Na Julius Konala,MbingaWAKULIMA wa zao la kahawa katika kijiji cha Kipapa Kata ya Kipapa iliyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuweka ruzuku ya pembeo katika zao hilo kama ilivyo katika zao la mahindi ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuinua uchumi wao.
Ombi hilo lilitolewa juzi na mmoja wa wakulima wa zao hilo,Oddo Ngahi wakati akizungumza na Mtandao huu wilayani Mbinga kwa niaba ya wakulima wenzake namna ya kuinua uzaishaji wa zao hilo .
Alisema kuwa uzalishaji wa zao hilo umeshuka ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kutokana na baadhi ya wakulima kushindwa kumudu ghalama za pembejeo kwa ajili ya zao hilo.
Aidha amewaomba maafisa ugani wa kata kuwatembelea wakulima wa zao hilo vijijini kwa ajili ya kuwaelimisha juu ya utunzaji wa mashamba na jinsi ya kupambana na wadudu aina ya vidung'ata ambao hushambulia zao hilo.
Mkulima huyo alibainisha kuwa mpaka sasa kaya zaidi ya 40 katika
kitongoji cha kishingo kilichopo katika kijiji cha kipapa zimeathilika na ugonjwa uliosabababishwa na wadudu hao.
Ili kukuza kilimo cha zao hilo wanaiomba Serikali kuwapa mkopo kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha zao hilo Wilayani humo jambo litalosaidia kukomesha uuzwaji wa kahawa mbichi maarufu kwa jina la magoma.
Akizungumzia kwa upande wa soko la zao hilo alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2011 kilo moja ya kahawa iliuzwa kwa bei ya shilingi 6000 wakati msimu wa mwaka 2012 kilo moja ya zao
hilo imeuzwa kwa bei ya shilingi 3000 jambao ambalo limezidi kuwakatisha
tamaa wakulima hao.
Alisema kuwa amesema pamoja na changamoto zinazo kabili zao hilo ameweza kufanikiwa kujenga Nyumba ,kununua Pikipiki na kusomesha watoto kutokana na faida aliyoipata katika zao la kahawa baada ya kujikita katika shughuli za kilimo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment