Wednesday, August 15, 2012

DC SONGEA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SEMINARI KUU PERAMIHO

Mkuu wa wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti akizungumza na Mkuu wa Seminari kuu ya Peramiho Padri titus Amigu(wa kwanza kulia).Katikati ni moja wa  Mapdri seminarini hapo .Amekuwa DC wa kwanza kutembelea Seminari hiyo kwa miaka 17 iliyopita.
 Hapa Dc Mkrikiti akizungumza na Wanaseminari
 Akipokea Kitabu cha Wageni toka kwa Padri Titus Amigu
 Akisaini kitabu cha wageni.
 Akiangalia picha za Mapadri waliosomea Seminari hiyo.DC huyo pia amesoma Seminari katika Seminari ya Uru Mkoani Kilimanjaro.Katikati ni Mwandishi wa gazeti la Majira Bi. Cresensia Kapinga.
 Akiangalia picha za  Wanafunzi wanaosoma hapo.
 Mandahari ya Seminari kuu Peramiho
 Akitembea kwenye Korido ya Seminari hiyo

 Akiangalia vitabu kwenye Makatba ya Seminari hiyo
 Akiwapungia mkono Wanaseminari wadomao hapo
 Akipata maelezo toka kwa Padri Titus Amigu kuhusu bustani ya seminari hiyo.
 Akiangalia darasa ambamo wanafunzi wanasomea.
 Akisali kanisani ili kupata uwezo wa kuweza kuwaongoza wananchi wa Songea.Biblia inasema Mfalme Suleimani aliambiwa na Mungu aombe atakalo atapewa na yeye akaomba apewe hekima ili aweze kuongoza vyema Taifa la Izraeli,naye DC aliomba hekima ili aweze kuonoza vyema.
Akipata maelezo kuhusu mti wa Mharadali huku akiwa ameshika punje za haradali.Mti huo ndio unaotajwa na Yesu kwamba watu wakiwa na imani kama chembe ya haradali wanaweza kuuambia mlima ng'oka neda ukajitupe baharini na ukafanya hivyo.

2 comments:

  1. nafurahi sana kuisikia seminari kuu ya peramiho
    MUNGU azidi kiubariki pamoja na padri:Titus Amigu mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  2. Mungu awe pamoja nanyi nyote katika kazi ya utumishi na kazinyingine zote katika kuijenga na kuiimarisha jamii ya watanzania. amina.

    ReplyDelete