WAZIRI NCHIMBI AZOMEWA AFUKUZWA KATIKA MAANDAMANO YA WANAHABARI JIJINI DAR ES SALAAM
Katika ya isiyo ya kawaida wanahabari jijini Dar es Salaam wamemzomea na
kumfukuza Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Dkt Emma nuel Nchimbi katika maandamano ya Kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi leo
jijini DAR.
Hatua hiyo imetokea baada ya waziri huyo wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kufika katika viwanja vya jangwani kwa ajili ya kujipa jukumu la kupokea maandamano bila mwaliko.
Kutokana na zomea zomea hiyo ya wanahabari hao dhidi ya waziri NCHIMBI hali ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo kuondolewa na rais wa UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari polisi.
Wakati hayo yakiendelea huko mkoani Mara jeshi la polisi lateka ofisi ya waandishi wa habari Kama njia ya kushinikiza wasifanye maandamano yao

HABARI HII NI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA FRANCIS GODWIN
No comments:
Post a Comment