Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo-Abdula Lutavi. |
Madini ya Urani yanayotarajiwa kuanza kuchimbwa Wilayani Namtumbo na Kampuni ya Mantra Tanzania.
KAMPUNI NYINGINE TATU ZAIDI
NAMTUMBO ZINAFANYA UTAFITI WA MADINI
YA
URANI
Na Joseph Mwambije,
Namtumbo
KAMPUNI tatu zaidi
Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma zinafanya utafiti wa madini ya Urani ukiondoa Kampuni ya Mantra Tanzania Limited
ambayo iko mbioni kuanza kuchimba madini hayo
na ikiwa madini hayo yataanza kuchimbwa yatainua uchumi wa Wilaya hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bw. Abdula Lutavi wakati akizungumza na
Waandishi wa habari Wilayani humo kuhusu maendeleo ya Wilaya hiyo kwa kipindi
cha miaka saba kuanzia mwaka 2005 hadi
2012.
Mkuu huyo wa Wilaya amezitaja Kampuni hizo kuwa ni Western
Metal (T) Ltd,Uranex Tanzania Limited na Frontier Resources Tanzania
Limited na kwamba kupitia Kampuni ya
Mantra Tanzania Limited Wilaya hiyo inatarajia kuwa na uwekezaji mkubwa wa
madini hayo baada ya makubaliano ya Serikali na Kampuni hiyo kukamilika.
Anasema kuwa kwa kipindi cha miaka saba Wilaya hiyo imepiga
hatua kubwa katika masuala mbalimbali ambapo uwezo wa Wilaya hiyo kukusanya
mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani umeongezeka na kufanya Wilaya hiyo kuweza
kuboresha maisha ya Wananchi wake.
‘Tumepiga hatua kubwa katika matumizi bora ya ardhi ambapo ndani ya kipindi cha
miaka saba tumepima Viwanja 7,307,mashamba 52,881.79,vijiji 57,tumetoa hati
miliki za mashamba za kimila 6345,hatimiliki za kimila kwa wanawake 835,vyeti
vya ardhi za vijiji 38 na tumetenga maeneo 27 kwa ajili ya matumizi bora ya
ardhi ’alisema.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka saba Wilaya hiyo
imefanikiwa kuboresha miundombinu yake
ya barabara na baraba ya lami
inayoiunganisha Wilaya hiyo na Wilaya ya Songea inatarajiwa kukamilika hivi karibuni na kwamba katika Sekta ya elimu wamefanikiwa kupunguza
mimba kwa wanufunzi na wameweka mikakati kuzuia kabisa mimba kwa Wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw.
Mohamed Maje anasema kuwa wameweka mikakati kuipaisha Wilaya hiyo kiuchumi
kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo
na kupunguza umaskini kwa wananchi wake.
Mwisho
Mjiolojia wa kampuni inayotafiti madini ya Urani Namtumbo,John Mtukula akitoa maelezo ya madini hayo wakati Wanahabari hao walipotembelea kwenye eneo la utafiti wa madini hayo Wilayani Namtumbo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo,Mohamed Mataje(kulia) akinong'onezana jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Steve Nana.
Madini ya Urani
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo.Kutoka kulia Albano Midelo wa gazeti la Kiongozi,Amon Mtega -Mtanzania,Cresensia Kapinga-Majira na Leticia Nyoni Meneja wa Kampuni ya Business Times Ruvuma.
Wanahabari hao wakiwajibika
No comments:
Post a Comment