Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga akimkabidhi Mwenyekiti wa
Jumuia ya watumia maji wa Bonde la JUWAMALU Christian Matembo
cheti baskeri nne zenye jumla ya thamani ya shilingi 660,000 kwenye
ukumbi wa Hoteli ya Mbicu wilayani hapo.(picha na Joyce Joliga,Mbinga)
WAKAZI wa Bonde la Mto Luwaita wilayani mbinga wameonywa kuacha
vetendo vya kufyatua matofari na kujenga nyumba kwenye kingo za mito
ili kuzuia uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa maji kwani wakikamatwa
wanafanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria .
Onyo hilo limetolewa jana kwenye ukumbi wa Hoteli ya Mbicu na
Afisa maji bonde la ziwa Nyasa toka makao makuu Tukuyu Witga
Nkondora wakati wa uzinduzi wa Jumuia ya watumia maji wa bonde la
JUWAMARU wilayani Mbinga.
Amesema,bado kuna changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili katika
utunzaji wa bonde hilo ambapo kuna baadhi ya wananchi wamepimiwa
viwanja katika kingo za mito ,kitu ambacho kinarudisha nyuma malengo ya
huifadhi wa bonde hilo.
Ameongeza kuwa,mbali na wananchi kupimiwa viwanja maeneo ya kingo
za mito pia wapo ambao wanafanya shuguli za kufyatua matofali, kulima
ndani ya vyanzo vya maji hivyo kuharibu mazingira.
"Tumejipanga kuhakikisha watu wote ambao wanafanya uharibifu kwenye
vyanzo vya maji wanachukuliwa hatua za sheria ilikuweza kudhibiti
tatizo la uharibufu wa mazingira katika mabonde ,"alisema Nkondola
Awali akizindua Umoja wa watumia maji , Mkuu wa wilaya ya Mbinga
Senyi Ngaga amewatataka wakazi wa bonde hilo kulitunza bonde hilo ,na
kufanya kazi ya kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa uadilifu na
uhaminifu mkubwa .
Natambua kazi iliyopo ,mbele yetu ni kubwa na ngumu ,bado wilaya
yetu inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya uharibifu wa mazingira
,naomba tufanye kazi hii kwa umakini, uzalendo na kwa uadilifu mkubwa
iwapo tatutunza vyanzo hivyo vizuri raslimali hiyo itakuwa
endelevu, "alisema Ngaga
Aidha ,ameongeza kuwa serikali ipo pamoja na wananchi na itaendelea
kushirikiana nao ili kuhakikisha malengo ya uhifadhi wa mabonde ya maji
na vyanzo vya maji yanatunzwa na kulindwa kwa manufaa ya jamii nzima na
vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment