendelea kwa takriban mwezi mmoja sasa, Mkapa alizitaka pande hizo mbili kutafuta mwafaka akieleza kuwa linalowezekana leo, lisingoje kesho.

“Mtafaruku huu haufai kuachwa na kutishia usalama, mipango ya maendeleo siyo siri, mikakati na mbinu za utekelezaji wake siyo siri. Maelezo yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo rasilimali zinawanufaisha wananchi wa eneo zilimo na taifa zima,” alisema Mkapa katika taarifa yake.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema jana kuwa kauli ya Mkapa ni nzuri, huku akisisitiza kuwa katika suala hilo, lazima utaifa uwekwe mbele.
“Hata wakati wa ujenzi wa Barabara ya Mtwara, wapo waliosema kuwa mikoa ya kusini inatengwa, kauli hizi zilikuwapo tangu zamani, kikubwa ni suala hili kuchukuliwa kitaifa zaidi,” alisema Dk Bana.

Wazee watafuta suluhu Dar
Wazee wa Mtwara Mikindani wako Dar es Salaam kusaka suluhu ya mgogoro huo, baada ya kusema kwamba wamebaini kuwa kutakuwa na uvunjifu wa amani kama suala hilo litaachwa liendelee.

Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wazee hao walisema suala hilo linaleta hofu kubwa kwa taifa hivyo linapaswa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Katibu wa wazee hao, Selemani Mademu alisema wananchi wa Mtwara wako tayari kufa kuliko kuona wakidharauliwa katika suala hilo.

Mademu alisema: “Wananchi wa Mtwara wanaamini kuwa kituo cha kuchakata gesi asilia kama kitajengwa Mtwara kitatoa fursa kubwa ya kushawishi wawekezaji ambao watajenga viwanda vitakavyotumia malighafi ya gesi asilia na hivyo kuchochea maendeleo ya Mtwara kwa jumla,” alisema na kuongeza kuwa kama Serikali inaamini kwamba wazo lake la kuisafirisha hadi Dar es Salaam ni jema na lenye manufaa kwa wananchi wa Mtwara, ingejikita katika kutoa elimu badala ya kukaa kimya na kuendelea na kile inachoamini.

“Wanamtwara hatupendi kuendelea kuelezwa kwamba tutanufaika na gesi iliyogunduliwa kwa kuahidiwa viwanda kama ambavyo imekuwa desturi ya Serikali yetu. Tunahitaji vitendo vitawale badala ya ahadi ambazo hazitekelezeki. Kwa mfano barabara, umeme, kuimarishwa kwa bandari, mikopo kwa ajili ya ujasiriamali, viwanda vidogo vya kubangua korosho n.k.” alisema.

Wengine wapinga
Mwenyekiti wa Umoja wa Maendeleo Mikoa ya Kusini (UMMK), Said Mannoro (72) alimshutumu Mkapa akidai kuwa ndiye chanzo cha gesi ya Songosongo kupelekwa Dar es Salaam.

Mzee Mannoro ambaye alifika katika ofisi za gazeti hili, Tabata Relini, Dar es Salaam jana alisema Mkapa anatakiwa kueleza faida walizopata wananchi wa Lindi baada ya gesi ya Songosongo inayozalishwa mkoani humo, kupelekwa Dar es Salaam.

Mbali na mzee huyo, baadhi ya viongozi wa dini na vyama vya siasa nao wamempinga Mkapa wakisema kuwa ushauri wake umeegemea upande mmoja na kwamba alipaswa kumshauri Rais Jakaya Kikwete.

Askofu Mteule wa Kanisa la KKKT Dayosisi Mpya ya Kusini Mashariki, Mchungaji Lucas Mbedule alisema Mkapa, amechelewa kutoa ushauri wake na kwamba kwa hali ya sasa alipaswa kumshauri Rais Kikwete akubaliane na matakwa ya wananchi.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

Friday, January 18, 2013

MAKALA YA MGANGA WA JADI BINTI NDEMBO NA UCHAWI


Mganga wa Jadi wa Namtumbo Songea Frola Ndembo Maarufu kwa jina la Binti Ndembo.

