Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Michango Inakaribia Shilingi Milioni Tano
MAREHEMU DAUD MWANGOSI(ALIYESHIKA MAIKI AKIZUNGUMZA)ENZI YA UHAI WAKE.WA PILI KULIA NI RPC WA MKOA WA IRINGA MICHAEL KAMUHANDA,ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA IRINGA DKT PRISCA WARIOBAMichango zaidi bado inaendelea kutolewa. na unaweza kutoa michango hiyo na kuikabidhi kwa mjane wa marehemu kama itakavyorekodiwa hapa. Hivyo, aliye na dhamira ya kumsaidia mjane wa Marehemu bado anakaribishwa kutoa mchango wake. Mwisho wa kukusanya ni mwisho wa mwezi huu ( Septemba)
Unaweza kuchangia kwa kutumia; M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa, Tafadhali nijulishe kama utatuma kwa njia ya Western Union )Background:Ndugu zangu, Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena.Nimemfahamu Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.
Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.
Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Napendekeza ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada mkubwa.
Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri. Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
JUMJLA YA MICHANGO HADI SASA NA WATOAJI WAKE:
1. Chris Cremence 100,0002. Anonymous 500,0003. Maggid Mjengwa 100,0004. Raymond Kasoyaga 20,0005.Edward Mgogo 10,0006.Joachim Kiula 5,0007.Libory Muhanga 5,0008.Geofrey Kagaruki 10,0009.Sadiki Mangesho 10,00010. Edwin Namnauka 40,00011.Daud Mbuba 10,000 12. Anonymous 200,00013.Mikidadi Waziri 6,00014. Bungaya Mayo 5,50015. Abraham Siyovelwa 50,00016. Godfrey Chongolo 22,22217. Jacob Mwamwene 51,00018. Denis Bwimbo 153,683 19. Zanzibar Ni Kwetu 150, 46420.Felex Mpozemenya 10,00021.Rweyendera Ngonge 11,00022. Festo Temu 10,00023. Azaria Mulinda 10,00024.Khatibu Kolofete 5,00025. John Bukuku 25,00026. Abel 10,00027. Hafidh Kido 10,00028. George Mtandika 16,000 29. Shy-Rose Bhanji 200,00030. Raymond Nkya 52,00031. Maganga Sambo 10,00032. Felix Mwakyembe 10,00033. Abdul Diallo 5,00034. Newton Kyando 20,000 35. Galanos Myinga 20,00036. Anonymous ( 200 Euro) 497,000 37. Yasinta Ngonyani 50,00038. Prosper/ Willy ( Japan) 314,00039. Nuru Mkeremi 131,00040. Anonymous 50,00041. Josephine Mahimbo 50,00042. Anonymous 150,00043. Heladius Macha 30,00044. Emma Malele 10,00045. Anonymous 60,00046. Hendry Mlay 35,00047. Hosea Ngowi 10,00048. Athuman Zuber 5,00049. Hyancinth Komba 7,50050. Edson Kihongole 11,50051. Godfrey Emmanuel 20,50052. Deus M 27,00053.Sigisto Amon 10,00054.Issa Kubonya 10,00055. Richard Dalali 6,00056.Fadhili Mtanga 20,00057. Polycarp Ngowi 5,00058. Salehe Mfaume 10,00059. Deodatus Balile 20,00060. Moses Ringo 15,00061. Dr Rukoma 100,000 62. Mobhare Matinyi 100,00063. Humphrey Simba 16,00064. Fredrick Kyambile 10,00065.John Mwakyusa 20,00066. Abdul Njaidi 40,00067. Fidelis Francis 10,00068.Mutachumwa Mukandala 10,00069. Augustino Lukosi 12,50070. Goodluck Arobogast 20,00071. Lusajo Mwasaga 15,00072. Carolina Reynolds 5,50073. Rugenamu Kawa 30,00074. Innocent Kimario 5,00075. Chadema UK 1,000,000
Jumla: 4,559,000 ( Milioni Nne Na Laki Tano Na Hamsini Na Tisa Elfu)
HABARI HII NI KWA HISANI YA KWA HISANI YA MTANDAO WA MJENGWA
No comments:
Post a Comment