Mkurugenzi Mtendaji wa Halmaashauri ya Mji wa Njombe Bw. George Mkindo
.HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE IMEPIMA VIWANJA 700
.HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE IMEPIMA VIWANJA 700
.VIWANJA 206 VIMESHANUNULIWA
.VIMEBAKI VIWANJA 494
Na Joseph Mwambije,
Njombe
HALMASHAURI ya mji wa Njombe Mkoani Njombe imepima Viwanja 700 katika maeneo ya Mjimwema Mkoani humo na
tayari imeshauza viwanja 206 kwa wananchi wa Halmashauri hiyo huku ikitoa wito
kwa wananchi na wawekezaji Nchini kuchangamkia Viwanja hivyo.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw George
Mkindo wakati akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusiana na
uendelezaji wa Halmashauri hiyo.
Anabainisha kuwa Viwanja vilivyopimwa ni vya Makazi,Hoteli,Kumbi za Starehe,Shule na
Maeneo ya Wazi na kubainisha awali
wananchi walivichangamkia Viwanja hivyo lakini kwa sasa mwitikio ni mdogo wa wananchi kuvinunua.
‘Tulikusudia kupima Viwanja 1000 lakini tumepima Viwanja 700
na tayari viwanja 206 vimeuzwa kwa wananchi na vimebaki Viwanja 494 hivyo ni wakati wa wananchi na wawekezaji kuvichangamkia viwanja hivyo’anasema
Mkurugenzi huyo.
Akizungumzia uendelezaji wa Halmashauri hiyo anasema kuwa
wanakamilisha Ujenzi wa Jengo jipya la Halmashauri ya Mji huo katika maeneo ya
Lunyanyu na kwamba wanahimiza ufanyaji
wa kazi kwa juhudi na maarifa kwa wananchi wa Halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment