Sunday, August 26, 2012

MADIWANI NA WATENDAJI WA ASERIKALI WATAKIWA KUJIBU KERO ZA WANANCHI



Na Muhidin Amri
Songea
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka watendaji wa serikali,na madwani mkoani humo kujibu na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Mwambungu aliyasema jana ofisini kwake mjini songea wakati akizungumza na na Mtandao huu kuhussiana na ochangamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mkoa huo.

Alisema wananchi wanamatarajio makubwa ya kuona hali ya maisha yao yanabadilika hasa baada ya Rais Jakaye Kikwete kufanya mabadiliko makubwa serikalini ikwemo ya kulibadili baraza la mawaziri na makatibu wakuu wa wizara mbali mbali.

Mwambungu alisema wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili kila siku ambazo zinapaswa kupatiwa majibu ni kazi ya watumishi wanazipatia majibu chaangamoto hizo na kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu shughuli zote za kimaendeleo zinazofanyika.

Alitolea mfano suala la pembejeo za ruzuku ambalo limekuwa katika baadhi ya maeneo likilalamikiwa ma wananchi pengine kutokana na kutotekelezwa vyema na baadhi ya mawakala hivyo sasa linapaswa kusimamiwa kwa ukaribu zaidi ili kuepusha malalamiko.


Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi wa mkoa huo kushirikiana na viongozi wao katika kujiletea maendeleo na kwamba wajitokeze kwa wingi katika kuchangia nguvu zao kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili hatimaye iweze kuwanufaisha wao wenyewe.

                            MWISHO.

No comments:

Post a Comment