Thursday, August 2, 2012

CHADEMA INAPOROMOKA KWA KASI ILE ILE WALIYOPANDA NAYO-DKT NCHIMBI

Waziri wa mambo ya ndani Dkt Emanuel Nchimbi(wa kwanza kulia) akiimba wimbo wa CCM yajenga Nchi na Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkilikiti na Meyawa Manispaa ya Songea Bw. Charles Mhagama kwenye mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Songea.


WAZIRI wa mambo ya ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la  Songea Mjini Dkt Emma nuel Nchimbi amesema kuwa Chama chake cha CCM bado kina nguvu na kwamba CHADEMA imeanza kuporomoka kwa kasi ile ile iliyopanda nayo.

Alitoa kauli hiyo juzi kwenye ukumbi wa Songea Club mjini Songea Mkoani Ruvuma wakati akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Songea  uliohudhuriwa na Wajumbe wa mkutano huo zaidi ya 900.

‘Ndugu zangu wajumbe wa mkutano huu CCM ipo na bado ina nguvu na hii inajionyesha  kuwa Wapinzani wanazidi kujiumbua na kuporomoka kwa kasi waliyopanda nayo’alisema Waziri huyo bila kufafafanua kauli hiyo.

Alisema kuwa Wabunge wengine hawaendi majimboni mwao na kazi yao ni kutoa miongozo bungeni wakati hawapeleki maendeleo jimboni mwao huku wengine wakiwa wametoa miongozo 14 Bungeni kwa kipindi hiki kifupi.

Mbunge huyo wa Jimbo la Songea mjini aliwapongeza Viongozi wa Chama hicho wapya waliochaguliwa toka kwenye Kata na Matawi yake na kuwataka kutambua kuwa viongozi bora hawatangulizi maslahi yao binafsi.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo alitoa gari la kubeba wagonjwa lenye thamani ya shilimgi milioni 32 ili liweze kuwasaidia wagonjwa kufikishwa Hospitalini hatua ambayo ilipongezwa na wananchi wa jimbo la Songea Mjini.

Waziri huyo  aliitumia nafasi hiyo kumpongeza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Songea Bw. Thomas Sabaya kwa ubabe wake kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hiyo na kumtakia kila la heri  Mkuu huyo wa wilaya.

Aidha alipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM  kwa kipindi cha Januari hadi juni mwaka 2012 toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph  Mkilikiti.
Mwisho


 Mamia ya Wapenzi wa CCM wakimsikiliza Dkt. Nchimbi.
 Mwenyekiti wa CCM Songea wa Wilaya ya Songea Mjini Bw. Hemed Dizumba akizungumza kwenye mkutano huo.
Gari la kubebea wagonjwa lililotolewa na Mbunge wa jimbo la Songea mjini Dkt emanuel Nchimbi kwa Manispaa ya Songea.

No comments:

Post a Comment