Tuesday, November 27, 2012

WASHUKIWA WA ICC KENYA KUUNDA MUUNGANO


Uhuru Kenyatta ni mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007
Washukiwa wawili wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, Uhuru Kenyatta na William Ruto wanajadiliana kwa lengo la kuunda muungano wa kisiasa watakaotumia kugombea uongozi wa nchi.
Taarifa za awali zilisema kuwa wawili hao tayari wameunda muungano huo ingawa baadaye afisa wa mawasiliano wa vigogo hao alikana kuwepo makubaliano yoyote.
Wawili hao ambao ni mahasimu wa jadi kisiasa,wanaanda mkutano wa pamoja siku ya Jumamosi mjini Nakuru mojawapo ya maeneo yaliyokumbwa na ghasia mbaya zaidi za kikabila baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007.
Na hataua ya wawili hawa inakuja wakati mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ikiwa wanaweza kugombea uongozi wakati wanakbiliwa na tuhuma za kuhusikana ghasia za baada ya uchaguzi ambapo mamia ya watu waliuawa.
Wanasema wameamua kuunda muungano watakaoutumia kuwania nafasi ya rais na makamu wake katika uchaguzi mkuu mwaka ujao kama ishara ya kuwapatanisha wakenya.
Wanatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya ICC baada ya uchaguzi mwaka ujao kujibu mashtaka ya kuhusika na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mwaka 2007-2008
Kenyatta ambaye ni naibu waziri mkuu na Ruto ambaye ni mbunge , wanasema kuwa muungano wao utakuwa wenye kauli mbiu ya kupigia debe umoja wa kitaifa, ustawi na kupatanisha wakenya .
Katika uchaguzi uliopita, wawili hao walikuwa pande pinzani. Na ulikuwa uchaguzi ulioshuhudia upinzani mkali zaidi katika historia ya Kenya.
Ulifuatiwa na ghasia za kikabila ambapo mamia ya watu waliuawa na maelfu wengine kuachwa bila makao mwaka 2007.
Wawili hao wamekanusha madai ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi hasa kupanga makundi ya watu walioshambulia makundi hasimu.
CHANZO-BBC

Sunday, November 25, 2012

KABILA ATAKA M23 WAONDOKE GOMA


Serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo inasema haitazungumza na wapiganaji wa M23 hadi waondoke mji wa Goma ambao waliuteka juma lilopita.
Wanajeshi wa serikali kabla ya mji wa Goma kutekwa
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu mjini Kampala, Uganda, kuwasihi wapiganaji waondoke Goma.
Msemaji wa wapiganaji, Kasisi Jean-Marie Runiga, alisema wapiganaji wataondoka Goma baada ya mazungumzo ya amani lakini siyo kabla.
Rais Joseph Kabila wa Congo alikutana na wawakilishi wa wapiganaji mjini Kampala Jumamosi.
Wakuu wa Uganda wanasema yamekuwapo mawasiliano baina ya pande hizo mbili.
CHANZO-BBC

RAIS PAUL KAGAME AUNGA MKONO MPANGO WA KUMALIZA MAPIGANO CONGO

 Rais Paul Kagame wa Rwanda ametangaza kuwa anaunga mkono mpango uliopendekezwa na viongozi wa Maziwa Makuu, ili kumaliza mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Rais Paul Kagame
Rais Kagame aliisihi serikali ya Congo na wapiganaji wa M-23 kutekeleza mapendekezo hayo, ambayo piya yanataka wapiganaji hao waondoke katika mji wa Goma.
Rwanda inakanusha tuhuma za muda mrefu kwamba inawasaidia wapiganaji hao upande wa pili wa mpaka wa Rwanda.
Rais Kagame hakuhudhuria mkutano wa viongozi uliofanywa Kampala, Uganda, Jumamosi ambapo mpango huo ulikubaliwa.
CHANZO-BBC

Saturday, November 24, 2012

PAPA BENEDICT AWAWEKA WAKFU MAKADINALI WAPYA

Papa Benedict amewatawaza makadinali sita wepya, kwenye sherehe iliyofanywa Vatikani.
Papa Benedict katika sherehe iliyofanywa Rome
Mmoja baada ya mmoja, wanaume sita kutoka Libnan, India, Nigeria, Philippines, Colombia na Marekani - walipiga magoti kuvishwa kofia nyekundu na pete ya wadhifa wao.

