Mkurugenzi wa maji safi na usafi wa mazingira(SOUWASA) Songea,Mhandisi Francis
Kapongo akitoa malezo kwa Naibu Waziri wa maji Mhandisi Binilith
Mahenge(kushoto) kuhusu Bwawa la kienyeji la kuhifadhi maji la Ruhila kwenye
chanzo cha mto Ruhila.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa SOUWASA,Wilson Mandia. |
NAIBU WAZIRI WA MAJI AIKATAA TAARIFA YA MKURUGENZI WA
SOUWASA SONGEA
Na Joseph Mwambije
Songea
NAIBU Waziri wa maji
Mhandisi Binilithi Mahenge ameikataa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira(SOUWASA) Mhandisi Francis Kapongo kutokana na mapungufu na kutoeleza
mapato na matumizi ya fedha inazozipata na zinazotolewa na Serikali na
Wafadhili mbalimbali.
Aliikataa taarifa hiyo juzi mara baada ya kusomewa katika
ukumbi wa Mamlaka hiyo na kushangazwa kuwa na mapungufu mengi na kutoeleza
tatizo la maji lililojitokeza mwaka jana na kupelekea Wizara hiyo kutuma
Watalaamu kuja kuchunguza.
‘Hii taarifa ina mapungufu mengi,haina mapato na matumizi na
haijaeleza tatizo kubwa la maji lililojitokeza mwaka jana na Wizara ya maji
ilivyolishughulikia hivyo basi niandalie taarifa nyingine ili matatizo niweze
kuyashughulikia’alisema Naibu Waziri huyo ambeye yuko katika Ziara ya siku tano
Mkoani Ruvuma.
Alisema kuwa taarifa hiyo ina mapungufu mengi na haijaeleza
wananchi wanahitaji kiasi gani cha maji,mapungufu ni kiasi gani na inatoa
huduma kwa wananchi wangapi na kushangazwa na
Mkurugenzi huyo kutoa taarifa yenye mapungufu kiasi hicho na kusema
taatifa aliyoitoa haifanani na Nafasi yake.
Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi huyo kumuandalia
taarifa nyingine ambayo itaeleza matumizi ya shilingi bilioni 36 zilizotolewa na Wafadhili kwa
kushirikiana na Serikali jinsi zilivyotumika katika Mradi mkubwa wa maji wa
mtandao wa maji taka ambao bado haujakamilika.
Alimuagiza Mkurugenzi huyo kuhakikisha Watumiaji wote wa
maji ya Mamlaka hiyo wanafungiwa mita na kuwasimamia vizuri Wateja wao katika
kulipia maji wanayotumia na wahakikishe Mamlaka hiyo inajiendesha kwa faida na
kubainisha kuwa makusanyo ya Mamlaka hiyo ni kidogo.
Awali akisoma taarifa hiyo kwa Naibu Waziri alisema kuwa
kuna vyanzo 9 vya chemichemi vilivyopo katika milima ya Matogoro ambavyo
huzalisha maji kwa matumizi ya mji wa Songea na kwamba havitoshelezi mahitaji
na hivyo chanzo cha mto Luhira hutumika kuongeza wingi wa maji.
Mhandisi Kapongo katika taarifa yake alisema Mtandao wa
bomba wa maji safi una urefu kilomita 37 na kwamba mabwawa 6 yamejengwa kwa
ajili ya shughuli za kutibu majitaka na kwamba kwa sasa Wateja waliounganishwa
na huduma hiyo ni 1020 huku lengo likiwa kuwaunganishia wateja 1500 ifikapo
juni 2013.
Alisema kuwa wanajipanga kuongeza vyanzo vipya vya maji na
kumalizia ujenzi wa mtandao wa maji safi katika maeneo katika Kata sita za Manispaa hiyo ambao
utagharimu shilingi bilioni 49.52 hadi kukamilika.
Pia alisema kuwa wanajipanga kupanua huduma ya maji taka na
maji safi katika maeneo ya mapya ya mji ambayo ni
Mshangano,Msamala,Ruhuwiko,Chabruma,Seedfarm,Mateka,Ruvuma kwa shilingi bilioni 40.314.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph
Mkirikiti alisema atasimamia maagizo yote ya ya Naibu Waziri huyo kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora ya maji na kutatua kero ya maji kwa wananchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment