Sunday, August 26, 2012

DC NYASA APIGA MARUFUKU WANAOOGA UCHI KANDOKANDO YA ZIWA NYASA



 DC NYASA APIGA MARUFUKU WANAOOGA UCHI KANDOKANDO YA ZIWA NYASA

Na Muhidin Amri,
NYASA

MKUU wa wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma Ernest Kahindi, amepiga marufuku watu kuoga wakiwa uchi kando kando ya ziwa Nyasa kwani tabia hiyo imekuwa ikiwadhalilisha  wanawake na watu wazima.

Kahindi amelazimika kuchukua hatua hiyo,kufuatia kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu siku hadi siku wanaokwenda kuonga  wa ziwani wakiwa utupu(uchi) jambo ambalo ni kinyume na utu wao na wakati mwingine kuleta matamanio kwa wenzao, na kusababisha  kuongezeka kwa vitendo vya ngono uzembe hivyo kuchangia ongezeko kubwa la maambukizi mapya ya ukimwi.

Alisema,tabia hiyo haiwezekani hata kama ni jambo la kawaida kwa wenyeji na wakazi wa ziwa ilo, na siyo kitu chenye sifa kwa mtu mzima kuvua nguo na kuoga mbele za watu na wakati mwingine  mbele ya watoto wako bila kujali aina ya jinsia ya watoto au watu hao.

"hii tabia kuanzia sasa nazuia watu kuendelea kuonga wakiwa uchi tena mbele ya kadamnasi mtu mzima unavuoa nguo ukiwa na watoto wako sijui unapata raha gani,hakuna kabila lolote lenye tabia hii hapa mimi natoka kanda ya ziwa lakini sijwahi kuona watu wakijiachia kiasi hiki"alisema.

Alifafanua kuwa,siyo kwamba anazuia watu kuoga ziwani,isipokuwa ni lazimakuwe na maeneo maalumu ya kufanyia shughuli hiyo na maeneo hayo yatenganishwe kati ya wanaume na wanawake tofauti na ilivyo sasa ambapo idadi kubwa ya watu hao wamekuwa wakioga sehemu moja au inayokaribiana kitu ambacho ni hatari na siyo cha ustaarabu kwa Watanzania.

Kahindi alitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wakazi wa Nyasa  kutokana na usumbufu watakaoupata, hata hivyo  alisema hali  hiyo itasaidia sana kujenga kizazi chenye maadili na kuanza kukubali mabadiliko mbalimbali yanayokuja baada ya kuwa wilaya kamili tofauti na siku za nyuma ambapo Wilaya hiyo ilikuwa kama sehemu ndogo na hakukuwa na idadi kubwa ya watu.

Alitaka kuongeza kasi ya uwajibikaji kwa kila mmoja katika kukabiliana na kasi ya maendeleo ili apo baadaye wasije kuwa vibarua kwa wageni walioanza kuingia kwa wingi  wilayani Nyasa kwa ajili ya kutafuta maisha huku wenyeji wakiridhika na kipato kidogo wanachopata kutokana na uvuvi.

Juu ya zoezi la sensa lililoanza jana nchini kote,Kahindi aliongeza kuwa zoezi ilo linaendelea vizuri na amefurahishwa na hali ya utulivu  na idadai kubwa ya watu walioshiriki kuhesabiwa na kutoa wito kwa watu ambao bada hawajahesabiwa kutoa kila aina ya ushirikiano kwa makarani wa sensa.


Aliwaonya watu watakajaribu kutaka kuvuruga zoezi ilo wasifikirie kufanya hivyo kwani serikali kupitia jeshi la polisi imejipanga kikamilifu kuwashughulikia watu hao kwani wanaweza kuleta madhara kwa wengine waliokuwa tayari kushiriki sensa ya watu na makazi.

                                          MWISHO

No comments:

Post a Comment