Afisa Mipango wa Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa habari Nchini(UTPC) Bw. Jacob Kambili akizungumza
wakati akitoa mafunzo kwa Viongozi wa Klabu ya Waaandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma(RPC) jana Mjini Songea kwenye Ofisi za Klabu hiyo.
VIONGOZI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA
WANOLEWA
Na Joseph Mwambije
Songea
VIONGOZI Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma(RPC) wamepatiwa mafunzo ya Uongozi
ili kuondokana na migogoro ya mara kwa
mara inyozikumba Klabu nyingi za Vyama vya Waandishi wa habari Nchini na
kudumaza maendeleo .
Klabu hiyo imeanza Vyema kwani mafunzo hayo yametolewa
jana katika Ofisi za Chama hicho mjini Songea na Muungano wa Klabu za
Waandishi wa habari Nchini(UTPC) ili kuwajengea uwezo Viongozi wa Klabu hiyo.
Mkufunzi katika mafunzo hayo alikuwa Afisa Mipango wa
UTPC,Jacob Kambili ambaye aliwataka Viongozi wa Klabu hiyo kushikamana na
kushirikisha wanachama katika mipango yao na kwamba ushirikishwaji utaondoa
migogoro katika Klabu.
‘Tunawajengea uwezo Viongozi wa Klabu kwa kuwa Klabu zikiwa imara na UTPC itakuwa
imara kwa kuwa Taasisi hiyo ni mali ya Klabu za Waandishi wa habari Nchini’alisema
Kambili.
Aliwataka Viongozi wa Klabu hiyo kuwa Waadilifu,Wenye
maadili na Mabalozi wema wa Chama chao,kutunza
siri za Vikao na kuwa na misimamo thabiti na kukubali kukosolewa huku wakiwa
wasikilizaji zaidi kuliko wazungumzaji.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Klabu hiyo,Andrew Chatwanga amesema Klabu hiyo imeanza vyema
Mwaka huu kwa kuwa mafunzo yamefanyika Januari mosi hivyo mwaka huu utakua mwema kwa Klabu hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Andrew Kuchonjoma alisema kuwa
Lengo la Klabu hiyo ni kuonyesha njia ndani
na nje ya Klabu hivyo mafunzo yao yatawasaidia kufikia malengo makubwa
iliyojiwekea ikiwa Kuanzisha Redio na Televisheni Mkoani Ruvuma.
Mafunzo hayo yametolewa kwa Kamati yote ya Utendaji ya Klabu
hiyo huku yakihudhuriwa na Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo na yataendelea
kutolewa na Klabu nyingine Nchi nzima.
Mwisho
No comments:
Post a Comment