Friday, November 9, 2012

WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI YA LORI MKOANI NJOMBE

 Wananchi wakitoa Lor lililoziba njia  baada ya kupata ajali na kuua watu wawili.
Hapa likiwa limeziba njia
Na Joseph Mwambije,
Njombe
WATU wawili wakazi wa Mkoani Njombe  wamefariki dunia kutokana na ajali mbaya ya Lori lenye namba  T 230ARG iliyotokea katika Milima ya Lukumbule Mkoani Njombe ambapo Lori hilo liliacha njia na kupiga kuta za barabara na kasha kuziba barabara.

Waliofariki katka ajali hiyo  iliyotokea jana wametambulika kuwa ni  Felix Mligo mmiliki wa gari hilo na  Kondakta mmoja aliye fahamika kwa jina moja la Majaliwa huku dereva wa gari hilo akiwa amenusurika na kujeruhiwa.

Ajali hiyo imeleta simanzi kubwa kwa wasafiri walikuwepo eneo la tukio waliolazimika kusimamisha safari na kulitoa gari hilo liloziba njia  ambapo wengine walisikika  wakisema Mmiliki wa gari hilo  amekufa na gari lake ambalo hakuwa na muda mrefu toka alinunue.

Mtandao huu ulishuhudia msururu mkubwa wa magari kutoka Songe na kutoka Njombe baada ya kusimama kutokana ajali hiyo iliyosababisha kufungwa kwa barabara.

Mfanyabiashara aliyesafirisha mbao zilizokuwa kwenye Lori hilo Bw. Kamilo anasema kuwa gari hilo  lilitoka Njombe mjini  Novemba 7 saa 6. Usiku nay eye alitakiwa kusafiri nalo lakini alikataa kusafiri pamoja na gari hilo kwa kuwa ilikuwa usiku.

‘Unajua mimi nilitakiwa kuwa miongoni mwa marehemu katika ajali hii kwa kuwa tulibishana na marehemu Mligo kuwa tusiondoke kwa kuwa usiku mimi nikakataa hivyo na mshukuru Mungu ingawa nimepata hasara kutokana ajali hii’alisema Bw. Kamilo wakati akizungumza gazeti hili katika eneo la tukio.

Baada ya Wasafiri wa pande zote mbili wa kutokea Mkoani Ruvuma na wa kutoke Mkoani Njombe na Iringa kufanikisha kulindoa gari hilo lililoziba njia waliendelea na safari.


 Msururu wa magari baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha gari kuziba njia.
 Baada ya Lori lililosababisha ajali kutolewa barabarani
Mbao zilizopakizwa kwenye gari hilo zikiwa zimetapakaa baada ya kutokea kwa ajali.

No comments:

Post a Comment