Sunday, August 26, 2012

MWANAMKE ALIYEMTUMPA MTOTO WAKE JALALANI ATIWA MBARONI


MWANAMKE ALIYEMTUMPA MTOTO WAKE JALALANI ATIWA MBARONI

Na Cresensia Kapinga
Songea
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limemtia mbaroni mwanamke aliyedaiwa kutupa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi mitano kwenye jalala la takataka lililopo katika eneo la mtaa wa Majengo katika halmashauri ya manispaa ya Songea. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani humo Deusdeti Nsimeki alisema kuwa mwanamke Zawadi (18) wa mtaa wa Majengo alikamatwa juzi  majira ya saa za usiku kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa amejificha uvunguni mwa kitandaakiwa analengo la kuukimbia mkono wa dola.

Kamanda Nsimeki alisema kuwa Bi. Zawadi baada ya kukamatwa na kuhojiwa kuwa kwa nini aliamua kumtupa mtoto na kukimbia alisema kuwa alikuwa amedanganywa na mwanaume ambaye hakumtaja jina kuwa amtupe mtoto alafu wafunge ndoa kisha waende Mbeya wakaendelee na maisha yao.

Alieleza zaidi kuwa awali alipohojiwa na polisi alisema kuwa alikuwa anakimbizwa na kichaa kitendo ambacho kilimfanya amtupe mtoto wake lakini alipobanwa zaidi ndipo alipokiri na kubainisha zaidi kuwa alikuwa ameingia kwenye dimbwi la mapenzi ambalo alidai kuwa angefanikiwa kumtupa mtoto wake maisha yake ya ndoa yangekuwa mazuri zaidi.

Alifafanuwa zaidi kuwa Polisi baada ya kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo badinaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na kwamba hali ya mtoto inaendela kuwa nzuri na hivi sasa kuna msamaria mmoja amejitokeza kumlea.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani wakati wowowte kuanzia sasa mara tu upelelezi utakapokamilika ili sheria iweze kuchukuwa mkondo wake.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment