WADAU WA ELIMU RUVUMA
WAILALAMIKI SERIKALI KWA KUANZISHA SHULE KISIASA
Joseph Mwambije
Songea
WADAU wa elimu katika Mkoa wa Ruvuma wameitaka Serikali
kuacha tabia ya kuanzisha Shule kisiasa bila kuzingatia mambo ya msingi na
hivyo kukosa sifa na kusababisha kiwango cha elimu kuporomoka na kwamba hiyo ni
hatari katika ushindani wa Sokola ajira
Afrika mashariki pindi vijana wa Kitanzania watakaposhindana na wenzao wa uknda
huo kusaka ajira.
Wadau hao wa elimu waliilalamikia Serikali kwa kitendo hicho
cha kuanzisha Shule kisiasa kwenye Warsha ya siku mbili iliyofanyika kwenye
ukumbi wa Chama cha walimu Mkoa wa
Ruvuma na kuitaka Serikali kushirikisha watalaamu wa elimu inapoanzisha
Shule na si kuanzisha kwa mashinikizo ya
Wanasiasa.
Akizungumza kwenye warsha hiyo Mwalimu kutoka Wilaya ya Mbinga ,Mwalimu Samwa Muhaiki alisema Shule nyingi za Sekondari za Kata zimejengwa kisiasa ambapo
hazina maabala na vifaa vyake na walimu wa kutosha hali inayotishia kuzalisha wasomi wa baadaye wasio kuwa na uwezo katika utendaji.
Mwalimu huyo aliitka Serikali kushirikisha Watalaamu kabla
ya kuamua kuanzisha Shule ili watoe mawazo yao na vigezo vya msingi
vinavyotkiwa katika kuanzisha Shule na pia kupatikana kwa walimu wa
kutosha,majengo ya kutosha na ya kisasa na vifaa vya maabala ili Nchi iweze
kutoa watalaamu wenye uwezo wa kushindana kwenye soka la ajira la Afrika mashariki.
Akichangia hoja kwenye warsha hiyo mwalimu mstaafu wa Wilaya
ya Songea, Mwalimu Antonia Kapinga alisema Shule nyingi za vijijini hazina
nyumba za kuishi walimu hivyo walimu wanatembea umbali mrefu kwenda kwenye
vituo vyao vya kazi na kwamba tatizo jingine linalowakwaza walimu katika kazi
yao ni ushirikiano mdogo kati ya walimu na wazazi wa wanafunzi.
‘Upatikanaji wa elimu umekuwa ukibagua jinsia ya motto ambapo
watoto wa kiume wamekuwa wakipewa
kiupaumbele na hilo linajionyesha katika Sherehe nyingi ambapo wanafunzi wa
kike wamekuwa wakipangwa kwenda kunengua na kukosa muda wa kujisomea,pia Shule
nyingi hazina majengo ya faragha ya kuzungumza na wanafunzi wa kike’alisema
mchangiaji Anna Tembo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake
Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Mratibu wa elimu wa Kata ya Lilambo katika
Manispaa ya Songea Mkoani humo Dunstan Mshanga alisema Shule nyingi
zimesahaulika na zinachukua hadi miaka 10 bila kutembelewa na wakaguzi wa elimu kwa malengo ya kutambua matatizo
yayozikabili ili kuweza kuyashughulikia hali inayochangia kiwango cha elimu
kushuka.
Akifungua warsha hiyo iliyowashilikisha wadau wa elimu 30 wa
Mkoaa huo Mwenyekiti wa Chama cha walimu(Cwt) Mkoa wa Ruvuma Kastor Ngonyani
alisema kwa kuwa elimu niufunguo wa maisha na taa ya maisha Cha cha walimu
kitahakikisha elimu inatolewa katika mazingira ya haki,usawa na amani na
kuzingatia ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa maana ya
miundombinu ya majengo na samani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment