Saturday, August 25, 2012

CCM IRINGA KUPELEKA CHUONI KUPATA MAFUNZO ELEKEZI MAKADA WAKE KWENYE CHUO CHAKE

 Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Emanuel Mteming'ombe
 Bw. Mteming'ombe

 
Na Joseph Mwambije,
Iringa
CHAMA  cha Mapinduzi(CCM) Mkoani Iringa kinatarajia kupeleka Makatibu Kata 93 wa chama hicho waliochaguliwa hivi karibuni  kupata  Mafunzo elekezi  ya utendaji kwenye Chuo cha chama hicho Mkoani humo  ili kuondoa migogoro ndani ya Chama hicho.
 
Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Katibu wa Chama hicho wa Mkoa wa Iringa Bw. Emmanuel Mteming’ombe wakati akizungumza na Mtandao huu Mkoani humo.
 
Alisema Ukarabati wa Chuo hicho umeshakamilika na Wanatarajia kupeleka Makada Chuoni hapo kupata mafunzo ya wiki moja kuanzia Septemba 3 hadi Septemba 10 mwaka huu.
 
Katibu huyo wa CCM alisema hatua hiyo inalenga kuwapatia mafunzo elekezi  Viongozi wa Kata waliochaguliwa hivi karibuni katika chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 200 kwa mara moja.
 
‘Tunalenga kuwapatia mafunzo makatibu wapya  ili wajue kazi za utendaji wa Chama ili waweze kukijenga Chama na baada ya mafunzo hayo tutatoa mafunzo mengine kwa Makatibu wa Matawi kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Iringa’alisema Bw. Mteming’ombe.
 
Alifafanua kuwa Makatibu hao wa Kata wote ni wa kutoka katika Mkoa huo wa Iringa na baadaye kutafuatiwa na  mafunzo mengine  kwa  Makatibu wa Matwi toka  Wilya ya Njombe yatakayoanz Oktoba 3 hadi Oktoba 10 mwaka huu.
 
Bw. Mteming’ombe anafafanua kuwa mafunzo kwa Makatibu Kata yanatarajiwa kufunguliwa Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho,Mbunge wa Jimbo la Isimani na Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge Bw. Wiliam Lukuvi.
MWISHO
 

 Jengo la CCM Mkoa wa Iringa
Jengo la CCM  Mkoa wa Iringa.

No comments:

Post a Comment