Ndugu Wasomaji wa Mtandao huu tunawaletea  Makala ya Binti Ndembo na Uchawi na Mchambuzi   wako wa masuala ya Uchawi Mwanahabari Adam Nindi.

Fuatana naye

Kwa habari za kina nilikuwa nikiifahamisha Jamii kwa kitu kinachoitwa uchawi ambacho ndicho changamoto kwa watu wanaoishi pembezoni.
Watu walio wengi huingiwa na hofu kufanya Maendeleo kwa kile kinachoitwa woga wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

                 Mganga wa jadi bint Frola Ndembo
Nikiwa katika kambi ya Mganga mashuhuri wa Nyanda za juu Kusini Mama Binti Flora Ndembo nimeweza kupata siri kubwa kuhusu uchawi. Wachawi wenyewe wamesema wamejiingiza katika uchawi baada ya kuona Jamii ikiwatenga, wale ambao ambao hawana uchumi wa kutosha ndio wanaunda umoja wa kuwatesa wenzao.

Mchawi mkuu wa wachawi wote ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalinina hatimaye kuchaguliwa kuwa katibu wawachawi mkoa wa Ruvuma  amesema yeye alijiunga na uchawi kwa ajili ya kutaka kujikinga na watu wabaya  lakini mara baada ya kustaafu alipendekezwa kuwa Katibu Mkuu wa wachawi Mkoa wa Ruvuma.
Lakini yeye mwenyewe amesema ameamua kujitoa baada ya wachawi wenzie kumuua mototo wake ambaye alifikia ngazi ya kuwa Askofu; hapo ndipo alipoona kuwa uchawi hauna maana.
Nikiwa mchambuzi wa habari za ushirikina  niliamua kumuuliza mzee kuwa mootto wake ambaye alikuwa mtu wa Mungu aliwezaje kuuwawa wakati yeye ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wachawi. Alijibu hakuna mtu anayeweza kuuwa katika ukoo kama ndugu hajaidhinisha na sheria hiyo hufuatwa kwa makini ukikiuka taratibu unauwawa mwenyewe “ndivyo ilivyonikuta kwa mototo wangu

Nikiwa katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake kuweka rehani mwili wake baada
Nikiwa katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo nilikutana na Mwenyekiti wa wachawi katika maeneo ya Mwambao wa ziwa nyasa. Yeye anasema alijitenga na Jamii na alikuwa akiishi mashambani ambako ndiko kulikuwa Makao Makuu ya Mikutano ya wachawi wote.
Yeye anasema alijiunga na uchawi baada ya kaka yake kuweka rehani mwili wake baada
wa kuuwawa au kulogwa. Kwani sumu ya kitu uchawi ni kuona maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Nikiwa bado katika Kambi hiyo ya Binti Ndembo, nilitiwa na fadhaha baada ya kumuona Binti mwenye umri wa miaka 10 aliyepewa uchawi na Mama yake na kuweza kupewa mboga ya akiba ambacho ni kidonda kilicho ubavuni ambacho yeye alikiri kuwa akikosa mboga hutumia kwa kuchovya kwenye kidondaMaskini Binti huyo katika maisha yake hadi kufikia miaka hiyo 10 alikuwa akichukia shule kama nini lakini baada ya kufika kwa Binti Ndembo ameacha uchawi na kuomba akaendelee na Masomo

Kamanda wa Polisi aliye hamia Iringa Michael Kamuhanda kushotona Kamanda Mpya Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kaizilege Nsimeki
 Ndugu yangu nikiwa katika kambi hiyo na Binti Ndembo nimeona mambo mengi cha kufurahisha mganga huyo hana uchochezi. Yeye amekuwa akipatanisha ndugu hao na kuwa Jamii moja. Nikiwa Kambini hapo nimeshuhudia Viongozi wa ngazi za juu akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma akitoa elimu Shirikishi kwa kutaka Jamii iachane na Mambo ya Ushirikina.
Mganga huyo mashuhuri mbali ya kutibu watu wenye asili ya Ushirikina lakini hata hivyo ameshaweza kukamata Majambazi Sugu, na wao kusalimisha silaha zao na kuachana na Ujambazi.
Jambo la kuingilia Masuala ya Ujambazi, Mganga huyo mashuhuri amepata misukosuko kwa kuwahi kupigwa risasi mbili na kukimbizwa Hospitali ambako alitolewa.
Amewahi kufungwa Kamba na kutupwa msituni na kuambiwa aachane na masuala ya kufuata Majambazi lakini uganga wake uliweza kumwokoa.
Pia kwa Mara ya Kwanza Mganga huyo aliweza kubainisha ndoa iliyofungwa kati ya Mama na Mtoto wake wa kuzaa mwenyewe. Hatimaye aliweza kuibainisha Ndoa hiyo hadharani.
   Ndugu zangu wasomaji, Shabaha yangu ni kutaka kuendelea kupata mawazo kutoka kwenu, kitu kikubwa ambacho kinasababisha Maendeleo kuto chukua Kasi ni Kushiriki katika Mambo ya Ushirikina.   Sasa hapa tumeona watu walio wengi wakiacha Uchawi na kutangaza Hadharani.

HALI YA DCI MANUMBA BADO MBAYA,BADO YUKO ICU


Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Inspekta Jenerali wa Polisi katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumlaki Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)  Kamishna Robert Manumba aliyelazwa hospitalini hapo. 
e

 FULL STORY

HALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Robert Manumba bado ni mbaya na jana Rais Jakaya Kikwete alikwenda tena ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam alikolazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), kumjulia hali.

Mbali na Rais Kikwete, viongozi wengine waliofika hospitalini hapo kumjulia hali DCI Manumba ni Mke wa Rais, Salma, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Said Mwema na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni. Pia walikuwapo ndugu, jamaa na marafiki ambao walikusanyika hospitalini hapo takriban siku nzima jana wakifuatilia afya yake.

Rais Kikwete alifika hospitalini hapo jana saa 11:15 na alitumia takriban dakika 10 tu kwani alitoka saa 11:26 huku akionekana mnyonge na alielekea kwenye gari lake na kuagana na IGP Mwema na Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee kisha kuondoka.

Juzi, Rais Kikwete alikwenda hospitalini hapo mara baada ya kumsindikiza Uwanja wa Ndege mgeni wake Rais wa Benin,Thomas Boni Yayi aliyekuwa nchini kwa ziara ya siku moja.
Jana, Mke wa Rais alikuwa wa kwanza kufika hopitalini hapo saa 10:20 na aliondoka saa 10:45 muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufika.

Habari zilizopatikana jana zilieleza kwamba kutokana na afya yake kuwa mbaya, wageni wengi wakiwamo viongozi waandamizi, walizuiwa kuingia kumwona.
Uongozi wa Aga Khan watoa tamko
Jana mchana, uongozi Aga Khan ulitoa taarifa rasmi kuzungumzia afya ya kiongozi huyo wa Polisi huku ukieleza kuwa kimsingi siyo nzuri na bado anahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari.

“Uongozi wa Hospitali ya Aga Khan ungependa kuujulisha umma kwamba Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Robert Manumba bado yupo hospitalini Aga Khan ambako anaendelea kupatiwa matibabu. Hali yake bado inahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Juzi, Dk Dharsee alisema Manumba alifikishwa katika hospitali hiyo akisumbuliwa na malaria huku hali yake ikiwa mbaya na hajitambui.

