Wasema 2012 walitimiza majukumu yao,2013 wataongeza ari ya kutimiza majukumu yao
Akishusha kitambaa kama ishara ya kuukaribisha mwaka 2013.Kushoto ni Mkuu wa Utawala wa Kikosi hicho Kapteni Gerald Lwenyagira.
Na Joseph Mwambije
Songea
WANAJESHI katika Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa cha 842 Mlale Wilaya ya
Songea Mkoani Ruvuma wametakiwa kuzingatia na kutii miiko ya Jeshi la Wananchi
wa Tanzania(JWTZ) ili kudumisha amani na mshikamano uliopo Nchini.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni wakati wa Sherehe za kuuaga
mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 na Mkuu wa Kikosi hicho Meja Thomas Mpuku
wakati akizungumza kwenye sherehe hizo zilizofanyika kikosini hapo.
Alichukua fursa hiyo kuzipongeza familia za Wanajeshi zilizodumisha
amani na upendo katika familia zao
kikosini hapo kwa mwaka 2012 na kuzitaka
familia za wanajeshi zilizoshindwa kuishi hivyo zijirekebishe na kuishi
kwa amani na upendo mwaka 2013.
Kwa upande wake Mkuu wa utawala wa Kikosi hicho Kapteni
Gerald Lwenyagira alisema kuwa kikosi hicho kilijitahidi na kutimiza majukumu
yake mwaka 2012 katika malezi ya Vijana,uzalishaji mali na kufanya Operesheni
mbalimbali za Kijeshi ikiwemo Operesheni ya miaka 50 ya uhuru na Opersheni
Sensa na kwamba kwa mwaka 2013 wataongeza ari ya kutimza majukumu yao.
Akishusha Kitambaa.Akisalimiana na baadhi ya Askari.
Mkuu huyo wa Kikosi Meja Thomas Mpuku akizungumza Kikosini hapo hivi karibuni.Kushoto ni Mkuu wa Utawala Kikosini hapo Kapteni Gerald Lwenyagira.
No comments:
Post a Comment