Saturday, November 24, 2012

VIONGOZI WA AFRIKA WAWATAKA WAASI CONGO KUSITISHA MAPIGANO

Viongozi wa Afrika wamewasihi wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuacha mashambulio.
Rais Joseph Kabila alihudhuria mkutano wa Kampala
Mwisho wa mkutano wao mjini Kampala, Uganda, viongozi hao wamewataka wapiganaji wa kundi la M23 waondoke kutoka mji wa Goma waliouteka hivi karibuni.

Viongozi hao piya walimsihi Rais wa Congo, Joseph Kabila, kushughulikia malalamiko ya wapiganaji.
Viongozi wane walihudhuria mkutano huo - Rais Paul Kagame wa Rwanda hajakuwepo.
Walipendekeza kuweka kikosi cha pamoja katika uwanja wa ndege wa Goma kitachokuwa na wanajeshi kutoka Tanzania, jeshi la Congo na M23.
Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia wapiganaji wa M23 - shutuma inazokanusha.
Baada ya kuuteka mji wa Goma, wapiganaji wamesonga ndani zaidi kwenye ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na serikali.
Mashirika ya misaada yanaonya kuwa hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya.
CHANZO-BBC

No comments:

Post a Comment