Msemaji wa familia atoa mafumbo
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo jana, msemaji wa familia ya DCI Manumba, James Kilaba alisema: “Maisha ndivyo yalivyo, huwezi kuzua ugonjwa na huwezi kubadili uhalisia wa mambo. Sisi kama familia, tunaamini Mungu yuko na ndugu yetu na ndiye atatenda yake na naomba Watanzania wamuombee.”

Hata hivyo, alikataa kuzungumzia ugonjwa wake zaidi ya kusema kuwa alipelekwa Jumanne iliyopita hospitalini hapo kwa ajili ya vipimo zaidi.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

WAJAWAZITO WADAI KUNYANYASWA MALAWI KUTOKANA NA MGOGORO WA ZIWA NYASA

Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Malawi Joyce Banda, wakitabasamu huku wakipeana mikono mara baada ya mazungumzo mjini Maputo
WAKATI mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyassa unaoendelea kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali na Malawi haujapatiwa ufumbuzi, mamia ya Wajawazito kutoka Tanzania kuelekea nchini Malawi kupata huduma ya Afya wamedai kunyanyaswa na baadhi ya watoa huduma katika Hospitali nchii humo.
Wakizungumza na Mtandao huu kwa nyakati tofauti huku wakiomba majina yao kutotajwa mtandaoni kwa madai kwamba bado wanategemea kupata huduma hiyo nchini humo, wamesema kwamba tangu mzozo huo ulipoanza wamekuwa wakipata huduma hiyo kwa shida tofauti ya siku za nyuma,
"Tangu mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyassa tumekuwa na wakati mgumu wa kupata huduma ya afya  kwa sababu baadhi wataalaam wa afya nchini humo hawataki kutuhudumia kwa wakati kwa madai kwamba hivi sasa nchi zetu hazina mahusiano mazuri kutokana na mzozo huo"aliema mama mjamzito ambaye ni mkazi ya kijiji cha Ikumbilo.
Ramani ya TanzaniaAkizungumzia sababu za wao kwenda kutafuta huduma ya afya nchini humo alidai kwamba ni kukiukwa kwa sera ya Afya ya mwaka 2007 inayosema kwamba wajawazito nchini Tanzania watapewa huduma za afya bure.
"Sera hiyo imekiukwa katika Hospitali za Wilayani Ileje Mkoani Mbeya,ndiyo maana baadhi ya wajawazito wilayani Ileje wanaacha Zahanati, vituo vya Afya na Hospitali Wilayani humo na kuvuka mpaka hadi nchi jirani ya Malawi kufuata huduma bora, tumekuwa tukivuka mpaka huu kwa miaka mingi,mfano mimi mwenyewe ninawatoto watano hivi sasa na wote nimewaza nchini Malawi"alifafanua mjazito mwingine.
Wajawazito hao wanatoka kata za Bupigu, Itumba na Isongole na wnakwenda nchini Malawi kwa wingi ili waweze kujifungulia huko na kupata huduma nyingine za afya.
Kutoka Isongole hadi Hospitali maarufu ya Chitipa nchini Malawi ni umbali wa kilometa 45, wakati umbali wa kwenda Hospitali ya Serikali ya Ileje ni kilomita tatu tu. Mwanamke moja mkazi wa kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete wilayani Ileje, aliyejitambulisha kuwa anaishi na virusi vya ukimwi (VVU) anasema aliwahi kujifungulia Hospitali ya Chitipa na mpaka sasa anapata matibabu yake huko. Wilaya ya Ileje ina Hospitali kubwa mbili – Hospitali ya Serikali mjini Ileje na ile ya Misheni ya Isoko.ambapo ndizo Hospitali ambazo zinategemewa kwa huduma ya uzazi.
CHANZO-HABARI MPYA.COM

Tuesday, January 15, 2013

VIJANA MSISUKUMWE KATIKA MAKUNDI YA KUVURUGA AMANI-KIGWENEMBE

 Mjumbe wa Baraza kuu la V ijana wa CCM  Taifa  akizungumza kwa hisia kali katika moja ya mikutano yake.
 Alfan Kigwenembe akizungumza na Vijana katika moja ya Mkikutano yake.
 
