Na Joseph Mwambije,
Dodoma
WAANDISHI wa habari Nchini wametakiwa kuandika na kutoa maoni yao kuhusiana na mchakato wa
kupata Katiba mpya ili Wananchi wajue kinachoendelea na kwamba umakini
unatakiwa ili iweze kupatikana Katiba bora.
Wito huo umetolewa
jana(leo) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba wakati
akitoa mada kuhusiana na Mchakato wa kupata Katiba mpya kwa Waandishi wa habari
zaidi ya 36 kutoka Mikoa mbalimbali Nchini ambao wanapatiwa mafunzo ya siku
mbili ya kujengewa uwezo wa wa kuandika habari kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya.
‘Waandishi pelekeni maoni yenu kuhusiana na mchakato wa
kupata katiba mpya na pia muandike habari na makala kuhusiana na Katiba mpya
ili tupate Katiba bora yenye maslahi kwa Taifa na wananchi’anasema Bw. Kibamba.
Alisema kuwa Watanzania wasipokuwa amakini itapatikana Katiba mbovu kuliko
iliyopo sasa hivyo alisisitiza kuwa umakini unatakiwa katika kuelekea
kupatikana kwa Katiba mpya.
Mwenyekiti huyo wa jukwaa la Katiba alisema kuwa Sauti ya
Jukwaa la Katiba itapelekwa kwa wananchi na Wanahabari na kwamba Jukwa hilo pia
linalinda Katiba iliyopo isivunjwe na ndio
maana alisema kuwa alipouawa Marehemu Daud Mwangosi wa hawakunyamaza kwa kuwa Katiba ilivunjwa.
Alisema kuwa katika mchakato wa kupata Katiba mpya
Wanahabari wana nafasi ya pekee na
kuwahamasisha waandishi wa habari kuandika habari kuhusiana na Mchakato wa kupata
Katiba mpya uanaoendelea.
Aliwataka Wanahabari kutokuwa waoga kuandika habari za Katiba na kubainisha kuwa wale
watakaonyanyaswa kwa kuandika habari za mchakato wa Katiba mpya Sheria
itawalinda.
Bw. Abdinery Chihimba Mtoa mada kutoka Kenya akitoa uzoefu wa Nchi hiyo kupata Katiba mpya
Watoa mada Profesa Abdul Sharif wa Baraza la Katiba Zanzibar na Deus Kibamba wakisikiliza kwa makini uzoefu wa Katiba mpya ya Kenya.
No comments:
Post a Comment