Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma Baraza Mvano akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi RC Mwambungu.
RC RUVUMA AWAASA
WANANCHI KUSHIRIKIANA NA ZIMAMOTO KWENYE MAJANGA YA MOTO
Na Joseph Mwambije
Songea
MKUU wa Mko wa Ruvuma
Bw. Said Mwambungu amewataka Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kushirikiana na
Jeshi la Zimamoto katika uzimaji wa moto
yanapotokea majanga ya moto badala ya kuwatupia mawe na kuwafanyia fujo Askari
wa Kikosi cha zimamoto.
Alitoa wito huo jana wakati akizindua Zoezi la kuzima moto
lililofanywa na Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Ruvuma na kufanyika kwenye Viwanja vya Bustani za Manispaa ya
Songea na kubainisha kuwa katika majanga ya moto mtu wa kwanza katika kuzima
moto ni mwananchi mwenyewe.
‘Muwe mnatoa taarifa
mapema kwa Kikosi cha Zimamoto badala ya
kuchelewa kutoa taarifa na Askari wa Zimamoto wana pochelewa mnawalaumu na kuwafanyia fujo wakati nyie
wenyewe mmechelewa kutoa taarifa’alisema na kuongeza
Tatizo lenu mmekuwa mkijaribu kuzima kwanza wenyewe moto pindi yatokeapo majanga ya moto mkishindwa
ndio mnawaita Askari wa Zimamoto wakati moto umeshaunguza kila kitu hivyo ni
vema mkabadilika na kutoa ushirikiano kwa
Kikosi cha Zimamoto.
Mwambungu aliongoza zoezi
la kuzima moto katika Operesheni maalumu ya kuzima moto iliyoandaliwa na
Kikosi cha Zimamoto huku Mtandao huu Cresensia Kapinga akiongoza kuzima moto kwa niaba ya Wanahabari
wa Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Bw. Baraza
Mvano alisema kuwa majukumu ya Jeshi la Zimamoto ni kuzima moto wenye madjhara pale unapotokea,kuokoa maisha
ya watu na mali zake,kufanya ukaguzi wa
Kinga na tahadhari ya moto na kutoa mafunzo ya kinga na tahadhari.
Baadhi ya Wananchi wakiongozwa na Amoni Mtega na Samweli
Mapunda wamesema kuwa mafunzo na elimu iliyotolewa na Jeshi la Zimamoto katika
Zoezi hilo imewasadia kuelewa Jeshi hilo linavyofanya kazi na hivyo watatoa
ushirikiano kwa Kikosi hicho pindi majanga ya moto yanapojitokeza.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizima moto
Mashauri wa Mgambo mkoa wa Ruvuma Kanali Fula akizima moto
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mkoa wa Ruvuma Bi. Cresensia Kapinga akizima Moto
Askari wazima moto wakizima moto
No comments:
Post a Comment