Mwandishi wetu,
Songea
Jeshi la Polisi Mkoani
Ruvuma limethibitisha kumshikilia na
kumuhoji Mfanyabiashara maarufu Mkoani
humo wa vifaa vya maofisini(Stationaries) Shukuru Changwa kwa tuhuma za
ujambazi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake juzi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma,Deusdedit Nsemeki alisema ni kweli walimshikilia na kumuhoji
Mfanyabiashara huyo kwa siku kadhaa
wakimhusisha na matukio ya ujambazi huku
ndugu zake na wafanyabiashara wenzake wakihaha kumtoa korokoroni alikokuwa
akishikiliwa.
Tukio hilo
la kuhusishwa kwa Mfanyabiashara huyo na matukio ya ujambazi limegusa hisia za watu wengi kwa vile ni muumini wa dhehebu moja la
kilokole huku Kamanda Nsemeki akisisitiza kuwa Mfanyabiashara maarufu si tiketi
ya kufanya ujambazi.
“Unajua nilishangazwa na
tukio la la kushambuliwa kwa
risasi kwa Mfanyakazi wa Kampuni ya
Mohamed Enterprises majira ya saa mbili asubuhi na kuporwa nyaraka ambazo
Wavamizi walizidhania kuwa ni fedha’a;isema Kamanda huyo na kuongeza
Na tulipofuatilia tukagundua nyuma ya pazia kuna
Wafanyabiashara wakubwa wa mjini hapa wanahusika,hivyo acha wazungumze maneno yao mitaani kwamba
tumewaonea na kuwadhalilisha lakini bado tunaendelea na uchunguzi ukikamilika
watafikishwa mahakamani.
Alisema liko genge la Wafanyabiashara linaliojihusisha na
ujambazi na ndio maana ujambazi umekuwa ukifanyika hata majira ya mchana ambapo anasema yeye hawamtishi na
wakibainika watachukuliwa hatua bila kujali pesa zao.
Kamanda huyo kijana ambaye
pia Mkoa wa Ruvuma ni wa
kwaza kufanyia kazi akiwa Kamanda wa
Mkoa alisema Jeshi lake
limejipanga vyema
kuhakikisha amani iliyopo inadumishwa hivyo mtu yoyote anayejaribu kuvunja
sheria atashughulikiwa bila kujali nafasi yake katika jamii.
Alisema ulinzi katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji utaimarishwa
ili kuzuia kuingia kwa silaha toka Nchini humo lakini pia aliwaomba Wananchi na
Waandishi wa habari Mkoani humo kumpa ushirikiano katika kuwafichua wahalifu.
Katika hatua nyingine wananchi Mkoani humo wamepongeza hatua
zinazochukuliwa na Kamanda huyo katika
kupambana na uhalifu ambapo hivi karibuni Jeshi lake Mkoani humo lilifanya
Operesheni maalumu ya kuwasaka wahalifu na kufanikiwa kukamata
silaha,bangi,pombe ya moshi na kukamata mali za wizi.
Tukio hilo
linakuja baada ya matukio ya hivi karibuni ya Mkandarasi mmoja kumfyatulia
risasi mbili Askari Polisi na kumjeruhi kwenye mapaja yote mawili na jingine la
Mfanyabiashara mmoja wa Kitukio cha Mafuta cha Kisumapai na Mkurugenzi wa Kituo
hicho kuporwa milioni 30 na Majambazi.
Katika tukio laKisumapai kuporwa milioni 30 lilikuwa
kama Sinema za mapigano hivi kwani Wanyang’anyi walimvamia majira ya saa 3
usiku wakati akirejea nyumbani akiwa
kwenye gari lake ambapo
walipiga risasi kwenye tari la gari lake
na kumuamuru awape mfuko
wenye pesa.
Wakati wakimuamrisha kutoa pesa motto wake wa kike ambaye
alikuwa naye kwenye gari aliwarushia mkoba wake wakasema si huo awape mfuko
mweupe ndio wenye opesa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment