Wednesday, October 17, 2012

RAIS OBAMA NA MIIT ROMNEY WATOANA JASHO

Rais Obama na Mitt Romney watoana jasho

 
Barack Obama na Mit Ronmney wamemenyana katika mjadala wa pili wa kempeini za uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao
Rais Barack Obama na mshindani wake wa Republican,Mitt Romney, wametoana jasho katika mdahalo wa pili kwenye kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.
Wawili hao walikabiliana mbele ya wapiga kura ambao bado hawajaamua nani watakaye mpigia kura kwenye uchaguzi huo mwezi ujao.
Walizungumzia sera ya kodi, ajira na nishati kila mmoja akijaribu kumtia dosari mwenziye wakati wakielezea watakavyofanikisha sera zao kuhusu maswala hayo.
Walikosoana mara kwa mara huku wakati mmoja Rais Barack Obama akimtuhumu Romney kwa kusema uongo.
Mpiga kura mmoja ambaye angali kuamua mgombea atakayemchagua, alisema kuwa hali ya ubishani kati ya wawili hao haikutoa taswira nzuri kuwahusu.
Mdahalo huu ni wa pili huku wagombea hao wakisubiri mdahalo mmoja na wa mwisho siku ya Jumatatu kabla ya uchaguzi kufanyika baadaye mwezi ujao.
Mhariri wa BBC wa maswala ya Amerika ya Kaskazini, anasema kuwa baada ya mjadala wa mapema leo asubuhi, Barack Obama ameweza kujiimarisha tena kwa wapiga kura kwani alionekana kuibuka mshindi.
Katika majibizano makali kuhusu mauaji ya balozi wa Marekani nchini Libya, bwana Romney alisema kuwa tukio hilo lilifedhehesha sera ya Obama katika eneo la Mashariki ya kati.
Naye Obama alisisitiza kuwa atafanya kila awezalo kuwakamata washukiwa wa mauaji hayo.

CHANZO-BBC

No comments:

Post a Comment