Friday, January 18, 2013

WAJAWAZITO WADAI KUNYANYASWA MALAWI KUTOKANA NA MGOGORO WA ZIWA NYASA

Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Malawi Joyce Banda, wakitabasamu huku wakipeana mikono mara baada ya mazungumzo mjini Maputo
WAKATI mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyassa unaoendelea kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali na Malawi haujapatiwa ufumbuzi, mamia ya Wajawazito kutoka Tanzania kuelekea nchini Malawi kupata huduma ya Afya wamedai kunyanyaswa na baadhi ya watoa huduma katika Hospitali nchii humo.
Wakizungumza na Mtandao huu kwa nyakati tofauti huku wakiomba majina yao kutotajwa mtandaoni kwa madai kwamba bado wanategemea kupata huduma hiyo nchini humo, wamesema kwamba tangu mzozo huo ulipoanza wamekuwa wakipata huduma hiyo kwa shida tofauti ya siku za nyuma,
"Tangu mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyassa tumekuwa na wakati mgumu wa kupata huduma ya afya  kwa sababu baadhi wataalaam wa afya nchini humo hawataki kutuhudumia kwa wakati kwa madai kwamba hivi sasa nchi zetu hazina mahusiano mazuri kutokana na mzozo huo"aliema mama mjamzito ambaye ni mkazi ya kijiji cha Ikumbilo.
Ramani ya TanzaniaAkizungumzia sababu za wao kwenda kutafuta huduma ya afya nchini humo alidai kwamba ni kukiukwa kwa sera ya Afya ya mwaka 2007 inayosema kwamba wajawazito nchini Tanzania watapewa huduma za afya bure.
"Sera hiyo imekiukwa katika Hospitali za Wilayani Ileje Mkoani Mbeya,ndiyo maana baadhi ya wajawazito wilayani Ileje wanaacha Zahanati, vituo vya Afya na Hospitali Wilayani humo na kuvuka mpaka hadi nchi jirani ya Malawi kufuata huduma bora, tumekuwa tukivuka mpaka huu kwa miaka mingi,mfano mimi mwenyewe ninawatoto watano hivi sasa na wote nimewaza nchini Malawi"alifafanua mjazito mwingine.
Wajawazito hao wanatoka kata za Bupigu, Itumba na Isongole na wnakwenda nchini Malawi kwa wingi ili waweze kujifungulia huko na kupata huduma nyingine za afya.
Kutoka Isongole hadi Hospitali maarufu ya Chitipa nchini Malawi ni umbali wa kilometa 45, wakati umbali wa kwenda Hospitali ya Serikali ya Ileje ni kilomita tatu tu. Mwanamke moja mkazi wa kijiji cha Ikumbilo, kata ya Chitete wilayani Ileje, aliyejitambulisha kuwa anaishi na virusi vya ukimwi (VVU) anasema aliwahi kujifungulia Hospitali ya Chitipa na mpaka sasa anapata matibabu yake huko. Wilaya ya Ileje ina Hospitali kubwa mbili – Hospitali ya Serikali mjini Ileje na ile ya Misheni ya Isoko.ambapo ndizo Hospitali ambazo zinategemewa kwa huduma ya uzazi.
CHANZO-HABARI MPYA.COM

No comments:

Post a Comment