MSANII
nyota wa filamu Juma Kilowoko “Sajuki” aliyefariki leo alfajiri, atazikwa kesho
kutwa kwenye makaburi ya Kisutu.
Na Mhaiki Andrew, Songea
WASANII wa vikundi vya waigizaji katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameungana na familia ya marehemu Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki wakati wa mazishi yake kwa kushiriki katika kuomba dua na sadaka nyumbani kwao Bombambili mjni hapa.
Wasanii hao waliongozwa na Katibu mkuu wa chama cha wasanii katika fani ya waingizaji, Shukuran Faraja(Roma) ambao walikwenda nyumbani kwa familia ya Sajuki kutoa pole kwa ndugu na jamaa ya familia hiyo wakati wa mazishi ya mziba wa msanii huyo aliyefariki na kuzikwa katika makaburi ya kisautu jijini Dar es Salaam juzi.
Wasanii hao pamoja na kusoma dua nyumbani kwao waliweza kuwatuma wenzao wawili kuhudhuria mazishi ya msanii huyo Asha Jaffari(Saidati) na Mohamed Mkawa(Fungafunga) wakiwa na ubani wao wa Sh 115,000 fedha ambazo zilitokana na michango ya wasanii hao kwa lengo la kumwenzi mwenzao aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu bila ya mafanikio.
Alisema pamoja na michago yao hiyo bado wameweza kuahidi kuendelea kuchangisha fedha zaidi kwa lengo la kumwenzi wasanii hao pamoja na wale wachanga ambao wanaibukia katika tasnia hiyo ya usanii nchini kama kuwatia chachu waliendelee katika kulitangaza Taifa letu
Mmoja wa wanafamilia hao ambaye shangazi ya marehemu, Sajuki , Hawa Kilowoko aliwashukuru wasanii hao kwa umoja wao walionyesha katika msiba wa mwenzao na amewaomba waendelee na umoja huo kwa wasanii wengine itajitokeza.
Hata hivyo Mama mdogo wa marehemu, Sajuki, Mariamu Dizumba pia aliwashukuru wasanii hao kwa kuwaomba na kusema mchango huo usiwahusishe zaidi wasanii wakubwa kwa wale wenye majina na badala yake waelekeze nguvu hizo hata kwa wasinii wachanga wanaochipukia.
Mmoja wa wasanii hao, Issa Bakari(Big) aliwataka wananchi wawe na mwamko wa kuchangia wasisubili matatizo yanapojitokeza katika kuinua tasnia ya filam pamoja na kuwakumbusha wasanii maarufu waache tabia ya kujisahau kurudi kwao ili waweze kutambulika kwa jamii na wasisubili matatizo yanapowakuta ikiwemo kifo

No comments:
Post a Comment