Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Mkoa wa Ruvuma,Alex Nchimbi akizungumza wakati akifungua Baraza la UVCCM Mkoa wa Ruvuma.Kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Ruvuma,Mwajuma Rashid.
KUPINGA GESI KUSAFIRISHWA NI KUPINGANA NA BABA WA
TAIFA-NCHIMBI
Na Joseph Mwambije
Songea
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Mkoa wa Ruvuma
Bw. Alex Nchimbi amesema kuwa kupinga
gesi kusafirishwa kwenda Daressalaam ni kupingana na Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere aliyetaka kuwepo na mgawanyo sawa kwa
rasilimali za Taifa kwa Mikoa yote Nchini.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua Barazaza la Vijana wa Chama hicho
lililofanyika hivi karibuni mjini Songea na kuwataka Vijana wa Chama hicho kuwa
makini wanapozijibia hoja za Kitaifa si kukurupuka kama hiyo ya gesi.
Alisema kuwa Baba wa Taifa aliweka mgawanyo sawa wa rasilimali za Taifa
na kuondoa ubaguzi wa kidini na Kikabila huku akiitambulisha lugha ya Kiswahili
kuwa lugha ya Taifa.
‘Tukisema rasilimali zinufaishe Mkoa husika pekee je Mikoa
isiyokuwa na kitu itafanyaje,kwa sisi Mkoa wa Ruvuma mahindi yetu yamekuwa
yakilisha Tanzania yote na Nchi nyingine za jirani’alisema.
Aliwataka Vijana hao kushirikiana na Jamii klatika masula ya
kijamii pamoja nma elimu katika Shule za Sekondari na Shule za Msingi ambako
alidai kuwa huko Umoja huo umekuwa ukipwaya wakati Vyama vya upinzani
vimejikita kwa kiwango kikubwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph
Mkirikiti ambaye alikuwepo kwenye Baraza hilo
aliwataka Vijana kushirikiana katika kuijenga Jumuiya yao ya UVCCM na
Chama chao kwa ujumla huku wakiwaunga mkono wanaokijenga Chama hicho badala ya
kuwapinga.
Alimpongeza mjumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana Taifa
Bw. Alfan Kigwenembe kwa kazi nzuri ya kufanya mikutano na kuongea na vijana
mbalimbali wa Chama hicho na ambao si wa Chama hicho huku akiyazungumzia
masuala mbalimbali ya msingi na kuyatolea ufafanuzi.
No comments:
Post a Comment