MVUA NJOMBE ZASABABISHA HASARA YA SHILINGI MILIONI 241
Na Joseph Mwambije,
Njombe
HALMASHAURI ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe imefanya tathmini
ya mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuharibu nyumba 178 na kubainisha
kuwa maafa hayo yamegharimu shilingi milioni 241.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya mji wa Njombe Bw. George
Mkindo anasema mvua hizo zilizonyesha hivi karibuni na kuambatana na upepo
mkali zImesababisha Kaya zaidi ya 100 kukosa mahala pa kuishi na kuharibu
mashamba na nafaka majumbani.
Anasema kuwa Uongozi wa Halmashauri hiyo umefanya tahmini na
kubainisha hasara iliyotokana na mvua hizo kuwa ni shilingi milioni 241 huku
akiomba Wasamaria wema kuwasaidia wananchi waliokumbwa na maafa hayo.
‘Mvua zile licha ya kuharibu mazao mashambani na nyumba
lakini pia zimeharibu miti na mali mbalimbali na kuwasababishia wananchi kukosa
mahali pa kuishi’anasema Mkurugenzi huyo.
Anasema kuwa mvua hizo zilileta madhara zaidi katika vijiji vya Kibena ambako nyumba 91
ziliharibiwa na mvua,katika kijiji cha Nundu nyumba 35 na maeneo ya Hospitali ya Kibena numba 15.
Anataja maeneo mengine kuwa ni katika kijiji cha Ngalanga
ambako nyumba saba zimeharibiwa,kijiji cha
Hagafilo Nyumba mbili na katika kijiji cha Peluhanda nyumba moja.
Amewashukuru wananchi waliotoa ushirikiano katika kuwasaidia
wenzao waliokumbwa na maafa na kuwataka kuendelea na moyo huo wa kusaidiana na
kubanisha kuwa mvua hizo hazikuleta madhara katika maeneo ya mjini.
No comments:
Post a Comment