Na Amon Mtega ,
Songea.
MWENYEKITI wa umoja wa vijana wa CCM- UVCCM wilaya ya Songea mjini
mkoani Ruvuma Victor Ngonyani amewataka vijana waliofikisha umri wa kugombea
kwenye chama hicho kuchukua form za kuwania nafasi hizo bila
kuogopa ili kuongeza nguvu ndani ya chama hicho .
Wito huo umetolewa
jana na mwenyekiti huyo wakati akifunga kikao cha baraza la vijana UVCCM mjini hapa kilicho kuwa kikipitia majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali wa jumuiya hiyo toka ngazi ya kata kwa kuangalia
sifa zao ili yapelekwe ngazi ya chama tayari kwa uchaguzi .
Ngonyani alisema kuwa
baraza hilo ni lamwisho kwa uongozi uliyokuwepo kwa kuwa kanuni ya chama
inaeleza kuhusiana na umri wa kuitumikia jumuiya hiyo basi vijana sasa wenyeumri wa kuvuka kanuni ya UVCCM basi
ni ruksa kwenda kugombea kwenye chama .
“Vijana acheni kujenga uoga wakuchukua form za uongozi ndani
ya chama kwa kuwa chama hiki kinahitaji nguvu ya vijana ili kiweze kusonga
mbele kwa kuendelea kushika dola ndani ya nchi hii .
‘’Kama
kuna mtu wa ndani ya chama chama chako anakuletea vikwazo vya kukutaka
usichukue form ya kugombea uongozi basi ni heri ukagombana naye kwa kukinusuru
chama kisiangamie kwa kuwa mbele ya safari mtaelewana tuu chama kikiwa
kimenusurika’alisema mwenyekiti Ngonyani .
Alisema kuwa
viongozi waliyokuwepo ndani ya uongozi wa vijana ambao wanaomaliza mda wao
wasisite kuendelea kutoa ushauri wa miongozo ndani ya jumuiya hiyo kwa kuwa
babo wao ni viongozi wastafu .
Aidha baadhi ya
wajumbe wakichangia hoja mbalimbali baada ya kupitisha majina walisema kuwa
vijana wengi wanaingiwa na uoga wa kuchukua uongozi ndani ya chama kufuatia
changamoto ambazo hujitokeza,kwa baadhi ya viongozi kutowaunga mkono vijana.
MWISHO.
Baadhi ya vijana wakifuatila kwa makini hoja katika Kikao hicho cha mwisho kwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment