Msimamizi wa NHIF Mkoa wa Ruvuma,Silively Mgonza akizwahamasisha
Wananchi wa Kijiji cha Madaba kujiunga na mfuko huo.
Na Joseph Mwambije,
Songea
WANANCHI Mkoani Ruvuma wamehamasishwa kujiunga na mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya na ule wa afya ya Jamii ili waweze kupata huduma za afya
zinazokidhi viwango kwa kuwa wanachama wanapo kuwa wengi ndivyo utoaji wa
huduma hizo unakuwa rahisi.
Wananchi walihamasishwa kujiunga na huduma hizo juzi katika
Kijiji cha Wino Songea Vijijjini Mkoani Ruvuma na Viongozi wa Bima ya afya (NHIF)
Kitaifa na Kimkoa ambapo mbali na uhamasishaji huo Viongozi hao pia walitoa mashuka
kwa Kituo cha Afya cha Madaba,Zahanati ya Mahanje na ya Wino na tisheti vyote
kwa pamoja vikiwa na thamani ya shilingi milioni moja.
Akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Zahanati ya
Wino uliowahusisha Wananchi wa kijiji Cha Wino na Viongozi wa ngazi ya
Kata na Kijiji hicho pamoja na wanachama
wa mfuko huo Meneja wa Wanachama wa Bima ya Afya,Elentruda Mbogoro amewataka
Wanachi kujiunga kwa wingi katika mfuko huo uli kurahisisha utoaji wa huduma
badala ya kulalamikia huduma zinazotolewa.
Meneja huyo anasema kuwa baadhi ya maeneo huduma za mfuko
huo zinakuwa hazikidhi viwango kwa kuwa
wanachama ni wachache hivyo na fedha nazo zinakuwa hazijitoshelezi na
kubainisha kuwa dhana ya kusema nachangi huduma lakini siugui si sahihi.
‘Unapokuwa umechangia huduma na haujaugua nalo ni jambo jema
kwa kuwa hakuna mtu anayependa kuuugua hivyo unakuwa umemchangia mtu mwingine
anayeumwa kupata huduma za matibabu’alisema Meneja huyo.
Awali katika Taarifa yake Afisa Mtendaji wa Kata ya
Wino,Notiwele Mtewele alisema kuwa Kata hiyo yenye Wakazi 12800 na Vijiji
vitano ina wanachama 84 wa huduma ya afya na inakabiliwa na upungufu wa madawa
kwenye Zahanati yake.
Naye Msimamizi wa NHIF Mkoa wa Ruvuma,Silively Mgonza
anasema kuwa wamejipanga kuondokana na tatizo la dawa kwa kutoa huduma ya Bima ya afya kwa Maduka ya dawa
muhimu yaliyosajiliwa na TFDA na kwamba tayari maduka mawili ya dawa mkoani humo
yameanza kutoa huduma hiyo lengo likiwa wananchi wapate huduma ya dawa.
Kwa upande wake Mganga wa Kituo cha Afya
Madaba,Maxencius Mahundi ameshukuru kwa
msaada huo na kubainisha kuwa walikuwa wakikabiliwa na upungufu wa mashuka na
kwamba yaliyopo yalikuwa yamechakaa.
No comments:
Post a Comment