Mwandishi wa BBC alioko Vatikani, anasema makadinali hao wameteuliwa baada ya malalamiko kutoka viongozi wa kanisa la Katoliki katika nchi zinazoendelea, kwamba makadinali walioteuliwa awali mwaka huu walikuwa wengi wazungu, hasa Wataliana wanaotumika Vatikani.
Kwa mara ya kwanza hakuna mzungu wala Mtaliana kati ya makadinali wepya.
Lakini wazungu ndio wengi ndani ya baraza kuu la makadinali 120 ambalo ndilo humchagua papa mpya.
Mtindo unaelekea kuwa na kanisa litalowakilisha wafuasi wake ulimwenguni.
Papa aliwakumbusha makadinali wepya kwamba kofia na makoti mekundu wanayovaa ni alama kuwa wamejitolea kumwaga damu kutetea imani yao ikihitajika.
Papa Benedict piya alisisitiza kuwa Kanisa Katoliki ni la binaadamu wote wa utamaduni na makabila yote.
Uamuzi wa Papa wa kuteua makadinali kutoka nchi tatu zenye Waislamu wengi, yaani Libnan, Nigeria na India, unaonesha ana wasiwasi juu ya uhusiano baina ya Ukristo na Uislamu.
Kadinali kutoka Libnan ni kasisi wa kati ya makanisa kongwe kabisa Mashariki ya Kati.
Askofu wa Abuja, kadinali mpya kutoka Nigeria ambako nusu ya wananchi ni Waislamu, anaweza pengine siku moja kuwa papa wa kwanza kutoka Afrika.
BBC

VIONGOZI WA AFRIKA WAWATAKA WAASI CONGO KUSITISHA MAPIGANO

Viongozi wa Afrika wamewasihi wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuacha mashambulio.
Rais Joseph Kabila alihudhuria mkutano wa Kampala
Mwisho wa mkutano wao mjini Kampala, Uganda, viongozi hao wamewataka wapiganaji wa kundi la M23 waondoke kutoka mji wa Goma waliouteka hivi karibuni.

Viongozi hao piya walimsihi Rais wa Congo, Joseph Kabila, kushughulikia malalamiko ya wapiganaji.
Viongozi wane walihudhuria mkutano huo - Rais Paul Kagame wa Rwanda hajakuwepo.
Walipendekeza kuweka kikosi cha pamoja katika uwanja wa ndege wa Goma kitachokuwa na wanajeshi kutoka Tanzania, jeshi la Congo na M23.
Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia wapiganaji wa M23 - shutuma inazokanusha.
Baada ya kuuteka mji wa Goma, wapiganaji wamesonga ndani zaidi kwenye ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na serikali.
Mashirika ya misaada yanaonya kuwa hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya.
CHANZO-BBC

Friday, November 23, 2012

MKUU WA MAJESHI DRC AFUTWA KAZI



Generali Amisi
Generali Amisi
Mkuu wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao mpia wameutekja mji wa Sake, lakini msemaji wa serikali Lambert Mende, amesema wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuumboa tena mji huo mdogo.
Waasi hao ambao wanaaminika kuungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa rais Joseph Kabila hatabuli kuanzisha mazungumzo ya amani.
CHANZO-BBC

Wednesday, November 21, 2012

ASKOFU WA KWANZA WA KIKE ATEULIWA

Ellinah Wamukoya
Ellinah Wamukoya
Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufalme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa kufuata siasaa za kihafidina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa la Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyo,bo vya habari, askofu huyo wa jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu mweusi, muafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Swaziland Manzin.
BBC

Tuesday, November 20, 2012

MVUA NJOMBE ZASABABISHA HASARA YA SHILINGI MILIONI 241


MVUA NJOMBE ZASABABISHA HASARA YA SHILINGI MILIONI 241
Na Joseph Mwambije,
Njombe
HALMASHAURI ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe imefanya tathmini ya  mvua zilizonyesha hivi  karibuni na kuharibu nyumba 178 na kubainisha kuwa maafa hayo yamegharimu shilingi milioni 241.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe  Bw. George Mkindo anasema mvua hizo zilizonyesha hivi karibuni na kuambatana na upepo mkali zImesababisha Kaya zaidi ya 100 kukosa mahala pa kuishi na kuharibu mashamba na nafaka majumbani.

Anasema kuwa Uongozi wa Halmashauri hiyo umefanya tahmini na kubainisha hasara iliyotokana na mvua hizo kuwa ni shilingi milioni 241 huku akiomba Wasamaria wema kuwasaidia wananchi waliokumbwa na maafa hayo.

‘Mvua zile licha ya kuharibu mazao mashambani na nyumba lakini pia zimeharibu miti na mali mbalimbali na kuwasababishia wananchi kukosa mahali pa kuishi’anasema Mkurugenzi huyo.

Anasema kuwa mvua hizo zilileta madhara zaidi  katika vijiji vya Kibena ambako nyumba 91 ziliharibiwa na mvua,katika kijiji cha Nundu nyumba 35 na maeneo ya  Hospitali ya Kibena numba 15.

Anataja maeneo mengine kuwa ni katika kijiji cha Ngalanga ambako nyumba saba zimeharibiwa,kijiji cha  Hagafilo Nyumba mbili na katika kijiji cha  Peluhanda nyumba moja.

Amewashukuru wananchi waliotoa ushirikiano katika kuwasaidia wenzao waliokumbwa na maafa na kuwataka kuendelea na moyo huo wa kusaidiana na kubanisha kuwa mvua hizo hazikuleta madhara katika maeneo ya mjini.

WAASI WA M23 CONGO WAUTEKA MJI WA GOMA


Watu wakikimbia mapigano Goma
Watu wakikimbia mapigano Goma

Wapiganaji wa waasi wa M23, hatimaye wamefanikiwa kuingia mji mkuu wa eneo la Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Mwandishi wa BBC mjini Goma anasema wapiganaji hao wa waasi walikabiliana kwa risasi na wanajeshi wa serikali, ambao walitoroka baada ya kuzidiwa nguvu.
Jeshi la Umoja wa Matifa la Kutunza amani katika eneo hilo limekanusha madai kuwa wapiganaji hao wa waasi wanathibiti uwanja wa NDEGE.
Maelfu ya watu wametoroka makwao kufuatia mapigano hayo, ambayo yamezua wasi wasi wa kuzuka upya kwa mapigano nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu milioni tano.
Hii ni mara ya kwanza tangu kumalizika kwa mapigano mwaka wa 2003, ambapo wanajeshi wa waasi wamefanikiwa kuingia mji huo wa Goma.
Takriban watu nusu milioni wanakadiriwa wanaishi mjini humo.
Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya mara kwa mara kutoka kwa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa inawaunga mkono wapiganaji hao wa waasi wa M23.
Awali serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilipuuzilia mbali makataa iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
CHANZO-BBC

Monday, November 19, 2012

MAPIGANO YAZIDI KURINDIMA CONGO

Wanajeshi wa Congo mjini Goma
Wanajeshi wa Congo mjini Goma

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imepuuzilia mbaya makataa iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi wa M23 wamesemekana kuukaribia mji huo huku maelfu ya raia wakikimbia makwao.
Mapema hii leo, wapiganaji hao walitoa ilaani ya saa ishirini na manne kwa serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo, ya amani la sivyo wataendelea na vita hivyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Barabaraza mji wa Goma haikuwa na raia kama kawaida na magari ya kijeshi na yale ya umoja wa mataifa ndiyo yaliyokuwa yakizunguka mji huo.
Waasi hao wa M23 wamesema kuwa ikiwa serikali ya nchi hiyo haitakubali kuanzisha mazungumzo hayo, hawatakuwa na budi ila kuendelea na mapigano hayo, hadi watakapoiondoa utawala wa sasa.
Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema waasi hao wanajumuisha wanajeshi ambao wanaungwa mkono na serikali ya nchi jirani ya Rwanda, ili kuficha vitendo vya kigaidi vinavyoendeleza katika eneo hilo la Mashariki.
Lakini serikali ya Rwanda imepuuzilia mbali madai hayo, ikisema kuwa hayana msingi wowote.
BBC

