Mkurugenzi Mtendaji wa Benki y Wananchi Njombe Bw. Michael Ngwira
BENKI YA WANANCHI NJOMBE YAKOPESHA SHILINGI BILIONI 4.6
.Wananchi wainua maisha yao kiuchumi
.yatoa mikopo ya kilimo
Na Joseph Mwambije,
Njombe
BENKI ya Wananchi Njombe(NJOCOBA) Wilayani Njombe katika
Mkoa mpya wa Njombe imetoa mikopo ya
shilingi Bilioni 4.6 toka ianzishwe Septemba 2010 kwa wananchi zaidi ya 3000 wa kada
mbalimbali na kuyainua maisha yao kiuchumi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Michael Ngwira wakati
akizngumza na Mtandao huu Ofisini kwake mjini Njombe namna Benki hiyo inavyowawezesha wananchi
kiuchumi na kusaidia katika kupambana na Umaskini.
Anasema kuwa walianza kukopesha Oktoba 2010 kwa watu,SACCOS na Vikundi mbalimbali vya
maendeleo na kwamba wamekuwa wakitoa
elimu namna ya kuitumia sekta ya kifedha.
Mkurugenzi huyo anabainisha kuwa katika Kitengo chao cha
mikopo wameanza kukopesha mikopo ya kilimo vijijini ambayo imeanza Septemba
mwaka huu na tayari wameshakopesha shilingi milioni.
‘Katika mikopo ya
kilimo riba yetu imekuwa ndogo sana kuliko Benki nyingi ambapo tumekuwa
tukitoa riba ya asilimia 8 na kufanya mikopo yetu ichangamkiwe na watu wengi na
kwa sasa tuna maombi ya mikopo ya shilingi Bilioni 6,’anasema Mkurugenzi huyo.
Anasema kuwa Benki hiyo imekubalika sana vijijini ambako wananchi wengi wanahitaji
huduma zao na kubainisha kuwa wao wanalenga kuwasaidia wananchi ndio maana
wanapeleka huduma huko ambako Taasisi za Kibenki ni chache.
No comments:
Post a Comment