VIJANA MSISUKUMWE KATIKA MAKUNDI YA KUVURUGA AMANI-KIGWENEMBE
Na Joseph Mwambije,
Songea
VIJANA  wametakiwa kutosukumwa katika makundi ya kuvuruga amani,kutumika kisiasa na kuandamana bila sababu za msingi na matokeo yake wao ndio wanaoathirika katika vurugu za kisiasa na maandamano na kuziacha familia zao zikiahangaika.
Wito huo ulitolewa juzi na mjumbe wa Baraza kuu la vijana wa CCM(UVCCM)Alfan Kigwenembe  wakati akizungumza na vijana kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Msamala mjini Songea mambo mbalimbali yanayowahusu Vijana.
Mwanasiasa huyo kijana alikuwa akizungumza na Vijana wote wa Manispaa ya Songea bila kujali itikadi zao za kisiasa kwa kuwa wao ndio rasilimali  ya Taifa na wamekuwa wakitumika vibaya na Wanasiasa kwa maslahi yao.
Alibainisha kuwa katika maandamano zinapotokea fujo vijana wanaathirika kwa kupata ulemavu wa maisha na wakati mwingine kupoteza maisha na kuziacha familia zao zikihangaika huku Viongozi wa  Siasa waliowasukuma kuandamana wakishindwa kuwasaidia na kusaidia familia zao baada ya wao kupoteza maisha.
‘Vijana lazima mtambue kuwa nyinyi ni rasilimali ya Taifa hivyo hampawi kushiriki katika fujo na kuvuruga amani ya Nchi yetu na kuandamana katika maandamano yasiyokuwa ya msingi na badala yake mjiunge katika Vikundi vya ujasiriamali ili mjiletee maendeleo’alisema Mwanasiasa huyo.
Aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujileteaaendeleo kwa kuwa maisha bora hayaletwi kwa kucheza bao na Pool na badala yake yanaletwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuongeza kuwa miradi mbalimbali ya madini Mkoani Ruvuma ukiwemo wa Urenium utaongeza ajira kwa Vijana.


Alfan Kigwenembe

KUPINGA GESI KUSAFIRISHWA NI KUPINGANA NA BABA WA TAIFA-NCHIMBI


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Mkoa wa Ruvuma,Alex Nchimbi akizungumza wakati akifungua Baraza la UVCCM  Mkoa wa Ruvuma.Kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Ruvuma,Mwajuma Rashid.


KUPINGA GESI KUSAFIRISHWA NI KUPINGANA NA BABA WA TAIFA-NCHIMBI

Na Joseph Mwambije
Songea

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Ruvuma Bw. Alex Nchimbi  amesema kuwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Daressalaam ni kupingana na Baba  wa Taifa Hayati Julius Nyerere  aliyetaka kuwepo na mgawanyo sawa kwa rasilimali za Taifa kwa Mikoa yote Nchini.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua  Barazaza la Vijana wa Chama hicho lililofanyika hivi karibuni mjini Songea na kuwataka Vijana wa Chama hicho kuwa makini wanapozijibia hoja za Kitaifa si kukurupuka kama hiyo ya gesi.
Alisema kuwa Baba wa Taifa  aliweka mgawanyo sawa wa rasilimali za Taifa na kuondoa ubaguzi wa kidini na Kikabila huku akiitambulisha lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya Taifa.
‘Tukisema rasilimali zinufaishe Mkoa husika pekee je Mikoa isiyokuwa na kitu itafanyaje,kwa sisi Mkoa wa Ruvuma mahindi yetu yamekuwa yakilisha Tanzania yote na Nchi nyingine za jirani’alisema.
Aliwataka Vijana hao kushirikiana na Jamii klatika masula ya kijamii pamoja nma elimu katika Shule za Sekondari na Shule za Msingi ambako alidai kuwa huko Umoja huo umekuwa ukipwaya wakati Vyama vya upinzani vimejikita kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti ambaye alikuwepo kwenye Baraza hilo  aliwataka Vijana kushirikiana katika kuijenga Jumuiya yao ya UVCCM na Chama chao kwa ujumla huku wakiwaunga mkono wanaokijenga Chama hicho badala ya kuwapinga.
Alimpongeza mjumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Taifa Bw. Alfan Kigwenembe kwa kazi nzuri ya kufanya mikutano na kuongea na vijana mbalimbali wa Chama hicho na ambao si wa Chama hicho huku akiyazungumzia masuala mbalimbali ya msingi na kuyatolea ufafanuzi.

