Wednesday, August 22, 2012

SHEIKH MKUU MUFTI SIMBA AZINDUA CHUO CHA MASHEIKH SONGEA

 Sheikh Mkuu Nchini Mufti Shaaban bun Simba akiweka jiwe la msingi kwenye Chuo cha kufundisha Masheikh na Mdrasa kilichojengwa kwa ufadhili wa Alhaji Ramadhan Kayombo katika kijiji cha Mgazini Songea Mkoani Ruvuma
 Mufti Shabaan Simba akitembea baada ya kuweka jiwe la msingi(wa kwanza kulia) ni mfadhili wa ujenzi wa chuo hicho Alhaji Ramadhan Kayombo.
 Mufti Simba akitoa dua baada ya kuweka jiwe la Msingi
 Kijana wa Kiislamu akitoa dua mbele ya Mufti.
 Sehemu ya Majengo ya Chuo hicho.
 Vijana wa Kaswida  wakipiga dufu kwenye uzinduzi wa Chuo hicho.
 Mfadhili wa Chuo hicho Alhaji Kayombo akisoma risala kuhusu ujenzi wa Chuo hicho na uenezaji wa dini ya kiislamu sehemu mbalimbali mkoani Ruvuma.
 Alhaji Kayombo akitoa maelezo kuhusu majengo  ya Chuo hicho chenye uwezo wa kuchukua kwa kuanzia Wanafunzi 30 lakini baadaye kitakuwa kinachukua wanafunzi 60 baada.
Akiendeleza maelezo kuhusu Chuo hicho.
 HABARI ZAIDI KUHUSU CHUO HICHO
Aidha katika uzinduzi wa Chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea wanachuo januari mwakani Vijana wa Kiislamu wametakiwa kujitokeza  kusoma Chuoni hapo ili kupata maadili mema katika kipindi hiki ambacho maadili yameporomoka.

Wito huo umetolewa juzi na Mufti Simba baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Chuo hicho na kuwataka vijana kwa ujula kuachana na mambo ya kihuni na kufuata miongozo ya Kurani tukufu.

Aliipongeza jamii ya watu wa kijiji cha Mgazini na Alhaji Kayombo kwa kueneza uislamu kwa vitendo na kuwataka waislamu wengine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake Mfadhili wa msikiti huo alisema kuwa hadi sasa amejenga misikiti mitano sehemu mbalimbali Mkoani Ruvuma kueneza dini ya kiislamu.Alisema katika Chuo hicho wanafunzi watakuwa wakisoma kwa miajka mitatu na kuhitimu mafunzo.

No comments:

Post a Comment