Mkurugenzi wa SDHEPHA Taifa Bw. Joseph Katto na Mwenyekiti wake Bi. Oliver Katto ambao walikuja Songea kutokana na mgogoro uliojitokeza uliotokana na kutafunwa kwa fedha hizo.
UMEIBUKA mgogoro mkubwa katika Chama cha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi(SHDEPHA+)
katika Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
ambapo chama hicho kimekuwa na Wenyeviti
wawili na Account zake zimefungwa
kutokana na ubadhirifu wa shilingi milioni 37 uliofanywa na Viongozi
walioondolewa ambao bado wanang’anga’nia madaraka.
Kufuatia mgogoro huo hivi karibuni Mkurugenzi wa SHDEPHA+
Taifa Bw. Joseph Katto na Mwenyekiti wake wa Taifa Bi. Oliver Mahenge
walikuja mjini Songea kusuluhisha
mgogoro huo mjini hapa hatua iliyoendana na kufunga Akaunti na kuzuia fedha
toka kwa Wafadhili wao ambao ni Shirika
la Walter Reed.
Mkurugenzi huyo wa Shirika hilo alisema kuwa hawawezi kufuga ufisadi
watafanya uchunguzi na wote waliotafuna fedha hizo watachukuliwa hatua za
kisheria na kwamba wanaumizwa na Mitandao ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali
kuwainglia kwenye shughuli zao.
Alisema kuwa baada ya kubaini kuwa kuna ubadhilifu wa
shilingi milioni 37 walifanya uchaguzi
na kuweka Uongozi mpya ambapo Bi. Imelda Fusi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na
kuuondoa uongozi uliokuwepo uliokuwa ukiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti Bw.
Benard Mapunda.
Katika uongozi mpya uliochaguliwa Bw. Pilimini Chanai
alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na
Wajumbe 11 wa Kamati ya Utendaji ili kukiweka Chama hicho kwenye mstari.
Alisema kuwa baada ya kufaya uchaguzi na Bw. Benard
kushindwa alienda kufunga Ofisi na kudai
kuwa uchaguzi haukuwa halali na haukufuata
taratibu na bada ya kufunga Ofisi
walishindwa kufaya shughuli zao na kulazimika kuzifanyia Hotelini katika Hoteli
Safina walikofikia.
Kwa upande wake Bw. Benard Mapunda alipoulizwa kuhusiana na
mgogoro huo na yeye kuondolewa Uongozini
alisema madai hayo si ya kweli bali fedha hizo zimefanya kazi iliyopangwa ya
kuhudumia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu,kulipa posho watu
wanaofaya kazi za kujitolea.
‘Awamu ya kwanza tulipewa shilingi milioni 17 na awamu ya
pili tukapewa milioni 20 kama kuna ubadhilifu
tusingepewa fedha nyingine za awamu ya pili na kuhusu kufunga Ofisi si kweli isipokuwa tulikuwa kwenye kazi nyingine za nje’alisema.
Anasema kuwa yeye bado Kiongozi wa Chama hicho kwa kuwa
Uchaguzi uliofanyika haukufuata Katiba
ya SHDEPHA na hivyo wanafanya taratibu
za kisheria ili waweze kumfikisha Mahakamani Mratibu wa Chama hicho wa Mkoa wa
Ruvuma Bi. Stella Komba kwa kufunga Akaunti yao.
Alisema kuwa kufunga Akaunti hizo kunawaumiza watoto yatima
na wanaoishi katika mazingira magumu 642 wanaowahudumia,wanafunzi wa Shule za
msingi 557 kwa sare za shule,viatu na daftari,Wanafunzi 10 wanaowasomesha
VETA na wagonjwa 720 wa kimwi
wanaowahudumia katika Kata 10 za Manispaa ya Songea.
Kuhusu ndoo zilizotakiwa kugawiwa kwa Wagonjwa wa ukimwi
zinazodaiwa kutumiwa kwa manufaa yao
binafsi anasema walipata ndoo 720 toka kwa Wafadhili na kati ya hizo 164
zilipotea shauri liko Polisi.
Alisema kuwa Chama hicho kina Wafanyakazi tisa wakiwemo Wakuu wa Vitengo
wanne,Meneja,Mhasibu,Mratibu,Afisa Tathmini,Katibu Muhtasi,Wafanyakazi 57 wa
kuhudumia wagonjwa kwa kujitolea ambao
wanawalipa shilingi 20000 kwa mwezi na Watoa elimu ya kimwi 15.
Kwa upande wake Mratibu wa SHDEPHA Mkoa wa Ruvuma Bi Stella
Komba anasema uchaguzi uliofanyika ni halali na
kutokana na ubadhilifu wa fedha na kunga’ngania madaraka ilhali
wmeondolewa madarakani wakaamua kuifunga Akaunti.
‘Kutokana na kunga’ngania madaraka tumeona tuwaachie Ofisi sisi tubaki na Akaunti na
sisi tutafanya kazi hata kwenye mti lakini tunatafuta vielelezo vinavyooyesha
Bw. Mapunda alikuwa akighushi sahihi ya Mwenyekiti wa mwazo ili tukabidhiwe
Ofisi kwa Polisi wamesema tukipeleka vielelezo watatukabidhi Ofisi’alisema.
Alisisitiza kuwa Bw. Mapunda amekuwa na matatizo kwenye
Uongozi wake na ndio maana
walipofika Viongozi wa Kitaifa hakwenda kuwapokea na kuzifunga Ofisi
Mwsho
Mweyekiti al;iyeng'olewa Bw. Benard Mapunda akionyesha Maboksi ya Kondomu ambazo wanazigawa kwa ajili ya kujikinga na ukimwi.
Hapa yupo Ofisini kwake,Oifisi ambayo inatakiwa aiachie
Meneja wa Mradi wa Shdepha Songea Bi. Elizabeth Kisuka akizungumza na Mtandao huu na Mhasibu wake Bw. Patrick Paul.
Mratibu wa SHDEPHA Mkoa wa Ruvuma Bi. Stella komba akizungumza na Mtandao huu kuhusu mgogoro huo.
Bw. Mapunda akionyesha picha za watoto yatima na wenye mazingira magumu wanaowahudumia
Hapa akionyesha sehemu ya ndoo 720 ambazo zinalalamikiwa kuuzwa mitaani badala ya kugawiwa kwa walengwa ambao ni wagonjwa wa ukimwi.
Akionyesha kondomu zinazotolewa kwa ajili ya kujikinga na ukimwi.
No comments:
Post a Comment