WAKULIMA RUVUMA WAPATA HASARA YA SHILINGI MILIONI 300 KWA
KUTUMIA MBOLEA ISIYOKUWA NA VIWANGO
Na Joseph Mwambije,
Songea
BAADHI ya wakulima Mkoani Ruvuma wamepata hasara ya shilingi
milioni 300 katika misimu ya kilimo ya 2009/2010 na 2011/2012 kutokana na kutumia mbolea isiyo na viwango
na hivyo na wengine wameshindwa kusomesha na kufanya mambo mengine ya maendeleo.
Hayo yalibainika juzi wakati wa Ziara ya Mkurugenzi wa
Mamlaka ya kudhibiti ubora wa molea
Tanzania Dkt Suzane Ikera kukagua Magahala ya kuhifadhi mbolea na Vituo
vya kuuzia mbolea kwa mawakala kuona jinsi inavyohifadhiwa na ubora wake na
kujione athari walizozipata wakulima kutokana na kutumia mbolea isiyokuwa na
viwango.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo wa mbolea,Mkurugenzi wa Mamlaka
hiyo Mwenyekiti wa Chama cha msingi cha ushirika cha Chandamali Bw. Merius Ponera alisema wakulima
wake vijijini wamepta hasara kubwa kutokana na kutumia mbolea isiyokuwa na
viwango na hivyo wameshindwa kusomesha,kujenga kugharamia matibabu na kulipa
madeni.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa katika misimu miwili ya
kilimo wakulima hao walipatiwa mbolea toka Kampuni ya YARA ya Nchini Norway
ambayo ilipimwa na Shirika la viwango Nchini na kubainika kuwa haina viwngo na
hakuna hatua zozote zilizochukuliw kwa Kampuni hiyo.
Alisema wakulima waliokopa kwenye chama chake walishindwa
kurejesha mikopo yao kutokana na kupata hasara kwenye mazao yao na hivyo chama chake kwa ujumla kilipata hasara kubwa
kutokana mikopo kiliyotoa kushindwa kurejeshwa.
Kimsingi tunatakiwa tulipwe faini
kwa hasara tuliyoipata kutokana na mbolea isiyo na viwango tuliyopewa na kusababisha
wakulima wetu wapate hasara,alisema Bw. Ponera
Alibainisha kuwa Sakata la kupatiwa mbolea isiyokuwa na
viwango lina harufu ya rushwa kwa kuwa Makampuni makubwa ya mbolea yanahonga kwa Viongozi Serikalini
na kugawa mbolea isiyokuwa na viwango na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
Kwa upnde wake Dkt. Ikera alisema atafuatilia Suala hilo kwa kuwa Mamlaka yake kwa muijibu
wa sheria ya mbolea ya mwaka 2009 ina uwezo wa kushtaki ikibainika mbolea isiyo
na viwango imesambazwa kwa wakulima hatua zitachukuliwa ikiwemo kwa Kampuni
husika kutozwa faini.
Kwa upande wake Mkufunzi Mkuu wa kilimo na Mkaguzi wa mbolea
toka Wizara ya Chakula na kilimo Bi. Stella Mutagwaba alisema mbolea
isipotunzwa vizuri ubora wake unaharibika na kwamba inatakiwa isichanganywe na
kitu kingine hivyo wao wanaangalia madukani
na Bandarini zinatunzwaje.
Naye Mhasibu wa chama
kikuu cha Ushirika cha Songea na Namtumbo(SONAMCU) Bw. Nurdin Ponera alisema
wakulima katika Mkoa wa Ruvuma wamepata hsara kubwa kutokana na kutumia mbolea
isiyokuwa na viwango.
Katika ukaguzi wao Dkt Ikera anasema
wamegundua yafuatayo, kuwepo kwa uchakachaji wa mbolea kwa kuichanganya na na
chumvi,utunzaji mbaya wa mbolea kwa kuiweka chini na juani na kwamba Wakaguzi
Wasaidizi wa mbolea wa Wilaya na Mikoa wanatakiwa kuwaelimisha Mawakala kuhusu
utunzaji wa mbolea.
Mwisho
No comments:
Post a Comment