Alfan Kigwenembe akizungumza na Vijana katika moja ya Mkikutano yake.
VIJANA MSISUKUMWE KATIKA MAKUNDI YA KUVURUGA
AMANI-KIGWENEMBE
Na Joseph Mwambije,
Songea
VIJANA wametakiwa
kutosukumwa katika makundi ya kuvuruga amani,kutumika kisiasa na kuandamana
bila sababu za msingi na matokeo yake wao ndio wanaoathirika katika vurugu za
kisiasa na maandamano na kuziacha familia zao zikiahangaika.
Wito huo ulitolewa juzi na mjumbe wa Baraza kuu la vijana wa
CCM(UVCCM)Alfan Kigwenembe wakati
akizungumza na vijana kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Msamala mjini
Songea mambo mbalimbali yanayowahusu Vijana.
Mwanasiasa huyo kijana alikuwa akizungumza na Vijana wote wa
Manispaa ya Songea bila kujali itikadi zao za kisiasa kwa kuwa wao ndio
rasilimali ya Taifa na wamekuwa
wakitumika vibaya na Wanasiasa kwa maslahi yao.
Alibainisha kuwa katika maandamano zinapotokea fujo vijana
wanaathirika kwa kupata ulemavu wa maisha na wakati mwingine kupoteza maisha na
kuziacha familia zao zikihangaika huku Viongozi wa Siasa waliowasukuma kuandamana wakishindwa
kuwasaidia na kusaidia familia zao baada ya wao kupoteza maisha.
‘Vijana lazima mtambue kuwa nyinyi ni rasilimali ya Taifa
hivyo hampawi kushiriki katika fujo na kuvuruga amani ya Nchi yetu na
kuandamana katika maandamano yasiyokuwa ya msingi na badala yake mjiunge katika
Vikundi vya ujasiriamali ili mjiletee maendeleo’alisema Mwanasiasa huyo.
Aliwataka vijana kufanya kazi kwa bidii ili
kujileteaaendeleo kwa kuwa maisha bora hayaletwi kwa kucheza bao na Pool na
badala yake yanaletwa kwa kufanya kazi kwa bidii na kuongeza kuwa miradi mbalimbali
ya madini Mkoani Ruvuma ukiwemo wa Urenium utaongeza ajira kwa Vijana.
No comments:
Post a Comment