Bw. Willon Kapinga
DIWANI wa Kata ya Ndilimalitembo Bw. Wilon Kapinga ameshinda
na kuchaguliwa kuwa Naibu Meya wa Halmashauri
ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma na kuahidi kushirikiana na Meya na
madiwani kuleta maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Awali katika uchaguzi wa ndani ya Chama chake cha CCM
alishinda kwa kupata kura 11 dhidi ya kura
nane alizopata Mpinzani wake Bw. Yobo Mapunda diwani wa kata ya
Ndilimalitembo baada ya hapo alipitishwa na Chama chake kushindana na diwani wa
Chadema.
Katika uchaguzi wa jumla Bw. Kapinga alishinda kwa
kura 19 na kumshinda diwani wa Kata ya Mango(CHADEMA)Bw.
Idd Ibrahim aliyeambulia kura nane.
Kwa matokea hayo msimamizi wa uchaguzi huo Mkurugenzi wa
Manispaa ya Songea Bw. Zakariah Nachoa alimtangaza Bw. Kapinga kuwa Naibu Meya
mpya kwa kipindi cha mwaka mmoja kuchukua nafasi ya aliyekuwa Naibu Meya Bi.
Mariam Dizumba(CCM) ambaye hakugombea.
‘Najisikia furaha kubwa kushinda nafasi hii na kwa imani ambayo Madiwani wezangu
wamenionyesha na kwa imani hii nitashirikiana na Maadiwani wenzangu kuleta
maendeleo kwenye Manispaa yetu’alisema.
Aliwataka wananchi wa Manispaa hiyo kutambua kuwa Halmashuri hiyo ni yao na kutoa ushirikiano
kwa madiwani katika kuleta maendeleo
kwenye maeneo yao kwa kuwa ustawi wa Halmashauri unategemea
Madiwani,Watalaamu(Watendaji) na Wananchi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment