Saturday, November 10, 2012

NJOMBE WATAKIWA KUTOKATA TAMAA YA KUTAFUTA MAENDELEO


Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Bw. George Mkindo
NJOMBE WATAKIWA KUTOKATA TAMAA YA KUTAFUTA MAENDELEO
Na Joseph Mwambije,
Njombe

WANANCHI katika  mji wa Njombe   Mkoani Njombe wametakiwa kutokata tama ya kutafuta maendeleo na kuwa tayari kupambana na mabadiliko ya dunia yanayojitokeza kila siku huku wakienda sambamba na mabadiliko ya Nchi.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Halmshauri ya mji wa Njombe George Mkindo wakati akizungumza na  Mwandishi wa habari hizi ofisini kwake kuhusiana na mwamko wa wananchi katika kufanya kazi.

Akizungumzia mwamko wa wananchi wake kufanya kazi alisema kuwa wananchi hao wamekuwa wakijituma katika kufanya kazi kwa bidii hususani katika kilimo ambapo anasema kipindi cha kilimo wengi huhamia mashambani.

Mkurugenzi huyo anasema katka Halmashauri hiyo  mahindi yamekuwa yakistawi vizuri kutokana na matumizi mazuri  ya pembejeo za kilimo na kufuata kanuni  bora za kilimo  ambapo kwa ekari moja wamekuwa wakipata  Junia 25.

‘Tunahimiza na kusisitiza maendeleo kwa watu wote na tunayapima kwa hatua na kwa sasa tupo katika hatua ya kuondoa nyumba za nyasi vijijini na  wananchi wanaitikia  mpango huo vijijini kwa kuezeka nyumba zao mabati’anasema Mkurugezni huyo.

Anabainisha kuwa mpango huo umepokelewa vyema vijijini ambapo wananchi wameanza kujenga nyumba bora za tofali za kuchoma na kuezeka kwa mabati hali inayojionyesha kuwa siku za usoni vijiji vya Halmashauri hiyo vitapiga hatua kubwa katika kuwa na nyumba bora.
mwisho

No comments:

Post a Comment