FRED MTOI WA BBC AFARIKI DUNIA

BBC inasikitika kutangaza kifo cha mtangazaji wao Fred Mtoi ambaye alifariki Ijumaa usiku mjini London.
Fredd Mtoi
Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa mafunzo.
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
BBC

Friday, November 16, 2012

KAMANDA WA BOKO HARAM AUAWA NIGERIA

Kamanda wa Boko Haram auawa

Silaha zilizonaswa na Jeshi
Silaha zilizonaswa na Jeshi
Wanajeshi wa Nigeria wanaendeleza operesheni kali ya kuwasaka wapiganaji wa Boko Haram katika eneo la Maiduguri Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wanajeshi hao wanatumia magari ya kivita na wanapewa usaidizi zaidi na helicopta za kijeshi.
Jeshi la Nigeria limedai kuwa limemuua kamanda mmoja mwandamizi wa Boko Haram Ibn Saleh Ibrahim.
Raia wa eneo hilo wamesema kuwa idadi kubwa ya watu wameuawa kwenye operesheni hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema Ibn Saleh Ibrahim aliuawa wakati wa makabiliano makali ya riasi wakati alipokuwa na walinzi wake sita.
Maafisa wa ulinzi nchini Nigeria wanaamini kuwa Bwana Saleh, alihusika na mauaji ya Generali mstaafu Mohammed Shuwa mwezi uliopita.
Kundi hilo la Boko Haram, ambao limeua raia wengi tangu mwaka wa 2009, halijasema lolote kuhusiana na kifo cha kamanda huyo.

Historia ya Boko Haram

Mwanzilishi wa kundi hilo, Mohammed Yusuf, aliuawa na maafisa wa ulinzi mwaka wa 2009.
Kiongozi wa Boko Haram
Kiongozi wa Boko Haram
Kwa sasa kundi hilo linasemekana kuongozwa na Abubakar Shekau.
Msemaji wa jeshi Luteni Kanali Sagir Musa, ameiambia BBC kuwa Bwana Ibrahim, alikuwa mshirika wa karibu wa Bwana Shekau na amekuwa na sifa ya nguvu na ushawishi mkubwa.
Kanali Luteni Kanali Musa ameongeza kuwa operesheni ya kuwaska wapiganaji hao katika eneo hilo la Maiduguri inaendelea.
Tayari jeshi hilo la serikali limenasa shehena kubwa ya silaha ikiwa ni pamoja na vilipuzi, alisema Luteni Kanali Musa.
Aidha amedai kuwa Bwana Ibrahim alihusika na kifo cha Generali Shuwa baada ya kupokea agizo kutoka kwa Bwana Shekau.
Gen Shuwa ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao jeshi la Nigeria, linawaona kuwa mashujaa wa vita, kutokana na juhudi zake katika harakati za kumaliza vita kati ya jeshi la serikali na waasi wa Biafra waliotaka kujetenga miaka ya sitini.
BBC

Wednesday, November 14, 2012

HIKI NDICHO KIKOSI CHA KAZI,SEKRETARIETI MPYA YA CCM

 Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa
 Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
 Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
 Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
 Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
 Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha
Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni:Picha zote na Bashir Nkoromo)


HALMASHAURI KUU YA TAIFA YAFANYA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA.


   Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012.

  Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa  na Mwenyekiti wa ChaCha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Ambapo Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo  Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na  Mhe. Abdulrahaman Kinana .
     Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
  1. Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
  2. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Mhe. Vuai Ali Vuai.
  3. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
  4. Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
  5. Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
  6. Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.

    Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

     Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.
CHANZO-  BLOGU YA FRANCIS GODWIN

Tuesday, November 13, 2012

BENKI YA WANANCHI NJOMBE YAKOPESHA SHILINGI BILIONI 4.6

 Jengo la Benki ya Wananchi Njombe
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki y Wananchi Njombe Bw. Michael Ngwira


BENKI YA WANANCHI NJOMBE YAKOPESHA SHILINGI BILIONI  4.6
 .Wananchi wainua maisha yao kiuchumi
.yatoa mikopo ya kilimo
Na Joseph Mwambije,
Njombe                             
BENKI ya Wananchi Njombe(NJOCOBA) Wilayani Njombe katika Mkoa mpya wa Njombe  imetoa mikopo ya shilingi Bilioni 4.6 toka ianzishwe Septemba  2010 kwa wananchi zaidi ya 3000 wa kada mbalimbali na kuyainua maisha yao kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki hiyo Bw. Michael Ngwira wakati akizngumza na Mtandao huu Ofisini kwake mjini Njombe  namna Benki hiyo inavyowawezesha wananchi kiuchumi na kusaidia katika kupambana na Umaskini.
Anasema kuwa walianza kukopesha Oktoba 2010  kwa watu,SACCOS na Vikundi mbalimbali vya maendeleo   na kwamba wamekuwa wakitoa elimu namna ya kuitumia sekta ya kifedha.
Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa katika Kitengo chao cha mikopo wameanza kukopesha mikopo ya kilimo vijijini ambayo imeanza Septemba mwaka huu na tayari wameshakopesha shilingi milioni.
‘Katika mikopo ya  kilimo riba yetu imekuwa ndogo sana kuliko Benki nyingi ambapo tumekuwa tukitoa riba ya asilimia 8 na kufanya mikopo yetu ichangamkiwe na watu wengi na kwa sasa tuna maombi ya mikopo ya shilingi Bilioni 6,’anasema Mkurugenzi huyo.
Anasema kuwa Benki hiyo imekubalika  sana vijijini ambako wananchi wengi wanahitaji huduma zao na kubainisha kuwa wao wanalenga kuwasaidia wananchi ndio maana wanapeleka huduma huko ambako Taasisi za Kibenki ni chache.

KAMANDA WA MAJESHI YA MAREKANI ACHUNGUZWA ACHUNGUZWA KWA KASHFA YA NGONO

.Ni Kashfa  inayotikisa Nchi

Kamanda John Allen

Idara ya ulinzi ya Marekani inamchunguza kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, Generali John Allen, kwa kutuma ujumbe usiostahiki wa barua pepe kwa mwanamke aliye na uhusiano na aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, David Petraeus.
Waziri wa usalama Leon Panetta anasema kuwa FBI iliwasilisha kashfa hiyo kwa wizara ya usalama siku ya Jumapili.

Generali Allen, anayekana kufanya jambo lolote baya, ataendelea na majukumu yake.
David Petraeus alijiuzulu siku ya Ijumaa baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa yake.
Bwana Panetta alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa aliomba uteuzi wa Generali Allen kuwa kamanda mkuu wa majeshi ya ushirika wa Marekani na Ulaya kucheleweshwa na kwamba Rais Obama aliitikia ombi hilo.
Aliamuru uchunguzi kufanywa dhidi ya Generali Allen siku ya Jumatatu.
Generali Allen anasemekana kumtumia barua pepe Jill Kelley, mwanamke aliyeolewa kutoka Florida. Tayari mwanamke huyo alikuwa ametajwa katika kashfa dhidi ya Petraeus baada ya kuambia FBI kuwa alipokea ujumbe wa kumdhulumu kutoka kwa watu asiowajua.
Bi Kelley inasemekana alipokea barua ya kumtisha maisha yake kutoka kwa mwanamke anayejulikana kama Paula Broadwell, mwanamke ambaye bwana Petraeus alikuwa na uhusiano naye.
Msemaji mmoja wa FBI amethibitisha kuwa maafisa waliingia katika nyumba ya familia ya Paula Broadwell, jioni, lakini hakuelezea ni kwa nini.
Anadaiwa kumtumia barua pepe za kumnyanyasa,Jill Kelley, ambaye aliwaripoti kwa rafiki yake katika FBI.
Idara hiyo ilitekeleza uchunguzi wa miezi kadhaa ambao uhusiano huo kati ya Paula Broadwell and David Petraeus ulifichuliwa.
Mshauri mmoja wa Jenerali huyo anasema Petraeus ana majuto mengi na amefedheheshwa na aibu kuhusu suala hilo.
Utata huo umeibua masuali magumu kuhusu majukumu halisi ya FBI na kwa nini Ikulu ya White House haikufahamishwa kuhusu uchunguzi huo wiki iliyopita.
CHANZO-BBC

KENYA YAZINDUA TRENI IENDAYO KASI

Treni za kisasa Kenya

Shirika la reli nchini Kenya limezindua treni mpya ambayo ina mwendo wa kasi ili kutoa huduma kwa wakaazi wa viungani mwa mji wa Nairobi.
Ni treni ya kwanza ya aina yake kuzinduliwa tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963.

Treni hiyo itatoa usafiri kati ya mji mkuu na mtaa wa Syokimau na viunga vyake, viungani mwa Nairobi ambako serikali imejenga kituo cha treni ambacho ni cha kwanza kukamilishwa chini ya mradi wa ukarabati wa mfumo wa reli ambao unafanyika kwa mara ya kwanza kwa miaka 80.

Treni hiyo inanuiwa kupunguza msongamano wa magari mjini Nairobi ambao ni mojawapo ya miji unaokuwa kwa kasi barani Afrika ukiwa na watu zaidi ya milioni tatu.

Rais Kibaki aliyefungua rasmi kituo hicho, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuipanda treni hiyo.
Kituo cha treni cha Syokimau ni cha kwanza cha aina yake nchini Kenya, kikiwa na mashine za elektroniki zinazokagua vyeti vya usafiri, pamoja na skirini kubwa ambazo zinatangaza safari za treni.

Kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria sabini pamoja na miamoja na ishirini watakao simama.
Huduma hiyo itakuwa ya kasi na bora zaidi ikilinganishwa na treni za hapo nyuma na pia zitatumia njia tofauti ya reli.

Safari ya kutoka mtaa wa Syokimau inachukua dakika kumi na tano kwa treni hizo huku ikiwa mtu atakwenda kwa gari itamchukua hata masaa mawili. Itamgharimu abiria shilingi miambili za Kenya kwenda na kutoka mjini.
CHANZO-BBC

Monday, November 12, 2012

SAFARI NGUMU KUTOKA DODOMA KUPITIA MTERA KUELEKEA IRINGA

 Hapa n  barabara imefungwa katika daraja la Konze Mkoani Dodoma ambapo gari letu lilikwama wakati tukijaribu kupita pembeni.
 Hapa ni Mtera na huu ni moja ya Mkahawa wa hapo Mtera.
 Ni Mtera kabla ya kuanza kuendelea na safari kuelekea Iringa.
 Huyu ni Dereva wetu Bw. Mtutuma ambaye alijitahidi kuendesha gari kwa umakini mkubwa katika barabara hiyo na hatimaye tulifika salama Iringa.
 Nikiwa Mtera
 Safari ngumu kutoka Mtera kuelekea Iringa hapa tunapishana na Scania,pembezoni ni kingo za barabara.
 Katika maeneo mengine tulishuka kushangaa uumbaji wa Mungu,ilikuwa ni kama utalii vile,wa kwanza kulshoto ni  Mkaguzi wa Shule za msingi Songea vijijini Mr Lima ,wa pili ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Namtumbo Bw. Komba Kachulichi  na huyu mwenye kofia ni Afisa maliasili Songea vijijini Bi. Evelyn Moshi ni Mwanamke pekee tuliyekuwa naye katika safari hiyo.
 Hapa  tukiwa tunataniana.Hapa nawatumia ujumbe ndugu na jamaa kuwaeleza mazingira ya safari.
 Bado utko maeneo hayo tukishangaa uumbaji wa Mungu
 Nikiwa nimepozi na Bw. Komba (kushoto) na Bw. Mtutuma dereva wetu
Tupo pamoja

POLISI 40 WAUAWA NA WEZI WA MIFUGO KENYA


Mmoja wa polisi waliojeruhiwa, waliletwa Nairobi kwa matibabu

Takriban polisi 40 wamethibitishwa kuuawa nchini Kenya katika shambulizi lililofanywa dhidi yao siku ya Jumamosi walipokuwa wanajaribu kuokoa mifugo waliokuwa wameibwa.
Maafisa hao walivamiwa katika eneo la Baragoi, kaunti ya Samburu, Kaskazini mwa nchi.

