.Ni baada ya gazeti moja la wiki kulihusha na mauaji
Na Joseph Mwambije
Songea
SHIRIKA la Watawa Wabenediktine la Peramiho Mkoani Ruvuma ambalo liko chini ya Kanisa Katoliki
limekanusha habari zilizochapishwa na gazeti moja la wiki likilihusisha na mauaji
ya Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Daressalaam kitivo cha Sheria Marehemu Profesa Jwan Mwaikusa aliyeuawa kwa
kupigwa risasi mwaka Julai 13 mwaka 2010.
Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Peramiho Songea
Mkoani Ruvuma Makamu Mkuu wa Shirika
hilo ambaye pia ni Mtawa wa Shirika hilo,Fidelis Mligo anasema kuwa
ameshtushwa na taarifa hizo alizodai kuwa ni za uzushi na hazina ukweli
wowote na zina lengo la kulichafua Shirika hilo la kidini.
Kiongozi huyo anasema kuwa hamfahamu Marehemu Profesa
Mwaikusa na hajawahi kumuona na kwamba aliyewahi kuwa Mtawa wa Shirika hilo ambaye
aliwahi kutiwa hatiani Januri 2012 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea kwa kosa
la kuiliibia Shirika hilo Bw. Nestory Muhuwa(Br Aidan) na ndiye anayemjua.
Ni Kiongozi Mkuu(Abate) wa Watawa Wabenediktine wa Peramiho Mtawa Anastasius Reiser OSB
Alidai kuwa shirika hilo linapakwa matope na baadhi ya
watu wenyenia mbaya kwa maslahi yao binafsi na kusahau kuwa shirika siyo la mtu
mmoja bali ni taasisi inayotengemewa na jamii kwa utoaji huduma zinazo stahili.
Akielezea kuhusiana
na Abasia hiyo kuwa wanahisa kwenye kampuni ya uchimbaji wa madini ya UMICO ya Lukarasi Wilayani Mbinga alisema kuwa
tangia mwaka 1990 walikuwa wamejiunga kuwa wanahisa na msimamizi mkuu alikuwa
Bw.Nestory Mhuwa [Br Aidan]na baadae shirika hilo lilijitoa kutokana na usimizi
mbovu wa Mtawa huyo ambaye alifukuzwa utawa kutokana na makosa mbalimbali.
“Shirika hili siyo
la mtu binafsi bali ni taasisi inayofanyakazi kwa taratibu na kanuni kwa mjibu
wa sheria zilizo wekwa tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria ,kwa kufanya
mipango ya kupaka matope na kutaka kukwamisha shughuli zinazofanywa na shirika
hilo mbele za jamii”alisema Kiongozi
huyo.
Anabainisha kuwa Shirika hilo halikupanga mauaji hayo na
kwamba hakukuwa na ugomvi wa kugombea umiliki wa mgodi wa dhahabu wa Lukarasi ulioko
Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma na kwamba wao hawakuwa wamiliki wa mgodi huo bali walikuwa Wanahisa
kabla ya kujitoa mwaka 2010.
Mtawa huyo anafafanua
kuwa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti ni za kupikwa na kwa mujibu wa
Sheria ya Kanisa Katoliki Mtawa haruhusiwi kuwa na mali binafsi na hivyo
umiliki wa hisa katika mgodi huo haukuwa wa siri.
Mwisho
haya magazeti inabidi kabla ya kuandika habari nzito kama hizi yafanye kwanza utafiti wa habari husika
ReplyDelete