SITAVUMILIA VURUGU ZA KIDINI,KIKANDA NA KIKABILA-JK


Rais Jakaya Kikwete 

Daressalaam

SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.
Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.

“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.

“Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu,” alisema Balozi Mpango.

Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.

Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.

Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.

Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.

“Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala.”
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

RC RUVUMA AWAASA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA KIKOSI CHA ZIMAMOTO KWENYE MAJANGA YA MOTO

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizungumza kwenye uzinduzi huo.
  
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma Baraza Mvano akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi  RC  Mwambungu.

RC RUVUMA AWAASA  WANANCHI KUSHIRIKIANA NA ZIMAMOTO KWENYE MAJANGA YA MOTO
Na Joseph Mwambije
Songea
MKUU wa Mko wa Ruvuma  Bw. Said Mwambungu amewataka Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kushirikiana na Jeshi  la Zimamoto katika uzimaji wa moto yanapotokea majanga ya moto badala ya kuwatupia mawe na kuwafanyia fujo Askari wa Kikosi cha zimamoto.

Alitoa wito huo jana wakati akizindua Zoezi la kuzima moto lililofanywa na Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Ruvuma na kufanyika  kwenye Viwanja vya Bustani za Manispaa ya Songea na kubainisha kuwa katika majanga ya moto mtu wa kwanza katika kuzima moto ni mwananchi mwenyewe.

‘Muwe  mnatoa taarifa mapema kwa Kikosi cha Zimamoto  badala ya kuchelewa kutoa taarifa na Askari wa Zimamoto wana pochelewa  mnawalaumu na kuwafanyia fujo wakati nyie wenyewe mmechelewa kutoa taarifa’alisema na kuongeza

Tatizo lenu mmekuwa mkijaribu kuzima kwanza wenyewe moto  pindi yatokeapo majanga ya moto mkishindwa ndio mnawaita Askari wa Zimamoto wakati moto umeshaunguza kila kitu hivyo ni vema mkabadilika na kutoa ushirikiano kwa  Kikosi cha Zimamoto.

Mwambungu aliongoza zoezi  la kuzima moto katika Operesheni maalumu ya kuzima moto iliyoandaliwa na Kikosi cha Zimamoto huku  Mtandao huu Cresensia Kapinga akiongoza kuzima moto kwa niaba ya Wanahabari wa Mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Bw. Baraza Mvano alisema kuwa majukumu ya Jeshi la Zimamoto ni kuzima moto  wenye madjhara pale unapotokea,kuokoa maisha ya watu  na mali zake,kufanya ukaguzi wa Kinga na tahadhari ya moto na kutoa mafunzo ya kinga na tahadhari.

Baadhi ya Wananchi wakiongozwa na Amoni Mtega na Samweli Mapunda wamesema kuwa mafunzo na elimu iliyotolewa na Jeshi la Zimamoto katika Zoezi hilo imewasadia kuelewa Jeshi hilo linavyofanya kazi na hivyo watatoa ushirikiano kwa Kikosi hicho pindi majanga ya moto yanapojitokeza.
 
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizima moto
 Mashauri wa Mgambo mkoa wa Ruvuma Kanali Fula akizima moto
 Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mkoa wa Ruvuma Bi. Cresensia Kapinga akizima Moto
 Askari wazima moto wakizima moto