Msemaji wa polisi aliambia BBC kuwa polisi 29 waliuawa pamoja na washambuliji watatu , lakini viongozi wa kijiji wanahofia kuwa huenda maiti zaidi wakapatikana. Hii leo miili zaidi ilipatikana na kufikisha idadi ya polisi waliouawa kuwa 40.

Wenyeji wa eneo hilo wana historia ya kupigana kwa sababu ya uhaba wa malisho ya mifugo wao
Wiki mbili zilizopita, watu 12 waliuawa katika shambulizi kama hilo kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.

Haya yanasemekana kuwa mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya polisi tangu Kenya kujipatia uhuru wake.
Maiti 11 walipatikana siku ya Jumamosi na wengine 19 kupatikana Jumapili.

Ramani ya Kenya

Inspekta wawili wakuu wa polisi wangali hawajulikani waliko.

Uvamizi huu ni pigo kubwa kwa idara ya ulinzi nchini. Baadhi ya polisi waliviziwa na kuuawa na wezi wa mifugo, katika eneo la Lomerok. Manusura tisa wangali wanapokea matibabu hospitalini.

Mauaji haya yanafikisha idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo katika wiki mbili zilizopita hadi 43.
Aidha mashambulizi haya yanatokea huku shughuli ya kuajiri inspekta mkuu wa polisi ikiendelea sambamba na polisi kususia kazi kwa sababu ya mzozo wa mishahara.
CHANZO-BBC

MATOKEO YA NEC YATIKISA DODOMA,UCHAGUZI KUHITIMISHWA LEO

.Kikwete,Mangula kuchaguliwa leo

.Sekretarieti mpya kuundwa baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti

Dodoma

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa (kushoto) akisikiliza kwa makini wakati mawaziri mbalimbali walipokuwa wakieleza ufanisi wa wizara zao kwenye mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma, jana. Pembeni kwake ni Katibu mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama. 

WASSIRA ATAJWA UKATIBU MKUU, WALIOSHINDA WATAMBIANA,  WALIOSHINDWA WATOWEKA
Full Story


WAKATI matokeo ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), yakiwa yamevuja baadhi ya wapambe wa wagombea walioshinda wameanza kusherehekea, huku wengine wakitambiana.

Hata hivyo, matokeo hayo yamekuwa machungu kwa baadhi ya vigogo walioanguka wakiwamo mawaziri, wabunge na watu maarufu.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuunda sekretarieti mpya baada ya uchaguzi wa mwenyekiti na makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar utakaofanyika leo.

Kwa upande wa Zanzibar, matokeo hayo yanaonyesha kuwa walioshinda ni pamoja na Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.

Wengine  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto.

Watu maarufu walioangukia pua katika uchaguzi huo ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Abdallah Juma Sadallah, mtoto wa Rais Mstaafu, Abdallah Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa Salehe na Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Abdisalaam Issa Khatib.

Walioshinda Bara

Majina ya wajumbe wa Nec walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (1,967), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824).

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana  na Michezo, Fenela Mukangara (984).

Wakati walioshinda Bara na wapambe wao wakitambiana, majina makubwa yaliyoanguka katika uchaguzi huo ni pamoja ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama, Richard Hiza Tambwe na Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Msafiri.

Wassira atajwa kumrithi Mkama

Habari zilizopatikana jana mjini hapa zinaeleza kuwa Wassira, anatajwa  kuwa anaweza kuikwaa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho.

Wengine wanaotajwa kuwa wanaweza kupata nafasi hiyo ya Katibu Mkuu ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  pamoja na Waziri Lukuvi.

Makundi yatambiana

Tambo na kejeli za wapambe, jana zilitawala katika viwanja vya Ukumbi wa Kizota unakofanyika Mkutano Mkuu wa CCM, baada ya baadhi ya wajumbe kuanza kusherehekea kutokana na kupata matokeo.

Nje ya ukumbi huo, tangu asubuhi wapambe wa wagombea hao walionekana wakiwa wamekaa katika makundi huku  wakinunuliana vinywaji.

Ingawa matokeo yalitarajiwa kutangazwa leo, lakini takriban wajumbe wote wa mkutano huo walionekana kuyapata hali ambayo iliwafanya walioshinda kupongezwa wakati wakiingia katika ukumbi wa mikutano.

