Tuesday, June 11, 2013

KAMPUNI YA VODA COM TANZANIA YAZINDUA MRADI WA MWEI (M-PESA WOMEN EMPOWERMENT INITIATIVE – SONGEA MKOANI RUVUMA

 Mkuu wa Wilaya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na akina mama wajane wa Manispaa ya Songea wakati wa uzinduzi  wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya
 Meneja wa Voda Com Fonundation Mwamvua Mlangwa akimpa maelekezo namna ya kujaza fomu za maombi ya mkopo Grace Kienyi mkazi wa kata ya Lilambo
 Washiriki wakijaza fomu za maombi ya mkopo
Kutoka kushoto ni Meneja wa Voda Com Fonundation Mwamvua Mlangwa akiteta jambo na Meneja mawasiliano wa Voda Com Rukia Mtingwa
 Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV mkoa wa Ruvuma Bw. Nathan Mtega akisalimiana na Meneja mawasiliano wa Voda Com Rukia Mtingwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) mkoani Ruvuma.
Hawa ni miongoni mwa mama wajane waliojitokeza wakisikiza kwa makini maelekezo ya mkopo wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative)
 Meneja wa Voda Com Fonundition Mwamvua Mlangwa akiwaelezea akina mama wajane  masharti ya mkopo wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative)
Meneja mawasiliano wa Voda Com Rukia Mtingwa akijaribu kuwafafanulia maana halisi ya neno mjasiriamali kwa akina mama wajane ambao ni wajasiriamali waliohudhulia katika uzinduzi wa mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) 
---------------------------------------------------------
Kampuni ya VodaCom Tanzania Limited kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii(Voda Com Fonundation) imebuni mradi wa MWEI (M-Pesa Women Empowerment Initiative) unaotumia huduma ya mpesa kuwapatia mikopo isiyo na riba akina mama wanaoishi katika maeneo ya vijiji.

Mradi huu ni mkakati wa kampuni ya Vodacom katika kusaidia juhudi za Serikali za kupiga vita umasikini hapa nchini. Mradi wa MWEI unalenga kuwaongezea  uwezo wa kiuchumi (Mitaji) akina mama wanaojishuhulisha na shughuli mbali mbali kwa lengo la kujipatia kipato.

Naye Meneja wa Voda Com Fonundition Mwamvua Mlangwa akisoma risala amesema mradi huu ulizinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Kayanda Pinda mwezi Julai 24. 2011 ambapo mpaka sasa umeshawafikia wakina mama zaidi ya 7000 Tanzania Bara na visiwani.

Kwa upande wa mkoa wa Ruvuma katika bajeti ya mwaka huu mradi huu unatarajia kuwanufaisha  akina mama 400 katika vijiji vya Peramiho, Muhukulu na Kigonsera.

 Akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti mbali ya kuishukuru kampuni hiyo ya simu za mkononi kwa kuwakumbuka akina mama wajasiriamali ambao ni walezi wakubwa wa familia lakini pia aliwaasa akina mama hao kuitumia fursa hiyo ipasavyo.

Pia amesema kuwa zipo taasisi na kampuni mbalimbali ambazo zimekuwa zikitoa mikopo huku ikiwa na mashariti magumu, riba pamoja na gharama za uendeshaji ambayo yamekuwa hayatoi fursa kwa baadhi ya makundi wakiwemo akina mama lakini imekuwa tofauti kwa kampuni ya simu ya mkononi ya voda Com kwa kupitia mradi huu wa kuwajengea uwezo akina mama wajasiliamali bila masharti magumu wala riba.

Aidha amesema kuwa serikali ya wilaya itahakikisha kuwa programu hiyo inakuwa endelevu kwa ajili ya kuwanufaisha akina mama wajasiliamali ambao ndiyo nguzo ya familia zao ambazo wanazilea bila kujali 

CHANZO-DEMASHO  BLOG

Friday, June 7, 2013

RASIMU YA KATIBU MPYA :MAWAZIRI KUKAIMU URAIS

.Ni mapendekezo ya Rasimu ya katiba mpya


  Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilali akionyesha Rasimu ya Katiba mpya kabla ya kuizindua Jijini Daressalaam.Wa kwanza  kulia ni Waziri Mkuu wa Tanzania,Mizengo Pinda.Wa kwanza  kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya  Joseph Warioba na anyemfuatia ni Makamu wa kwanz wa Rais Zanzibar Seif Sharif .

