Thursday, August 30, 2012

Operesheni kali dhidi ya wapigananaji Sinai



 
Na Mashirika ya habari
Ulinzi mkali Sinai
Maafisa wa usalama nchini Misri, wamewaua wapiganaji kumi na moja tangu kuanzisha operesheni kali dhidi ya wapiganaji hao katika rasi ya Sinai, mapema mwezi huu . Hii ni kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ulinzi nchini Misri.
Operesheni hiyo, iliyoanzishwa baada ya kuuawa kwa walinzi kumi na sita wa mpakani katika shambulizi lililofanywa tarehe tano mwezi huu, pia imewezesha kukamatwa kwa washukiwa 23 na hata kunasa silaha.
Maafisa wengine wa ulinzi walitarajiwa kepelekwa huko hii mnamo Jumatano kuweza kukamilisha msako wa washukiwa wa ugaidi.
Hata hivyo, hatua ya kuongeza idadi ya wanajeshi mpakani tayari imeweza kuzua wasiwasi kwa serikali ya Israel.
Tangu mwaka 1982, wakati wanajeshi wa Israel walipoondoka mpakani eneo la sinai limesalia chini ya ulinzi mkali, kufuatia makubaliano ya amani kati ya nchi hizo mbili ambayo yalisainiwa mwaka 1979, ambayo yanazuia Misri kutumia nguvu za kijeshi katika eneo hilo.
Mnamo siku ya Jumatatu,rais wa Misri, Mohammed Mursi alisisitiza kuwa nchi yake itatii mikataba yote ya kimataifa na bila ya kutaja Israel ikasema kuwa hakuna nchi zingine zinapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu hatua zake huko Sinai.
Misri ilianzisha operesheni yake ya usalama kwa jina "Operation Eagle", ambayo imehusisha maelfu ya wanajeshi wakisaidiwa na vifaru na silaha zingine nzito baada ya walinzi kumi na sita kuuawa katika operesheni dhidi ya kambi yao karibu na ukanda wa Gaza.
Baada ya kuwaua wanajeshi, wapiganaji hao walivuka mpaka na Israel katika jariibio lao kufanya shambulizi lengine. Ingawa waliuawa katiakmashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israel.
Hata hivyo yeyote amewajibika na mashambulizi hayo ingawa wanaoshukiwa sana kuhusika ni makundi ya wapiganaji ambayo yanajulikana kwa kuendesha shughuli zao mashariki mwa Sinai.
Katika siku za kwanza za operesheni hiyo majeshi yalifanya msako mkali katika maficho ya wapiganaji hao.

No comments:

Post a Comment