Mtandao huu   ulimshuhudia, Waziri Mathayo akipongezwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo nje ya ukumbi wa mkutano asubuhi.

Pamoja na kupongezwa na wajumbe wa mkutano huo hata washindi wa uchaguzi huo nao walipokutana walipongezana.

Mwananchi lilimshuhudia, Shigela akimpongeza Waziri Wassira na baadaye walikumbatiana na kupongezana na Nchemba. Baadaye baadhi ya wajumbe walimbeba Shigela juu juu wakimpa pongezi.

Wakati Shigela akibebwa, baadhi ya wajumbe walimfuata Wassira na kumpongeza kwa kumshika mikono na wengine kumkumbatia huku yeye wenyewe akitamba kuwa ni mwarobani wa Chadema.

Waziri Membe akiwa ndani ya ukumbi wa mkutano, baadhi ya wajumbe wanaomuunga mkono walimfuata na kumzunguka huku wengine wakimkumbatia.

Walioanguka watoweka

Wakati walioshinda wakionekana kufurahi na kupongezwa, hali ilikuwa tofauti kwa wagombea walioshindwa, kwani baada ya kupata matokeo hayo wengi walitoweka katika eneo la ukumbi huo.

Kamati ya Uchaguzi yalala ukumbini

Kamati iliyokuwa ikisimamia uchaguzi huo jana ililala katika ukumbi wa kuhesabia kura kutokana na kazi hiyo kumalizika usiku wa manane, huku baadhi ya watu waliokuwa wakifanya kazi hiyo kunyang’anywa simu zao ili matokeo yasivuje.

Watu hao waliondoka katika ukumbi wa kuhesabia kura uliopo katika Ukumbi wa Kizota saa 12:00 asubuhi.

CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

WANANCHI NA WAWEKEZAJI WATAKIWA KUCHANGAMKIA VIWANJA NJOMBE

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmaashauri ya Mji wa Njombe Bw. George Mkindo

.HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE IMEPIMA VIWANJA 700

 .VIWANJA 206 VIMESHANUNULIWA
.VIMEBAKI VIWANJA  494
Na  Joseph  Mwambije,
Njombe
HALMASHAURI ya mji wa Njombe Mkoani Njombe imepima Viwanja  700 katika maeneo ya Mjimwema Mkoani humo na tayari imeshauza  viwanja 206 kwa  wananchi wa Halmashauri hiyo huku ikitoa wito kwa wananchi na wawekezaji Nchini kuchangamkia Viwanja hivyo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw George Mkindo wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na uendelezaji wa Halmashauri hiyo.

Anabainisha kuwa Viwanja vilivyopimwa ni  vya Makazi,Hoteli,Kumbi za Starehe,Shule na Maeneo ya  Wazi na kubainisha awali wananchi walivichangamkia Viwanja hivyo lakini kwa sasa mwitikio ni mdogo  wa wananchi kuvinunua.

‘Tulikusudia kupima Viwanja 1000 lakini tumepima Viwanja 700 na tayari viwanja 206 vimeuzwa kwa wananchi na vimebaki  Viwanja 494 hivyo ni wakati wa wananchi  na wawekezaji kuvichangamkia viwanja hivyo’anasema Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia uendelezaji wa Halmashauri hiyo anasema kuwa wanakamilisha Ujenzi wa Jengo jipya la Halmashauri ya Mji huo katika maeneo ya Lunyanyu na kwamba wanahimiza ufanyaji  wa kazi kwa juhudi na maarifa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.

ILI KUWA NA TIMU BORA YA KUOGELEA VIJANA DODOMA WAFUNDISHWA KUOGELEA

 Vijana wakijianda kuogelea wakimsikiliza Mwalimu wao wa kigeni(kulia)
 Hapa Mwalimu wao wa Kigeni akitoa maelezo,wa  pili ni Mwalimu msaidizi wa darasa la kuogelea.
 Vijana wakiwajibika.
 Vijana wakifurahia kuogelea
 Darasa likiwa limeoga
Nami nilikuwepo Dodoma hivi karibuni,hapa ni Dodoma Hoteli nafuatila darasa hilo la uogeleaji.