HABARI KAMILI......

 Kutokana na rasimu ya Katiba Mpya kupendekeza kufutwa kwa nafasi ya Waziri Mkuu, rasimu hiyo inapendekeza waziri yeyote mwandamizi ateuliwe kukaimu nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa rais na makamu wake hawapo nchini kutokana na sababu zozote zile.
Mapendekezo hayo ni tofauti na Katiba ya sasa ambayo inatamka kwamba ikiwa Rais na Makamu wake hawapo, basi nafasi hiyo ya juu katika nchi itashikwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mkuu aliwekwa katika orodha ya wanaoweza kukaimu nafasi hiyo katika marekebisho ya Katiba yaliyofanywa mwaka 2000 kupitia waraka maalumu wa Serikali (white paper) na baadaye kupitishwa na Bunge.
Kabla ya marekebisho hayo ya 13, Ibara ya 37(3)(a) na (b) ilikuwa ikieleza kuwa iwapo Rais na Makamu wake hawapo nafasi hiyo ilitakiwa kushikiliwa na Spika wa Bunge na kama hayupo basi Jaji Mkuu wa Tanzania ndiye alitakiwa kukaimu nafasi hiyo.
Lakini mapendekezo ya Rasimu ya Katiba Mpya katika Ibara ya 73(1)(b)na (c) inaeleza kuwa endapo Rais na Makamu wake hawatakuwapo basi nafasi hiyo itashikiliwa na waziri mwandamizi na kama hatakuwapo basi Baraza la Mawaziri ndilo litakalokuwa na dhamana ya kuchagua mtu wa kukaimu nafasi hiyo.
Hata hivyo, mtu yeyote atakayekaimu nafasi ya madaraka ya Rais, kwa namna yoyote ile, hatakuwa na madaraka ya kuteua au kumwondoa madarakani kiongozi yeyote yule aliyeteuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba au jambo jingine lolote kama litakavyoainishwa na Rais katika hati ya kukasimu madaraka yake.
“Rais atakasimu madaraka yake kwa hati maalumu aliyotia saini yake,” inaelekeza rasimu hiyo iliyozinduliwa Jumatatu wiki hii na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Kadhalika rasimu hiyo inaeleza kuwa endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili, linaweza kuandaa azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, hawezi kumudu kazi zake.
“Baada ya kupokea azimio hilo, atateua bodi ya utabibu ambayo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu ipasavyo,” inaelekeza rasimu hiyo.
Jaji Mkuu baada ya kutafakari ushauri na ushahidi wa kitabibu, atampelekea Spika hati ya kuthibitisha kwamba kutokana na maradhi ya mwili au akili, Rais ameshindwa kumudu kazi zake, na iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha hati hiyo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba kiti cha Rais kipo wazi.
Kutokana na hali hiyo, bodi ya utabibu itakayoteuliwa kwa mujibu wa Katiba itajumuisha watu wasiopungua watatu kutoka miongoni mwa madaktari bingwa wanaotambuliwa na sheria inayohusu madaktari ya Tanzania.
“Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi, kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au akili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na kushika madaraka ya Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano,” inaeleza sehemu nyingine ya rasimu hiyo.

CHANZO-MWANANCHI

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA SINGAPORE KWA KISHINDO

RAIS KIKWETE AMLIZA ZIARA YA SINGAPORE KWA KISHINDO

Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huoleo Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia. w2Mojawapo ya vivutio vikubwa katika jiji la Singapore ni hoteli hii ya kitalii na casino iitwayo Marina Bay ambayo kuna jengo la mgahawa  lenye umbo la meli juu ya majengo yake mawili w3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya  ya Singapore leo Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu. w4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore leo Juni 6, 2013.w7 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu
w10 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa miji ya Singapore leo Juni 6, 2013