Hoteli ya Agereenment ni miongoni mwa Hoteli zilizokumbwa na ukosefu wa maji .Nimepozi mbele ya Hoteli hiyo nikitafakari tatizo la ukosefu wa maji katika Mji wa Njombe.
Nikitafakari ni kwa nini Hoteli nzuri kama hii ikose maji
NYUMBA ZA KULALA WAGENI NJOMBE ZAKOSA MAJI
.Wateja washindwa kupata huduma ya kuoshewa maji
.Wengine wakosa maji ya kuoga
Na Joseph Mwambije,
Njombe
NYUMBA za kulala wageni,Taasisi na nyumba nyingine za
wananchi zimekumbwa na tatizo la ukosefu wa maji na kufikia hatua wateja kukosa
hadi maji ya kuoga katika Mji wa Njombe kutokana na tatizo kubwa la maji
lililoukumba mji huo.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilli umebaini kuwa Mji huo
umekumbwa na tatizo la maji kwa mwezi
mmoja sasa hali inayofanya wananchi na wageni kulalamikia tatizo hilo.
Mwandishi wa Mtandaohu u aliyetembelea nyumba ya kulala
wageni ya Mwambasa na Monica Lodge
alishuhudia hali mbaya zaidi ambapo wageni waliofikia nyumba hiyo ya kulala
wageni wamekuwa wakishindwa kuoshewa
nguo zao kwa madai kuwa hakuna maji.
Katika Nyumba ya kulala Wageni ya Monica hali ni mbaya zaidi
ambapo wakati mwingine wateja wamekuwa wakishindwa hata mai ya kuoga
na kulalamikia tatizo hilo na kuitaka Serikali kushughulikia tatizo hilo
haraka.
Mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni ya Monica
ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini anasema kuwa wamelazimika kuajiri
Mfanyakazi kwa ajili ya kutafuta maji ambayo wanayatoa mbali toka visima
mbalimbali katika mji huo.
Akizungumza na gazeti hili jana Muhudumu huyo anasema kwa siku hiyo ya jana
walikuwa wamebakiwa na lita 10 za maji pekee hivyo hata maji ya kuoga wateja
wao yanakosekana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe
Bw. George Mkindo amethibitisha kuwepo tatizo hilo na kubainisha kuwa tatizo
hilo linatokana Mji kukua na watu
kuongezeka wakati mfumo wa maji ni wa zamani. Ambapo wanawahudumia wananchi
55,000 kwa huduma ya maji.
Anasema kuwa tatizo jingine linatokana na mabadiliko ya
nchi na uharibifu wa maji na kusababisha
vyanzo vya maji kukauka hali inyosababisha kuwa na tatizo kubwa la maji katika
kipingi cha Kiangazi na kwamba mvua inaponyesha matatizo ya maji yanaisha.
Anasema kuwa tatizo hilo litakwisha baada ya kukamilisha
Mradi mkubwa wa maji kutoka chanzo cha maji cha Hagafilo na kuunganishwa na
Chemchem ya Myenza na kwamba utaratibu
unafanyika kutatua tatizo hilo la maji
haraka.
No comments:
Post a Comment